Apigwa na askari hospitalini akisubiri kununua dawa za mama yake mzazi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga

Champion_Boy

Member
Jul 13, 2018
24
77
Kipande kifupi cha video tulichotumiwa na Lydia Lefi, Mkazi wa Shinyanga cha tukio la Walinzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga kumchapa mikanda kijana ambaye amedai ni mdogo wake kwa kosa la kupitiliza muda wa kuona wagojwa katika hospitali hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Lydia anasema, kaka yake huyo Daudi Lefi (anayepigwa) alipewa Control namba ili akanunue dawa kwa ajili ya mama yao ambaye amelazwa katika hospitali hiyo, lakini jina halikuonekana na aliporudi kuhoji kwa daktari ndipo mlinzi akamtoa nje akidai muda umekwisha wa kuona wagonjwa, ndipo mlinzi huyo akaanza kumsukuma kumtoa nje na baada ya mabishano akavua mkanda na kuanza kumchapa.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospital hiyo,Luzila Boshe amekiri kutokea kwa tukio hilo na kubainisha atatoa taarifa kamili baadae.




Your browser is not able to display this video.
 
Dawa inanunuliwa kwa control number?
Kifupi tu wabongo sio watu wa kujali, hapo unaweza kuta jamaa alikuwa anaforce kuingia hata Kama hakuruhusiwa
 
Wakuu mambo yanazidi kunoga nchini Tanzania, baada ya vipigo kwa raia kurasimishwa rasmi.

Video hii inawaonyesha wanaodaiwa kuwa walinzi wa hospitali ya Mkoa wa Shinyanga wakimtandika bila huruma mtu aliyedaiwa kuzidisha muda wa kuona wagonjwa.

Your browser is not able to display this video.

Mhanga huyo alipohojiwa alikiri kuzidisha muda uliopangwa ili kuona wagonjwa lakini anadai kwamba kilichomchelewesha ni kusubiri taarifa ya gharama za matibabu ya ndugu yake ili mipango ya malipo ifanywe.
 
Mmewasikiliza walinzi mkapata balanced story au ndio walewale WEZI wa vifaa tiba kama ilivyowahi tokea hapo awali kwenye hispitali hiyo hiyo ikiwahusisha watumishi na walinzi pia.
 
Walinzi acha wapige wazembe maana na wenyewe wanahitaji mapumziko.
 
Hizi video zinaendelea kuzagaa kwenye mitandao namna Watz wanapitia vichapo, hii nyingine. Walinzi na wao hawajabaki nyuma

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…