Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,263
- 44,393
kumbe unalinganisha simu? hukusema toka mwanzo?Mkuuu naona umekwepa swali langu , sasa tumalize huu utata, Tangu huu uzi upande mmoja imesimama Iphone X na upande mwingine zipo simu mbali mbali yaan X ishalinganishwa na simu kibao, hii inaonesha kiasi gani hii simu iko next level. Sasa naomba unitajie simu moja tu inayoweza ku compete na iphone X kwa kila kitu kama performance, display, camera, Battery na Build. Naomba hiyo simu iwe nje ya kampuni ya apple. Nafikiri utata utaishia hapa.
binafsi mimi simu bora kabisa duniani kwa sasa ni samsung galaxy s6 active. . tuanze na zako then nitamalizia zangu
nayalist
-battery
-perfomance
-display
-camera
-build
1. simu yenye quad HD inayokaa na chaji zaidi. (gsmarena)
compare na iphone x
hivyo mkuu ukiangalia kwenye ukaaji chaji haina mjadala kila idara active ipo juu kuanzia standby, call time, browsing hadi video playback.
2. build quality
bila kupepesa macho active ipo juu sababu ni rugged phone utapata vitu kama
-water proof
-shock proof
-best build quality na imara inayovumilia mianguko, simu kama hii hata cover haihitaji
3. display
zote ni quad HD na on paper ya iphone x ni nzuri ila haiwezi fanya haya hivyo anyday anytime nitachagua ya active.
-hakuna themes wala black mode kwenye ios, ukiwa na kioo cha oled rangi nyeusi ni nzuri sana, najua kuna invert mode, ila invert sio black mode. utasave charge na themes nyeusi kwenye amoled ya active. (serious 2017 ios haina blackmode? karibu zama za mawe)
-Hakuna VR- tunajua display inakula sana charge na lengo kubwa la kuwa na display yenye resolution kubwa ni kuangalia video za 3d au video za 360, ila ios na iphones kwa ujumla hazikubali haya mambo hivyo resolution kubwa ni useless kwao, nikiwa na s6 active yangu navuta tu headset ya VR au natengeneza mwenyewe (rahisi tu) kisha naangalia zangu 3d kiulaini.
4.perfomance
again on paper iphone x ni monster ina cpu kali, almost inai double nguvu s6 active, ila in reality ni joka la kibisa haling'ati, unaweza nipa matumizi makubwa ya ios yanayohitaji powerfull cpu? kwenye android s6 active unafanya haya
-ndio simu ya kwanza ku emulate dolphin na kucheza games za nintendo wii na gamecube, games kali sana huwezi fananisha quality yake na games za simu
-utafanya pia emulation nyengine kama vile kurun visoftware vidogo vidogo vya windows na linux distro.
-unaweza ukawa na user hata watatu kazini, personal, guest kwenye simu yako na zote ukazi process kwa pamoja
kuna mambo mengi sana unaeza ukatumia processor yako kwenye android ila kwenye ios huwezi.
5. camera
iphone x ina camera nzuri zaidi kuliko s6 active
hayo ni mambo yako na mimi naongezea yangu
6. bei
s6 active unaiokota ebay chini ya $200 sometime mpaka $120 kwa hela za kitanzania ni around 400,000 wakati iphone x ni dola 1000 kupanda aka 2,300,000 kupanda.
7. connectivity
nikiwa na s6 edge yangu nitachomeka waya wa HDMI na adapter ya usb, nikiamua nitatumia wifi kama miracast au widi nitaangalia kwenye tv kupitia simu etc, iphone x ina airplay tu hio hio ndio utumie kama huna utajijua mwenyewe na airplay ni weaker kuliko miracast. pia naweza chomeka vitu kama hard disk, mouse, game controller za usb, keyboard na vyenginevyo kwenye usb port.
8. 3.5mm jack
iphone x haina sehemu ya kuchomekea earphone zaidi ya ile port ya kuchajia, ukitaka kusikiliza kitu huku unachaji mpaka ununue adapter. huku kwenye active hakuna hayo.
etc etc etc yapo mengi sana.
so bwana island ungetoa milioni 2.3 kununua simu dhaifu au utoe 400,000 kununua simu bora zaidi?