KERO Apps za mikopo mitandaoni, serikali ipo wapi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Naamini hakuna anaelazimishwa kukopa huko! Yeye alipe tuu, mambo yasiwe mengi. 😊
 
Wananchi mmeambiwa na serikali msikope kwenye hizo Apps halafu mnaendelea, kama sio dharau ni nini? Nyie wakopaji mnapata wapi ubabe wa kupuuza maelekezo ya serikali? Ndugu ishi kulingana na kipato chako ili uepuke mikopo. Au fanya hata vibarua vya hapa na pale uongeze kipato badala ya kukopa.
 
Hizo hela piga,tulia,acha wapige mayowe,mi nishazipiga sana
 
Naomba mkopo🤣
 
Tembelea website ya bot.go.tz kuna orodha ya application zilizoruhusiwa. Kama hiyo haipo kaa kimya hawatakufanya kitu
 
Wengi wanatumia neno kukopa bila ya kuwa na nia ya kulipa tangu mwanzo.

Wengine hawaangalii riba za mikopo hii ambazo ni kubwa sana. Ni zaidi ya 100% kwa wiki. Unachopewa ni pungufu sana kutoka kinachoandikwa umekopa.
 
Wengi wanatumia neno kukopa bila ya kuwa na nia ya kulipa tangu mwanzo.

Wengine hawaangalii riba za mikopo hii ambazo ni kubwa sana. Ni zaidi ya 100% kwa wiki. Unachopewa ni pungufu sana kutoka kinachoandikwa umekopa.

Anakopa tuu, anafikiri atawakimbia hawa jamaa. Kitendo cha kuingiza taarifa kwenye apps zao, faili lako lote wanalo, mpaka ndugu zako, wapenzi wako n.k. Hizo apps za kichina hizo.
Mtu smart hawezi hata kupakua apps za hao jamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…