We didnt spend "Big" in January...huenda ikawa ni sababu ya kuukosa ubingwaKumekucha, pamoja na kupata droo ktk mechi ya jana, kidogo nimefarijika maana tungekua na wakati mgumu zaidi iwapo tungepoteza hii mechi. Lazima tukubari kua tumekua na matokeo mabaya dhidi ya Man UTD kwa muda mrefu sana. Kuhusu ubingwa kweli bado itategemea mipango ya Mungu kwa maana timu ya ubingwa inatakiwa ishinde zile mechi ngumu hususani waliopo big four kwa kasi hii sidhani kama tutaweza kumpiga Chelsea au Man City.
Thanks Gunner.
what a terrible game!
Nilisema mapema kuwa, kuwakosa Aaron Ramsey na Theo Walcott ni pigo kubwa sana kwetu kwa sababu hawa walikuwa mpaka wanamfanya hata Olivier Giroud aonekane ni mshambuaji hatari wakati kiuharisia ni average player ambaye hawezi hata kwenda na playing style ya Arsenal. Slow, dreadful first touch, immobile....
Kukaa hapa na kusema tungeshinda hii mechi wakati hatujashinda ni kujifariji faraja ambayo haina impact yoyote katika uharisia.
Gosh, Sijawahi kuona timu mbovu kutokea katika viunga vya mitaa ya Sir Matt Busby Way, Old Trafford kwa muda mrefu kama hii Man United ya mwaka huu lakini cha kushangaza ndiyo imeondoka kwenye viunga vyetu vya Emirates Stadium na point moja kibindoni kitu ambacho kwa Man United hii ni ushindi.
Ukiangalia na kuchunguza utagundua kuwa tulikuwa tunacheza mpira with fear of the unknown kama vile tunapambana na Man United ya Sir Alex Ferguson wakati wachezaji wa Man United pia walikuwa na wasiwasi mkubwa wa kufungwa as a result, Man United were excellent defending deep and in numbers,
Let's forget and move on kwa sababu kuna makombora Jumapili yako mbioni tena kushuka Emirates kutoka Merseyside saa 16:00 GMT kwa ajiri ya mtifuano wa FA CUP fifth round. Hata hivyo, nina uhakika hiyo mechi tutashinda.
Tukutane tena kwenye kijiwe chetu hiki Jumapili.
Once a Gunner, Always a Gunner.
Chu, ande goshi ulenamakoye.
Nhamala, Ule mhola kwenuko!.
Hujakumbana na Msukuma aliyeendelea ambaye anafunga redio kwente baiskeli kama car redio kwenye car dashboard!
Mimi pia nimeendelea kwa kiwango cha kuingia kwenye mechi za mpira na kushuhudia kabumbu badala ya kushuhudia mashindano ya ngoma ja bhagalu na bhagika wakati wa kiangazi.
Unenhe nale ngika.
Sitaki hata kulisikia hilo Lichelsea.Sasa Umekosea! Ungeshabikia li Chelsea la Mourinho kuliko Hiyo timu ina ukame Wa makombe!
Sitaki hata kulisikia hilo Lichelsea.
Wewe endelea tu kulishabikia huku nalo likiendelea kununua vikombe mbali mbali.
Yaani haiingii akilini Manchester hii ambayo timu kama Stoke city na Fulham wameigeuza kichwa cha mwendawazimu kwa kujifunzia kunyoa eti inakutana na timu mzuri kama Arsenal tena tupo nyumbani alafu tunadroo!!? Kweli hii ni haki?
Kwa upuuzi huu ubingwa tutaendelea kuusikia na kuusubiria hadi masiyah aka Jesus atakaporudi Duniani(kama ni kweli)
Hilo halina tatizo hata kidogo. Nikiyavaa sikai karibu na mti wakati nikiwa machungani!.Sasa Wewe unashabikia li timu lenye jezi nyekundu badala ya ya buluu km zile nguo zetu za machungani!
Utapigwa radi ukivaa nguo nyekundu machungani!
Chelsea ndio bingwa!
Hilo halina tatizo hata kidogo. Nikiyavaa sikai karibu na mti wakati nikiwa machungani!.
Litimu gani hilo lina kiwanja kwenye sehemu ya matajiri matajiri utadhani washabiki wake wote ni matajiri wakati wengine ni wakulima wa pamba na mahindi Kama kina Ntuzu
acha povu wewe,hujui kuwa hawa walibeba ndoo za kutosha?acha kujitoa fahamu
mnasubiria dua ya mchinjaji ambae hamna mtu wa kuchinja
Sasa Umekosea! Ungeshabikia li Chelsea la Mourinho kuliko Hiyo timu ina ukame Wa makombe!
Tulia wewe mnyantuzyu kule uliko wewe ni Genge tu la watu wenye interest ya aina 1 walijikusanya eti na wao wakajiita timu.
Shida ni kwamba kisu alikabidhiwa Giroud, na inaelekea yeye anaogopa kuona damu!!
Acha hizo weye
Mbona hamkutufunga Gunners?
Kutukosa mara tatu au saba hakuwezi kuondoa ukweli wa mchezo kwa jinsi ulivyokuwa umepangwa na mameneja wa timu mbili.Mkuu una ushabiki wa ajabu!!!! Van persie aliwakosa mara tatu. Pamoja na kugongesha mwamba mara mbili, Bado tu huamini na nyie mliponea kwenye tundu la sindano?