TRANSFER UPDATES
Wakuu goodmorning,
Habari za usajili wa mshambualiaji kwa timu yetu ya Arsenal zimepamba moto lakini maskauti wapo busy sana na Ivan Gazidis na mwenzie Dick Law ambao ndio wataalam wa kuzungumza biashara za usajili baada ya kuagizwa na mzee Wenger, bado wanazungumza na Real Madrid kuhusu Morata.
Kuna kila sababu kwamba deal la paundi milioni 2 linaweza kufanywa ili Morata aende Arsenal kwa miezi 6 ili apate uzoefu zaidi kutokana na Morata mwenyewe kupendelea option hiyo badala ya kuhama kabisa.
Alvaro Morata
Wapo nchini Spain na pia maskauti wameulizia kuhusu mshambuliaji mwingine Jackson Martines ambae ni mColombia kuhusu availability yake pale Porto nchini Ureno kama option endapo deal la Morata litashindwa.
Kuna kila dalili kwamba deal la Morata lina usumbufu ukizingatia pia habari kwamba baadhi ya timu za PL zimeingia kwenye mchakato wa kumsajili mchezaji huyo na moja ya timui hizo ni Liverpool.
Lakini "penye udhia penyeza rupia"
COYG!