Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Wakuu niaje?, naona Arsenal sasa imekamilika kila idara na kwa kweli tushindwe sisi tu.

Wachezaji wengi isipokuwa Theo Walcott ni salama tayari kumalizia mechi 16 za ligi kuu ya Uingereza pamoja na CHampions league na FA Cup.

Aaron Ramsey, Lucas Podolski, Nicklas Bendtner, Alex Oxlade Chamberlain wote sasa wapo fit.

Ni Yaya Sanogo na Abou Vasiriki Diabi ndio wanaobakia kuuguza majeraha.

Kuhusu usajili kama ilivokuwa ikitarajiwa kuwa Arsenal wangesajili wachezaji kadhaa, hali haijawa hivo na wachezai hao imekuwa ni vigumu kuwapata kwa msimu huu wa baridi.

Lakini jioni hii chanzo kimoja cha habari na ambae ndie aletoa dondoo kuhusu deal la Mesut Ozil, ametoa dondoo usiku huu kwamba deal la Julian Draxler limekubaliwa na Schalke na huenda mchezaji huyo akaingia London wiki ijayo kukamilisha taratibu za usajili.

Julian-Draxler-3023635.jpg

Julian Draxler

Schalke walikuwa wanataka pesa yote ya milioni 37 zilipwe na inaonekana kumekuwa na "breakthrough".

Meneja Arsene Wenger anataka kumbadilisha Draxler awe mshambuliaji kama alivofanya kwa Robin Van Persie ambae Arsenal ilimsajili kutoka Feyenoord.

Van Persie alisajiliwa na Arsenal mwaka 2004 kuchukua nafasi ya Dennis Bergkamp na alikuwa akicheza kwenye nafasi ya kiungo pale Feyenoord.

Baadae Van Persie alikuja kuwa mmoja wa washambuliaji hatari kabisa kwenye ligi kuu ya Uingereza na barani Ulaya kwa ujumla.

Kama Draxler atakuja Arsenal basi atakuwa ni mmoja wa washambuliaji makini baada ya kufuata maagizo ya kitaalam ya meneja Arsene Wenger.
 
Thanks Gunners.

Tumetoa dozi kama ilivyotarajiwa. Bahati pia ilikuwa upande wetu kutokana na wao kukosa nafasi za wazi.

Huyu Nicklas Bendtner hovyo kabisa. Tunahitaji mshambuliaji mwingine kama kweli tunataka kufika salama kwenye position tuliyonayo kwa sasa katika ligi hasa ikichukuliwa kuwa ni point 9 tu zinazotuachanisha na timu ya sita kwenye premiership table.

Hiki kitabu cha Coventry tumekifunga, tunasubiri hiyo Tuesday, 28 January kutoa tena vidonge pale St. Mary's Stadium. Huyu mgonjwa Southampton ninafahamu atakuwa mbishi kunywa dawa yetu hasa ikichukuliwa kuwa atakuwa nyumbani kwake.

In Arsene We Trust and Once a Gunner, Always a Gunner.
 
Dogo Gedion Zelalem Jumapili anatimiza miaka 17 na atasaini rasmi mkataba na Arsenal wa miaka 2 na nusu.

Zelalem alizaliwa wakati maneja Arsene Wenger akiwa na mwaka tangu aanze kuifunza Arsenal na ilikuwa ni katika msimu wa 1996/97.
article_img.jpg

Kila la kheri Gedion Zelalem.

Zelalem anachezea timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 21 ya Ujerumani na wakti huohuo anaruhusiwa kuchezea timu ya taifa ya Ethiopia ambako ndiko wazazi wake wanatoka na pia timu ya taifa ya marekani USA ambako aliwahi kuishi.

Arsenal walimchukua mchezaji huyo kutoka timu ya Hertha Berlin ya Ujerumani.
 
Tuna siku kama 3 au 4 za kujiandaa na game ijayo nadhani bado usukani 2taendlea nao. Big up kwa wanaochungulia bila ya wao hamna chalengs
 
humu ndani nimepamiss sana asee...hope kila member ni mzima hapa
after all gunners wanazidi kutupa raha daily

Mkuu, tupo ila shuguli zimekuwa nyingi tunasubiri kuazia kesho Arsenal watatangaza mikataba mipya ya Per Mertesacker, Thomas Rosicky, Bacary Sagna na Gedion Zelalem ambae anasaini mkataba wa miaka miwili na nusu.

Halafu Arsenal pia watatangaza meneja Arsene Wenger kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu ya nyongeza ambao utamuingizia kiasi cha paundi milioni 24, yaani milioni 8 kwa mwaka.

Baada ya hapo tunaamini kuwa kuelekea mwishoni kabisa mwa muda wa usajili kwisha Arsenal watatangaza usajili wa wachezaji wawili ambao kama ni kweli inasemwa kwamba ni kiungo Julian Draxler wa Schalke ya Germany na mshambuliaji Mirko Vucinic wa Juventus ya Italy.

Premiership-Transfers-3050516.jpg

Mirko Vucinic

Vucinic alikuwa asajiliwe kwa timu za Juventus na Inter Milan kubadilishana kati yake na kiungo Fred Guarin lakini deal hilo limekufa.

Hivyo Vucinic mwenye umri wa miaka 30 akiwa na wazo la kombe la dunia mwzi June mwaka huu anataka acheze mechi nyingi ili awe na nafasi kwenye timu ya Italy.

Nicklas Bendtner kwenye mechi na Coventry hakuonekana kama anaweza kuwa reliable na ufungaji wake na huenda hali hiyo imewafanya Arsenal waangalie mshambuliaji mwingine ambae ni "ready made".

LIVE--Julian-Draxler-3059591.jpg

Julian Draxler

Inasemwa kwamba deal lake limekamilika na nae ataingia Emirates wiki ijayo.

COYG!
 
Duh, draw ya FA CUP Fifth round imetutupa na wazee wa Merseyside!. Hata hivyo tuna advantage ya kuwa tutakuwa kwenye uwanja wetu wa kutoa dose. Arsenal v Liverpool

Ninatumaini tutaendelea kwenye Sixth round.

Draw nyingine nzuri iliyofanyika niya Wazee wa kununua vikombe England kwa pesa ya oil wamewekwa pamoja ili wapambane. Manchester City v Chelsea.

It's really exciting for me!

To be the best we have to play against the best.
 
Tarehe 2 February tunawakaribisha Crystal Palace.

Tarehe 8 February Arsenal tunaenda Anfield kucheza na Liverpool na siku chache tena tunawakaribisha Man Utd tarehe 12 February.

Jumamosi ya tarehe 15 tunawakaribisha Liverpool Emirates kwenye FA Cup, kabla ya kumalizia na Bayern Munich Jumatano tarehe 19 February.

Tutaumaliza mwezi wa February kwa kuwakaribisha Sunderland Emirates.

February ni mwezi muhimu sana kwa Arsenal.

COYG!!
 
ebana ratiba yetu ya February nuksi. Tuna mechi kibao muhimu zimeshonana kati ya siku chache za kupumzika. Natumaini tutaondoka na points zote COYG!!!
 
Babu wenu anaangalia kama kuna wengine wanauzwa
 

Attachments

  • 1390770908900.jpg
    1390770908900.jpg
    12.5 KB · Views: 104
Back
Top Bottom