Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

skysports_3550634b.jpg

Tunae legend Thiery Henry

Haya Team news:

Arsena wanaanza bila Mesut Ozil na Alexis Sanchez.

Mesut Ozil hayupo hata bench.

Mohamed Elneny yupo kwenye bench.

Sasa timu zenyewe:

Arsenal- Kipa Cech, Kulia Bellerin, Kushoto Monreal na mabeki wa kati ni Boss na Mertesacker.

Katikati kuna Flamini, Ramsey, pembeni kulia Joel Campbell pembeni kushoto yupo Walcott. Alex Oxlade Chamberlain anaziba nafasi ya Mesut Ozil na mbele kuna Olivier Giroud.

Bench lina kipa Ospina, Gibbs, Mohamed Elneny,Gabriel, Arteta, Alex Iwobi, na Calum Chambers.

Stoke City wana: Butland, Johnson, Shawcross, Wollscheid, Pieters, Whelan, Afellay, Walters, Krkic, Arnautovic na Joselu.
 
Asante sana kwa utangulizi mzuri mkuu,,,,vp uonavyo ww leo tutatoka kweli!?
 
Kaka kuna live streaming ya kuchek hii game nipo mbali na banda umiza
 
Habari zinasema kwamba Mesut Ozil yupo nje anauguza maumivu ya mguu. Hio inawesekana ikawa mbinu ya kumpumzisha kusubiri mechi na Chelsea wiki ijayo.
 
Mkuu Richard hebu fanya mambo niichek hii game kwenye kadevice kangu mana npo road nw
 
Mwamuzi wa mchezo wa leo anaitwa Craig Pawson ambae ni mkazi wa mji wa Sheffield. Ni kijana ambae ana umri wa miaka 36.

Hopefully atakuwa mwangalifu na mechi hii myhimu kwa kila moja ya timu hizi.

Mwamuzi huyu kijana amekuwa mwamuzi wa akiba katika mechi mbili za Arsenal kwenye kombe la FA ile dhidi ya Wigan mwaka 2014 na ile dhidi ya Aston Villa mwezi Mei mwaka jana ambapo Arsenal ilishinda mechi zote mbili na kunyakua kombe hilo.
 
Asante sana kwa utangulizi mzuri mkuu,,,,vp uonavyo ww leo tutatoka kweli!?

Stoke wamedhamiria kufanya mashambulizi ya nguvu dakika za mwanzoni hasa zile ishirini.

Arsenal watataka kucheza mtindo wa 4-3-2-1 na watakuwa wakifanya counter attack.

Mimi nafikiri kutakuwa na magoli Zaidi ya moja na inaweza kuishia Arsenal 2 Stoke 1
 
Timu ndio zaingia uwanjani. Arsenal wakiwa na jezi yao ya ugenini ya rangi la dhahabu na mistari myembamba na bukta za bluu iloiva.

Stoke wana jezi za rangi nyeupe zenye mistari ya rangi nyekundu huku wakiwa wavevaa chini bukta nyeupe.
 
Prof anacheza na hawa Potters anawafahamu vizuri sana, Mesut mpira kama huu hafai watamuumiza bure na hilo ndilo Le Prof kaliona. tutakomaa nao tu leo.
 
Prof anacheza na hawa Potters anawafahamu vizuri sana, Mesut mpira kama huu hafai watamuumiza bure na hilo ndilo Le Prof kaliona. tutakomaa nao tu leo.

Ni kweli kabisa.

Na mzee amethibitisha kwamba kijana anapumzika.

Walters anampiga kiatu Walcott na anapona kupewa kadi ya njano.
 
Good game kwa vijana nao wanapiga kiatu cha hapa na pale Flamini amefanya kwa Anaurtovic.
 
Dah leo kivumbi. No Sanchez no Ozil... Nevertheless COYG!!!!!
 
_87757562_stoke_city_getty.jpg

Kama inavyoonekana hapo juu kifuu cha snow ... ... ... kimelundikwa.
Mtanange umeanza mi mkali sana na rafu za hapa na pale
Rambo anazomewa kama kawa, ..... .... (very unsports).
 
Arsenal wanatawala mchezo dakika hizi 5 za kwanza.

Mashabiki wa Stoke wanapiga kelele sana.

Arsenal wana Ramsey, Chamberlain na Campbell ambao wapo nyuma ya Olivier Giroud.

Dakika inakwenda ya 7 Arsenal 0 Stoke 0
 
Back
Top Bottom