Apigwa na askari hospitalini akisubiri kununua dawa za mama yake mzazi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga

Weka na ile ya Wachina wakiwashikisha adabu ndugu zako huko Kunya.

Hii hapa
Watanzania wacharangwa mapanga ndani ya Tanzania na Wachina

Wachina watano mbaroni kwa kujeruhi Watanzania kwa sime

Wachina watosa watanzania baharini

Hii nyingine

2371932_Clipboard03.jpg
 
Wakuu mambo yanazidi kunoga nchini Tanzania , baada ya vipigo kwa raia kurasimishwa rasmi

Video hii inawaonyeaha wanaodaiwa kuwa walinzi wa hospitali ya Mkoa wa Shinyanga wakimtandika bila huruma mtu aliyedaiwa kuzidisha muda wa kuona wagonjwa .

View attachment 1683835


Mhanga huyo alipohojiwa alikiri kuzidisha muda uliopangwa ili kuona wagonjwa lakini anadai kwamba kilichomchelewesha ni kusubiri taarifa ya gharama za matibabu ya ndugu yake ili mipango ya malipo ifanywe .


Mgambo wengine huvuta bangi kabla ya kuingia kazini, hiyo ni "motivation" ya bangi tu.

Bangi mbaya sana.
 
Hehehe, tazama hiyo video niliyoweka hapo ndio uone unavyotia aibu kwa kuleta maambo ya watoto.
Wewe vipi? -- hivi kweli unajitambua? Hebu sasa angalia vituko na ukatili na UUAJI wa polisi wenu kwa raia wenu na ulinganishe na hilo tukio moja dogo lililotokea huko Shinyanga.

Screenshot_20210123-043051.png
 
Wewe vipi?--- hivi kweli unajitambua? Hebu sasa angalia vituko na ukatili na UUAJI wa polisi wenu kwa raia wenu na ulinganishe na hilo tukio moja dogo lililotokea huko Shinyanga.

View attachment 1683878

Masuala ya polisi yapo duniani hata juzi Marekani kumetokea maandamano taifa lote kupinga ukatili wa mapolisi, humu hata nikiamua kukusanya nyuzi au taarifa za uchafu wa polisi wenu nitajaza server za watu bure, ila tunazungumza kuhusu haya matukio ambayo yameanza kuibuka.

Bongo mnavyochapwa viboko na viongozi wenu, imekua jambo la kawaida sana mijitu kulazwa chini na kutembezwa viboko, mumejiachia legelege naona hata walinzi wa kawaida nao wameamua nao wasiachwe nyuma.
 
Katika hali isiyotarajiwa mwanaume aliyejulikana kwa jina la Daudi Lefi (40) amejikuta katika wakati mgumu baada ya kushambuliwa na Walinzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wanaodaiwa kumtaka aondoke wodini kwamba muda wa kusalimia wagonjwa umeisha.

Tukio hilo lililozua gumzo la limetokea leo Ijumaa Januari 22,2020 majira ya saa 11 na dakika 45 jioni wakati kijana hiyo akiwa aktika wodi ya wanawake namba 1 ambako mama yake mzazi Victoria Lugano Mwakagari amelazwa hospitalini hapo jana.

Akisimulia kuhusu tukio hilo, ndugu wa kijana huyo Lydia Lefi ameiambia Malunde 1 blog kuwa kaka yake amekutwa na mkasa huo wakati akiwa katika harakati za kulipia dawa za mama yao ambaye amelazwa katika hospitali hiyo jana Januari 21,2021 lakini jina lilikuwa halionekani kwenye Computer.

“Kaka alikuwa alipie dawa, alipewa karatasi ya kwenda kulipia dawa, alipoenda kufuata Control number ili alipie, jina likawa halionekani kwenye Computer, ikabidi aende wodini kwa mgonjwa kuangalia/kuulizia amesajiliwa kwa jina gani,akiwa wodini hao walinzi ndipo walipoingia wodini na kumtaka aondoke kwamba muda umekwisha.

"Walivyomtaka aondoke wodini akawaambia amekuja kuangalia jina gani mgonjwa ameandikishwa, wale walinzi wakamwambia aondoke muda huo huo, akawaomba lakini wakamwambia Huwezi kutupangia kazi. Kaka akasema nitaondokaje mama hajapata huduma ,wale walinzi wakaanza kumsukuma, ndipo mlinzi mmoja akachomoa mkanda wa suruali na kuanza kumshambulia huku mwingine akimsukuma, wakati purukushani zikiendelea baadae akaja mlinzi wa kike akasogea na kuwaachanisha”,ameeleza Lydia.

Daudi Lefi amesema walinzi hao wanaodaiwa kuwa ni wa Suma JKT walidhani amefika muda huo huo hospitalini wakati yeye alikuwa amefika hospitalini hapo muda mrefu lakini Computer za Hospitali zikawa hazisomi jina la mgonjwa wake wakati anataka kununua dawa.

"Sikurusha ngumi kwa sababu ni eneo la hospitali wangesema nimeenda kufanya vurugu. Walionishambulia walikuwa wawili lakini mmoja ndiyo aliyeanza kwa kunichapa na mkanda akisema nitamtambua kuwa yeye ni nani huku akinitukana,nami nikamsihi aache kutumia lugha chafu eneo la kazi",amesema Daudi.

"Hayo yote yametokea wakati nikimweleza kuwa nimefika wodini kuulizia ndugu zangu na mgonjwa kuwa wameandikisha jina gani mapokezi kwani jina halionekani mapokezi ili nilipie dawa,wakati naendelea kushambuliwa nikamuona mama yangu mgonjwa akitoka wodini huku akihema presha imepanda akifuatilia nini kinaendelea ndipo nikaanza tena kumrudisha wodini kumhudumia nikaulizia jina aliloandikisha nikaenda kuchukua dawa nikamletea wodini", ameeleza Daudi.

Daudi amesema kutokana na kipigo hicho ameumia mkono wa kushoto ambao umevimba na kuchanika kwenye kiwiko.

"Baada ya tukio hilo wamenifuata na mkubwa wao na kuniomba tuyamalize kwamba kijana wao amekosea nami nimeamua kuwasamehe. Katika hali ya ubinadamu nimeamua kumsamehe kijana huyo baada ya kuomba radhi",ameongeza.

Baadhi ya wagonjwa na watu wanaouguza wagonjwa wameeleza kusikitishwa na kitendo cha mlinzi kumpiga ngumi na mkanda na kuongeza kuwa baadhi ya walinzi katika hospitali hiyo wana lugha mbaya na wanatumia ubabe hawaangalii utu.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, Luzila John Boshi amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa atatoa taarifa baadae na kwamba yupo kwenye kikao

Malunde blog
 
Masuala ya polisi yapo duniani hata juzi Marekani kumetokea maandamano taifa lote kupinga ukatili wa mapolisi, humu hata nikiamua kukusanya nyuzi au taarifa za uchafu wa polisi wenu nitajaza server za watu bure, ila tunazungumza kuhusu haya matukio ambayo yameanza kuibuka Bongo mnavyochapwa viboko na viongozi wenu, imekua jambo la kawaida sana mijitu kulazwa chini na kutembezwa viboko, mumejiachia legelege naona hata walinzi wa kawaida nao wameamua nao wasiachwe nyuma.

Sasa una support nini na unapinga nini? kama huko America mambo hayo yapo unashangaa nini
yakiwepo Tz?

Sasa huyo aliyepiga mtu ni nani??--- hujui kwamba polisi (au millitia man/local police) ni watu wanaotekeleza sheria, "law enforcers " na wakati fulani wanaruhusiwa kutumia nguvu katika kutekekeza majukumu yao??

Wewe chuki yako ya kikabila ya huko kwenu unaielekeza Tz (it is just the same tribal hatred into play but this time against Tz).
 
Sasa una support nini na unapinga nini??, kama huko America mambo hayo yapo unashangaa nini
yakiwepo Tz?!!

Sasa huyo aliyepiga mtu ni nani??--- hujui kwamba polisi (au millitia man/local police) ni watu wanaotekeleza sheria, "law enforcers " na wakati fulani wanaruhusiwa kutumia nguvu katika kutekekeza majukumu yao??

Wewe chuki yako ya kikabila ya huko kwenu unaielekeza Tz (it is just the same tribal hatred into play but this time against Tz).

Nawahurumia maana imekua mwendo wa kipigo kutoka kwa viongozi na sasa mpaka kwa walinzi....mumekua legelege sana..
 
Hawa walinzi wa summa jkt wana nini?Maana sio mara ya kwanza kufanya mambo ya kijinga namna hii.

Pale Dodoma stand mpya walikuwa wanawarukisha kichura abiria kwa sababu za kijinga kabisa. Naamini kuna shida mahali fulani wanatakiwa wajirekebishe.

Wajifunze kwa makampuni ya wazungu wako smart sana
 
Jkt inafanya watu wakose ubinadamu sasa hasira za kukosa kazi depo unaamishia kwa raia.

Anyway mwamba ana moyo mkubwa sanaa Mungu amlinde na amponye mama etu
 
Hawa walinzi wa summa jkt wana nini?Maana sio mara ya kwanza kufanya mambo ya kijinga namna hii.
Pale Dodoma stand mpya walikuwa wanawarukisha kichura abiria kwa sababu za kijinga kabisa.Naamini kuna shida mahali fulani wanatakiwa wajirekebishe.
Wajifunze kwa makampuni ya wazungu wako smart sana
Kila sehemu ni hivyo jamaa hawajui kujali wateja wapigwe semina kabla ya kuja kitaaa maana wanajiona kama wanajeshi kumbe makuruti tu.
 
Nawahurumia maana imekua mwendo wa kipigo kutoka kwa viongozi na sasa mpaka kwa walinzi....mumekua legelege sana..
Unashindwa kujihurumia nyie wenyewe uje utuhurumie sisi??!🤣

Nani legelege kati yetu na nyie?? Alshabab tu wanawatoa kamasi, askari wasiokuwa na mafunzo, majambazi wa kisomali.🤣🤣

Angalia woga wenu ulipofikia sasa mnaomba pooo kwa majambazi 🙉

Screenshot_20210123-060735.png
 
Unashindwa kujihurumia nyie wenyewe uje utuhurumie sisi??!🤣

Nani legelege kati yetu na nyie?? Alshabab tu wanawatoa kamasi, askari wasiokuwa na mafunzo, majambazi wa kisomali.🤣🤣

Angalia woga wenu ulipofikia sasa mnaomba pooo kwa majambazi 🙉

View attachment 1683888

Subiri nikipata fursa nitakuewekea hizo video za mnavyo charazwa viboko na viongozi wakiwemo hata viongozi wa kike, mnaitia Afrika aibu kwa kweli...hehehehe
 
Back
Top Bottom