Alex Sanchez akishangilia goli alilofunga kati ya mawili.
Kwa mara ingine tena, Mesut Ozil ndiye aliekuwa akivuta kamba zote na kuwarahisishia kazi Alexis Sanchez na Alex Iwobi.
Mwamuzi Roger East akimwonyesha kadi nyekundu beki wa Hull City Jake Livermore baada ya kuunawa mpira ndani ya eno la 18.
Granit Xhaka nae akifurahia goli alilofunga na mshambuliaji Lucas Perez.
Kitu kingine nilichoona leo Wenger hakuanza na Perez kule mbele bali aliamua kuanza na Theo Walcott ambae alileta matatizo kwa ngome ya Hull hadi alipotolewa Livermore, ila kwa ujumla kikosi kilikuwa safi khasa katikati ambapo Coquelin, Cazorla na Xhaka walitawala
.