Champion_Boy
Member
- Jul 13, 2018
- 24
- 77
Kipande kifupi cha video tulichotumiwa na Lydia Lefi, Mkazi wa Shinyanga cha tukio la Walinzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga kumchapa mikanda kijana ambaye amedai ni mdogo wake kwa kosa la kupitiliza muda wa kuona wagojwa katika hospitali hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya Lydia anasema, kaka yake huyo Daudi Lefi (anayepigwa) alipewa Control namba ili akanunue dawa kwa ajili ya mama yao ambaye amelazwa katika hospitali hiyo, lakini jina halikuonekana na aliporudi kuhoji kwa daktari ndipo mlinzi akamtoa nje akidai muda umekwisha wa kuona wagonjwa, ndipo mlinzi huyo akaanza kumsukuma kumtoa nje na baada ya mabishano akavua mkanda na kuanza kumchapa.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospital hiyo,Luzila Boshe amekiri kutokea kwa tukio hilo na kubainisha atatoa taarifa kamili baadae.

Ofisi ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga ikiongozwa na Kaimu mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Luzila Boshe imelaani kitendo kilichotokea Tarehe 21 january 2021. Na kuahidi kutoa Tamko la tukio hilo kwa siku chache zijazo.
Nilibahatika kuongea na Dada wa mhanga wa tukio hilo Lydia Lefi aishiye kata ya Ndembezi Mjini shinyanga.
Alisema kwamba kaka yake Daudi lefi (Mkazi wa Mjini Shinyanga) ameshambuliwa na walinzi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga (SUMA JKT) wanaodaiwa kumtaka aondoke wodini kwamba muda wa kusalimia wagonjwa umeisha ili hali akisubiri kupatiwa gharama za dawa kwa ajili ya mgonjwa wake.
Aliendelea kusimulia kwamba wao Walifika Hospitalini hapo baada ya mama yao mzazi Kuugua na kupatiwa huduma ya kulazwa katika hospitali hiyo,Katika jitihada za kuokoa maisha ya Mama yao Daktari aliwaandikia dawa na kupatiwa control namba ili kulipia kwa ajili ya kupatiwa dawa hizo,kutokana na Mtandao kuwa mbovu control number waliyopewa ilishindwa kufanya kazi,Hivyo iliwalazimu kurudi kwa Daktari kuandikiwa control number mpya.
Baada ya kurudi kule lydia Lefi amesema kuwa walinzi hao walidhani kaka yake amefika muda huo huo hospitalini wakati yeye alikuwa amefika hospitalini hapo muda mrefu lakini Computer za Hospitali zikawa hazisomi jina la mgonjwa wake wakati anataka kununua dawa.
Baada ya kumuona Askari hao walimtoa kwa nguvu licha kujieleza vizuri kuwa alitaka kupatiwa control number ya Mgonjwa wake.Baada ya kukataa kutoka Askari hao walianza kumshambulia kwa ngumi na Mikanda Kaka huyo.
Baadhi ya wagonjwa na watu wanaouguza wagonjwa wameeleza kusikitishwa na kitendo cha walinzi hao kumpiga ngumi na mkanda na kuongeza kuwa baadhi ya walinzi katika hospitali hiyo wana lugha mbaya na wanatumia ubabe hawaangalii utu.
Gusa link Kuangalia Video ya Baadhi ya matukio..