Transfer Updates.
Wakuu mambo yanafanywa kwa siri sana na wachezaji mmoja au wawili watatangazwa kabla ya muda wa usajili kwisha,
Ila katika orodha niliyoweka ya wale watano, inaonekana Llorente ndie amepatikana na anakuja kama back-up kwa Olivier Giroud na Juventus wamekubali paundi 10milioni.
Hata hivyo tunawatakia kila la kheri wachezaji kadhaa ambao wameenda kuchezea timu zingine barani Ulaya.
Wojciech Sczzesny amekwenda timu ya Roma ya Italy kwa mkopo wa msimu mmoja.
Abou Vasiriki Diaby amekwenda nyumbani France ambapo atakuwa akichezea timu ya Olympic de Marseille. Diaby amekataa kuchezea timu za West Brom Albion na Liverpool ambao ni wapinzani wa Arsenal kwenye ligi kuu.
Pamoja na hawa kuna wachezaji wengine kama Ryo Miyaichi ambae amekwenda kuchezea timu ys St Pauli ya daraja la pili huko Germany.
Yaya Sanogo amekwenda Ajax Amstredam ya Holland kucheza kwa mkopo.
Mathieu Flamini amekwenda Garatasaray ya Turkey bila sda yoyote.