Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mimi nimeshawazowea baadhi ya washabiki wa Arsenal , aliposajiliwa Welbeck kuna waliomuita ni next Henry kwamba anaumaliziaji mzuri kuliko Giroud. But tangu ahamie Arsenal sikumbuki Welbeck kufunga magoli mengi zaidi ya Giroud regardless Welbeck injuries issues sidhani kama ni mfungaji mzuri. Tusubiri tuone Lucas atakuwaje
 
Ni kweli mbna giroud alikua mfungaji bora kwao lakini alikutana na yapi??
 
Giroud alikua mzuri toka kwao sio kama ilivyo pale emirate kingine ni ligi tofauti kaka
 
I hope Perez to prove me wrong. Lakini sitegemei miujiza toka kwake. Ligi ya England ipo tight sidhani kama atapata nafasi za kukimbia na mpira kama inavyoonekana alivyofanya Spain.
 

Samir Nasri amesajiliwa na Sevilla kwa mkopo.

Wilfried Bonny anazungumza na Stoke City hivyo kuweza kusababisha dogo Saido Berahino kubakia West Brom.

Ikumbukwe Berahino ambae ana asili ya Burundi ana shida sana na meneja Tony Pulis ambae anataka kuhakikisha kijana huyo hafiki mbali kimpira.

Mario Balotelli kuhamia timu ya Nice, hivi sasa anazungumza nao.

Joe Hurt amejiunga na Torino ya Italy kwa mkopo.

Moussa Sissoko anajiunga na Tottenham ambao wamemuachia Nacer Chadli kwenda West Brom.

Jack Wilshere huenda akajiunga na Roma akacheze na kipa wa Arsenal Cheza -Wojciech Szczesny.

Islam Slimani tayari amejiunga na Leicester City.

Waliobakia ni Kone, MacCarthy, Berahino na Sakho.
 
Vipi kuusu daniel sturridge naona kuna dalili za kumnyakua dk za mwisho
 
Wilshere already making important research about life in Italy

Jack Wilshere anafanyiwa medical Bournemouth.

Anakwenda kucheza na mchezaji mwenzie Benik Afobe ambae aliwahi kuchezea Arsenal huko nyuma.


Jack Wilshere akiwa Bournemouth atacheza na mchezaji mwingine wa zamani wa Arsenal Benik Afobe ambae ni mshambuliaji wa timu hiyo ya pwani ya Dorset kusini mwa Uingereza.

Afobe ni rafiki yake wa karibu Jack Wilshere na walianza kuchezea Arsenal wakiwa na umri wa miaka 5 na ndiye aliemshawishi Jack kwenda Bournemouth.
 
Usajili Updates: Eliaquim Mangala aenda Valencia kuziba pengo la Mustafi:

Eliamquim Mangala ndiye aliekuwa alichelewesha usajili wa Chkodran Mustafi kwenda Arsenal kwa kiasi kikubwa ambacho Man City wanataka na mshahara wake.

Mangala atakaa Valencia kwa msimu mzima wa 2016/17

Wakati huohuo beki wa zamani wa Arsenal Phillipe Senderos amejiunga na timu ya Rangers ya Scotland kwa mkataba wa mwaka mmoja.



Itakumbukwa Senderos alikuwa mmoja wa mabeki watano wa Arsenal ambao hawakuwa na uwezo kabisa wa kuhimili mikikimikiki ya ligi kuu akiwa na wezake Johan Djourou, Sebastien Squillaci, Andre Santos na kipa Manuel Almunia.
 

Dogo Gnabry kauzwa W.Bremen,kila heri dogo uko uendako natamani kuwe na buy back clause kwenye mkataba wake.
 

Duh kila la heri JW10 naamini utarudi home muda ukifika hii ni habari mbaya kwangu kwenye dirisha la usajili safari hii.
 
Nasikia Benzema anataka kuondoka Real Madrid. Wenger yupo simuni....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…