MwafrikaHalisi
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 1,741
- 511
Kifo cha MENDE, chali pwaa. ChachaWANGWE uko wapi mukulu. hopefully VICHAKANI hahahahaha. Poleni chana.Dah kazi kweli kweli ..... Arsenal Out
Unajua kinachowapa jeuri jamaa ni the fact kwamba Arsenal ni timu inayopendwa na neutrals wengi, kuna watu wengi ambao sio mashabiki wa Arsenal lakini wanapenda kuwaangalia wakicheza, pia location yao ya london inawasaidia sana coz watalii wengi wanapenda kwenda kuwaona so hawa jamaa hawategemei sana mashabiki damu kama sisi. One of the most expensive club (kama sio the most expensive) to watch. Kinachoudhi ni kuwa uongozi unajali zaidi balance sheet na kusahau kuwa hiyo kitu haina maana yoyote kwa mashabiki, wao wakimaliza kwenye top 4 tu, hilo ni bonge la achievement coz wanajua mamilioni ya champions league yataingia, mimi nasali sana tumalize nje ya hiyo top 4 ili wakose hela na wao wapate uchungu, na hiyo hasara itawalazimisha wanunue wachezaji wa maana.
Strategy ya AW ya kununua watoto ingefanya kazi kama tungekua hatuuzi, watoto wanakuja wakikaa few seasons na kuwa finished articles wanapigwa bei! Ni kama vile unajenga nyumba halafu ukifika juu badala ya kupaua unapiga kozi kadhaa chini halafu unaanza tena kujenga, huo ujenzi hauishi! Naamini kama tungekua hatuuzi wachezaji wetu, hakuna timu ingekua inatia mguu kabisa! Achilia waliouzwa zamani, rudisha tu Clichy, Fabregas, Nasri, RVP na Song kichwani mwako uone hii timu ya sasa inavobadilika..And did I say Theo and Sagna wanaondoka next month??
chini ya top 4 sio rahisi kukwepa msimu huu tunashuka kwenye 7
Mkuu KKN,
Hao wote ni walewale Arsenal haters ni wengi mno na wanafurahia sana hali iliyopo sasa.
Wenger ataendelea kuwa meneja wa timu ya Arsenal na ana mkataba amabo unamalizika 2014.
Amekiri kwamba Arsenal imepoteza mhimili pale kwenye midfield na hasa pale alipomuuza Fabregas na Nasri.
Jioni hii AST tumeambiwa kwamba kuna funds iliyopo kuhakikisha kunasajiliwa wachezaji muhimu ifikapo January.
Haya matokeo ya Bradford waliocheza kama wapo kwenye fainali hayapotezi usingizi.
Richard nimefurahi kukuona tena hapa mkubwa, long time sana- am back!
Tatizo la Arsenal ni kwamba kila siku wanasema kuna fungu la kusajili wachezaji lakini hatuoni wakisajili, ukitaka midfielder au striker wa maana kwenye soko la sasa basi uwe tayari kulipa above £20m kitu ambacho AW haoni kuwa ni sahihi. Inabidi babu akubaliane na hali halisi ya soko tu. Na pia kuna haja ya kubadili salary structure, wachezaji wengi wanaondoka kwa kuwa wanapata offer nzuri kwenye vilabu vingine. Miaka 7 bila kombe lolote ni aibu kubwa kwa club kama arsenal na mashabiki wana kila sababu ya kuwa na hasira na AW.
Mkuu mie nimeshapoteza imani siku nyingi sana na AW na management yote ya Gunners. Walinimaliza nguvu kabisa pale walipoamua kumuuza Van Puuuu.... kwenda MANU. Makosa kama hayo ya kumuuza mchezaji wenu star kwa timu ambayo iko EPL hata siku moha SAF huwezi kumsikia akiyafanya. Nakumbuka miaka michache iliyopita Rooney alitingisha kibiriti na kutaka kuondoka MANU. SAF hamkutolea uvivu na kamwambia una uhuru wa kuondoka tutakuuza katika timu yoyote ambayo itatupa pesa nzuri lakini ujue timu hiyo haitakuwa UK bali ni nje ya UK kwa maana nyingine kuhamia katika ligi ya Germany, Spain, Italy etc Rooney mwenye akanyoosha mikono juu na kutia wino ili kubaki MANU.
Timu inashuka hadhi taratibu na ilhali Bank account ya Gunners imenona vibaya sana. Wanataka wachezaji wa bei poa matokeo yake one of the mighty team among the best teans in EPL, Europe and the World sasa hivi imekuwa kibonde cha hali ja juu. Siku hizi nikiangalia mechi najua uwezekano wa kwanza ni kufungwa, kutoa draw au tukibahatika kushinda kimanati manati.
Wachezaji pamoja na kulipwa mabilioni lakini nao wanataka kubeba makombe mbali mbali ya EPL, FA, UEFA etc lakini timu yetu ya Arsenal kila mwaka nafasi ya kufanya hivyo ndio inazidi kututupa mkono. wachezaji wa zamani wa Gunners wamejaribu sana kuongea kwenye vyombo vya habari mbali mbali kuhusu umuhimu wa kuwa na wacheza ambao wana experience ya kutosha lakini management ya Gunners imetia pamba masikioni huku timu ikizidi kudorora msimu hadi msimu.
Sasa hivi hata kuwapata wachezaji wakali duniani itakuwa ni kazi mno!!! maana inaonekana Gunners haiwajali hata masuperstar wake mbali mbali na hivyo kuhakikisha inafanya juu chini ili kutowapoteza na hivyo kujenga timu imara ya kuweza kupambana na MANU, MANC, BARCA, RM etc..Siku hizi hata tukicheza na vibonde wanajua hawa Gunners ni vibonde wenzetu tukikaza msuli basi tunaweza kuondoka na 3 points!!! :target::target:
Nitafurahi kuona mechi za nyumbani za Gunners uwanja unakuwa mtupu hivyo kuwapa mstuko mkubwa owners na management in order to kick them where it hurts the most, Gunners' bank account...labda ndio watatia akili kichwani na kuirescue timu kabla haijashuka daraja. Na kwa matokeo ya hivi karibuni sitashangaa kusikia Walcott naye ameamua kuvua jezi na kwenda MANC, MANU au Tottenham... nasubiri kwa hamu mchapo mkali wa J'pili kati ya MANU na MANC
Msema kweli....