Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

243C3F8900000578-2884363-image-a-2_1419326311354.jpg


Theo na mkewe wanakula x-mass .... .


243B039900000578-0-image-a-31_1419288482176.jpg


Mesut Ozil alikuwepo ... ..


243AE24D00000578-0-image-a-32_1419288487711.jpg


OG na mum sap wake .... .... .

243B1A7D00000578-0-image-a-33_1419288750298.jpg


Germany contigent .... .

2015 kitaeleweka tu #COYG
 
............hivi Top Four yetu tutaikamata kweli msimu huu?

Chelsea, Man City, Man United hawawezi drop points nyingi compared to us,
wakati huo huo "chasing pack" iliyokuwa na Everton na Spurs pekee msimu ule,
safari hii kuna West Ham na Southampton pia.
:coffee:

Cc; BAK, Richard, Balantanda, Sizinga, Wandugu Masanja, Wacha1, piere.fm, rubaman....et al

Mkuu Mbu binfsi naamini bado tuna nafasi ya kuwa higher than 4th place na bado naamini kuanzia january mambo yatakuwa mazuri na hasa ukizingatia licha ya majeruhi waliopo kurejea lakini pia babu wenger katoa ahadi kuwa lazima ataingia sokoni, so matumain yangu kuwa dirisha likifunguliwa tutapata CB na DM. So wewe endelea kupata ghahawa bila wasi wasi.
#COYG .
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Mie naamini tutaikamata na pia tunaweza kuwa juu zaidi. Naamini hivi kwa sababu majeruhi wetu wote watakuwa available kuanzia January 2015, hivyo kama tutaweza kuhakikisha tunashinda mechi 15 kati ya 19 za ngwe ya pili ya msimu huu basi tutajiweka katika nafasi nzuri sana ya kuwemo kwenye top 4 or even higher than 4th position.

#InGunnersWeTrust

Kushinda game 15 ngwe ya pili hicho kitu hakiwezekani. Mtapoteza kwa hizi zilizopo top 3 kwa sasa. Kisha mtatolewa kijasho na down 4 kwa wakati huo. Kisha mta draw na zile zenye kiwango chenu, hizi ni pamoja na spurs, Everton, soton na west ham. Zilizobakia mnaweza kushinda.

Hii maanake ni top 4 Hamna na ni sababu tosha ya kumwonyesha mzee wenga mlango wa kutokea...jeuri hiyo mnayo?
 
140710062820_sergio_ramos_spain_tatoo_624x351_bbc_nocredit.jpg




Huyu Ramos baada ya kusikia tetesi kwamba wenga anamtaka akachora hiyo tatoo mguuni sijui alimaanisha nini
 
Ramos amewahi kubeba Hayo makombe yote mawili! Wenger sio saizi ya Ramos! Ramos hafikirii EPL tu!
 
............hivi Top Four yetu tutaikamata kweli msimu huu?

Chelsea, Man City, Man United hawawezi drop points nyingi compared to us,
wakati huo huo "chasing pack" iliyokuwa na Everton na Spurs pekee msimu ule,
safari hii kuna West Ham na Southampton pia.
:coffee:

Cc; BAK, Richard, Balantanda, Sizinga, Wandugu Masanja, Wacha1, piere.fm, rubaman....et al

Mkuu, kwanza kheri ya Xmas.

Uwezekano wa Arsenal kuwemo kwenye "top four" upo na unaweza kuwepo kwa matokeo ya ya ushindi kwenye mechi za Arsenal dhidi ya QPR,West Ham na Southampton.

Baada ya hapo Arsenal itakuwa na points 39 na kama inavyozungumzwa tutafanya usajili wa beki, mshambuliaji na mchezaji wa kiungo.

Katika wachezaji hawa nafasi mbili za beki wa kati na kiungo mkabaji ndizo nafasi zenye kupewa kipaumbele maana ALex Song atatuonesha ujasiri wake tutapocheza na West Ham Jumapili ijayo.

Zaidi ya hapo kuna habari za ndani kabisa kwamba Arsenal watasajili mshambuliaji kwa sababu Lucas Podolski anatakiwa na Inter Milan ya Italy na kwa vile nafasi yake imekuwa adimu kwenye first 11 basi anataka kuondoka.

Pia Yaya Sanogo atapelekwa kucheza kwa mkopo kwenye moja ya timu za kwenye PL na hivo kupata uzoefu wa mikikimikiki ya PL.

Hivyo basi ifikapo mwezi ujao tarehe 1 dirisha la usajili litakapofunguliwa kuna wachezaji kadhaa ambao huenda wakasajiliwa na Arsenal - Moussa Sissoko kutoka Newcastle, ambae atasaidia sehemu ya kiungo ambayo ina Mikael Arteta na Mathieu Flamini ambao siku zao za uchezaji zinakaribia mwisho.

Katika mechi na Liverpool Flamini aligundulika kuwa the "weakest link" na kugeuzwa kuwa "windsreen wiper" kuwalinda Philipe Coutinho na Adam Lallana na mpaka mwisho Liverpool wakapata goli la kusawazisha.

Hali hio ni lazima mzee Wenger atakuwa aliiona na ataifanyia kazi kumsajili Sissoko ambae ana miaka 25 na atakuwa ndio Patrick Vieira.

Mwingine ni Paulo Dybala kutoka Palermo ambae atasaidiana na Giroud na Danny Welbeck ambao ndio watakuwa washambuliaji rasmi wa Arsenal baada ya Podolski na Yaya Sanogo kupisha. Dybala anagharimu kama paundi milioni 20 hivi na hizo si nyingi kwa Arsenal kama wanataka kuepuka Europa League.

Mchezaji mwingine ni Sergio Ramos wa Real Madrid ambae amekataa kuongezewa mkataba muda si zaidi ya miaka miwili na inasemwa kwamba wakala wake amewasiliana na Arsenal. Ramos atasaidia sana sehemu ya ulinzi ambayo imepwaya sana.

Morgan Schneiderlin ni mchezai mwingine ambae Arsenal wanaweza kufanya usajili wa kueleweka kwani walikishazungumza na mchezaji huyo mwezi julai mwaka huu lakini timu yake ya Southampton ikamkatalia kuondoka.

Schneiderlin ni mrefu mwepesi na ana nguvu za kukabiliana na wachezaji wengine wa kiungo wa ligi ya Uingereza.

Hivo basi ushindi pekee katika mechi zijazo ndio njia pekee ya kuepuka muanguko mkuu ifikapo tarehe 1 Januari mwaka 2015.
 
Hii inahusu mashabiki wa Gunners nafahamu #Mburukenge watavamia tu, wakuu nafahamu wengi mmekula sikukuu kwa ya X-mass kwa sherehe na mbwembwe kibao hongereni kwa hilo. Kuhusiana na mambo ya soka prof yupo Gado anawafunda vijana kama kawa, Thiery Henry anaanza u-pandit na Sky .... ..... .... yaani 2015 looks more brighter than before, wachezaji wengi majeruhi ndio kwanza wanarudi na ile hang-over ya world cup ndio kwanza inaisha ... ... ... tupo kwenye kinyang'anyiro cha CL, EPL na FA cup. Nafahamu wengi hawatupi nafasi lakini sina wasi wasi na timu yetu, vijana wapo imara, Prof ana imani na wachezaji wake 100%. Kesho oops leo baadaye kidogo tutakwaana na QPR Emirates Stadium ni timu ya London hivyo tegemea mchezo utakuwa mkali sana .... .... .... .#COYG
 
Nafasi ya nne ni ya Arsenal. Wengine wanapoteza muda tu.

Mkuu, hii siyo nafasi ya kujisifia hata kidogo.... Tunataka silverware pale Emirates, nafasi ya nne is for losers and we should not always be losers!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
BINAFSI SINA WASIWASI NA ARSENAL...HASA NIKIANGALIA REKODI ZAKE ZA NYUMA NA THE WAY TULIVYO SASA....KAMA UNAKUMBUKA 2010/2011 VAN PERSIE ALIIKOKOTA TIMU FROM THE BOTTOM TUKAKWEA MPAKA NAFASI YA 4 (Jina la Van Magoli ndo lilipoanzia), HAWA AKINA OZIL & Co wakirudi tu January, tutaanza kuwaza UBINGWA.( Mark My Words) Mbu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, hii siyo nafasi ya kujisifia hata kidogo.... Tunataka silverware pale Emirates, nafasi ya nne is for losers and we should not always be losers!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app

Hii hali ya kila msimu kugombea kuwepo katika top four tumeichoka sasa. Ni wakati sasa wa kuchukua hii ndoo ya epl. Nadhani mwezi ujao wenger atafanya utaratibu wa kurekebisha kikosi.
 
140710062820_sergio_ramos_spain_tatoo_624x351_bbc_nocredit.jpg




Huyu Ramos baada ya kusikia tetesi kwamba wenga anamtaka akachora hiyo tatoo mguuni sijui alimaanisha nini

Hovyooo . Misinformation. Jamaa alizipata hizo tats kusheherekea ushindi wa UCL na World Cup mwezi wa May, 2014.
 
BINAFSI SINA WASIWASI NA ARSENAL...HASA NIKIANGALIA REKODI ZAKE ZA NYUMA NA THE WAY TULIVYO SASA....KAMA UNAKUMBUKA 2010/2011 VAN PERSIE ALIIKOKOTA TIMU FROM THE BOTTOM TUKAKWEA MPAKA NAFASI YA 4 (Jina la Van Magoli ndo lilipoanzia), HAWA AKINA OZIL & Co wakirudi tu January, tutaanza kuwaza UBINGWA.( Mark My Words) Mbu

Kwa kujifariji tu, siwawezi! Kwa hiyo, timu nyingine zitakuwa zinawasubirini tu?!?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom