rubaman
JF-Expert Member
- Sep 10, 2011
- 4,983
- 3,084
Jamani eeh tusianze kumsifia huyu dogo kabla hatujaona anachezaje. Wengi wetu tumemsikia juzi juzi na clips za youtube haziwezi kuwa proof ya kuwa jamaa ni mzuri kama Patrick Vieira au sijui nani. Wapenzi wengi wa Arsenal navyowajua hamkawii kulalamika kuwa Wenger kaingia mkenge kwa kununua mchezaji huyu au yule. Miaka yote tunasikia jinsi watu wanavyowatukana kina Flamini, Arteta, Giroud etc, muda Fulani ilikuwa kina Ramsey, Wilshere. Msimu huu sijasikia mkimtukana Giroud sababu anafunga magoli karibia kila mechi. Tusubiri tuone itakavyokuwa baada ya mechi kama 6 au 10 atakazocheza ndio tutoe verdict.