Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

So far so good na Arsenal wanatawala mchezo kwa asilimia 73 huku Stoke City wakiwa wanacheza ndani ya eneo lao.

Dakika inakwenda ya 21
 
May be Arsenal players think that a match can be won on shots on target basis....Score goals dammit.
 
Arsenal walitakiwa wawe wanaongoza kwa magoli 3 au hata 4 kwa uchezaji wao na kutawala mchezo.

COYGs!
 
Stoke City wamshukuru Butland kwa kupangua shuti la Coscielyn na Cazorla na sasa ni kona

Dakika inakwenda ya 29
 
Goooooooooooal Arsenal Theo Walcott

Arsenal 1 up

Hii ilikuwa ni counter attack ya Arsenal, Francis Coquelinn aliuzuia mpira katikati ya eneo la Arsenal akatoa pasi ndefu kwa Mesut Ozil ambae alimpasia Theo Walcott na Theo bila wasiwasi wowote ule akamalizia kazi hio.

Goli limefungwa dakika ya 31
 
Mesut Ozil anapewa kadi ya njano kwa kumvuta shati beki Eric Pieters
 
Na mwamuzi sasa anapuliza kipenga tunakwenda mapumziko kwa dakika 15

Arsenal 1 Stoke City 0

What a pass kutoka kwa Ozil kwenda kwa Theo Wlacott ambae akaenda kufunga!
 
Ni goli la kwanza kwa Theo Walcott ndani ya Emirates na kwa kweli inabidi Arsenal waendelee na mtindo wa counter attack kama Stoke City wataendelea na kujaza basi.

Pia Stoke City inabidi kumshukuru kipa wao Jack Butland ambae amezuia mipira mingi isiingie nyavuni kwa kupangua mashti ya Coscielyn na Alexis Sanchez na Ramsey.
walcott_3437829b.jpg


Walcott akishangilia goli la kwanza
 
Ramsey is killing our game upfront. Should not come back after the break.

Usiwe na wasiwasi Alex Oxlade Chamberlain yupo nje anasubiri, pia wapo Giroud na Arteta pia wanaweza kuja kipindi cha pili.

Ukumbuke ni wachezaji hawahawa juzi tu walikuwa kwenye mechi za qualifiers.
 
Timu zinaingia uwanjani kuja kumalizia ngwe ya pili.

Na kama ilivyo kwenye msimamo wa ligi hivi sasa Arsenal inashika nafasi ya tatu, Stoke City nafasi ya 18 na Chelsea sehemu Fulani palepale chini kwenye msimamo huu.
 
Back
Top Bottom