ArchBishop Rugambwa ni Raia wa Wapi?

ArchBishop Rugambwa ni Raia wa Wapi?

Bazazi

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2008
Posts
2,806
Reaction score
3,524
Najua watu wengi watanishangaa kwa kuuliza swali hili:

ASKOFU MKUU NOVATUS RUGAMBWA NI RAIA WA NCHI GANI?

Ninajua kabisa kuwa kwa kuzaliwa ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa lakini ninaamini kabisa kuwa ni raia wa Vatican kiroho. ArchBishop Rugambwa ameteuliwa kuwa mwakilishi wa papa (balozi wa Vatican) ktk nchi za Angola na Sao Tome and Principe.

Hoja na wasiwasi wangu ni kuwa yeye atakuwa mwaminifu kwa nchi gani kati ya nchi hizo mbili? Je ni Tanzania kwa kuwa tu ni nchi yake ya kuzaliwa au Vatican nchi yake ya kiroho? Naomba tuijadili hoja hii bila jaziba wala kashfa ili tuweze kupanuana mawazo na ufahamu kuhusu masuala mazima ya kiimani.

Naomba Kuwakilisha

BAZAZI
 
Wewe unataka awe mwaminifu kwa nani? SIoni mantiki ya swali lako maana majibu unayo; kama bosi wako anakutuma kufanya kazi fulani nje ya nchi yako utakwenda kumwakilisha nani kama si aliyekutuma?
Labda nawe tukuulize swali; unajua anaenda huko kwa maswala gani? Kisiasa au? Ndo maana ni Archbishop (Kiongozi wa Kiroho) na hayo ndo majukumu yake.
 
Lol yaani hapa napo umeshindwa kufafanua mpaka ijadiliwe? Hebu fikiria leo uchaguliwe kuwa mwakilishia wa UNICEF Nigeria je utaenda kuiwakilisha Tanzania au UNICEF hebu fikiri kwanza bana mbona vitu vingine ni rahisi sana ati?
 
Back
Top Bottom