Kati ya watu wa ukweli wa soka kwenye jukwaa la sports hapa JF, wewe ni mmoja wa watu hao.
Morgan ni mashine inayofanya kazi ambayo watu wasio wa soka hawawezi kuiona na kuielewa kazi yake.
Saluti pia kwa kuwa muwazi na kukubali kile dogo Oxford alichokifanya kwa Masoud.
Chifu, saluti kwa kuongea kama mpenzi wa soka, na siyo mnazi wa klabu ya soka.
Ahsante mkuu mimi napenda mpira na Arsenal ni timu nnayoipenda sana.
Ila mimi sikucheza sana mpira lakini nnacho kipaji cha kuchambua wachezaji na hivi karibuni nimejiunga na mascouts walio na kazi ya kutafiti wachezaji.
Tatizo wachezaji wa kutoka Afrika kwa sasa ni vigumu sana kupenya labda waende kwa mpangp wa baadhi ya watu walio na connections kwenye timu za Ulaya.
Lakini kwa muda wote ambao nimeishi katika bara la Ulaya nimejifunza u-scout wa kutafuta vipaji vya wachezaji.
Hivyo nikiwa uwanjani pamoja na kwamba naisupport Arsenal lakini pia huwa naangalia new edition against the established na ndio kilichotokea leo.
Dogo Reece leo ndio ilikuwa ndio mechi yake ya kwanza ya ligi kuu ya Uingereza na ameonyesha kwamba anaweza kukabiliana na watu kama Ozil pale kwenye kiungo.
Pia leo yeye alikuwa ndie DM wa West Ham.
Ukuzaji wa vipaji na ukaviendeleza ndio njia pekee ya kuwa na timu imara yenye wachezaji walozoeana.
Lakini ikifika wakti fulani unatakiwa uangalie na uzoefu pia na juzi tu Henry amemwabia Wenger kwamba Giroud sio mmaliziaji mzuri na inabidi Wenger amsajili Benzema, amemwambia ukweli bosi wake wa zamani.
Hivyo kama kweli Benzema yupo London hivi sasa, basi atakamilisha usajili wiki hii.