Apigwa mapangwa baada ya kukataa kuteremsha bendera ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Apigwa mapangwa baada ya kukataa kuteremsha bendera ya CHADEMA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 12, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mfanyabiashara acharangwa mapanga katika vurugu za siasa

  NA MWANDISHI WETU
  11th October 2010  Vurugu zinazohusishwa na masuala ya kisiasa zimezuka katika mji mdogo wa Malampaka uliopo wilayani hapa Mkoa wa Shinyanga na kusababisha mfanyabiashara mmoja kujeruhiwa kwa kucharangwa kwa mapanga.

  Vurugu hizo zinadaiwa kuwahusisha wafuasi wa vyama vya siasa wanaodaiwa kumvamia na kumcharanga kwa mapanga mfanyabiashara huyo, Charles Njige maarufu kwa jina la Mwanangolo wakimtaka ateremshe bendera ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyokuwa inapeperushwa nje ya duka lake.

  Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 5:30 asubuhi na kusababisha shughuli za kijamii kusimama kwa muda wa saa tano katika mji huo.

  Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu mjini humo, Njige alisema kuwa akiwa dukani mwake, yalifika magari mawili yanayomilikiwa na mmoja wa wagombea ubunge wa Jimbo la Maswa Magharibi (jina tunalihofadhi) yakiwa na mabango ya picha yake na kuteremka watu watatu kila mmoja akiwa na panga.

  Alisema watu hao ambao anawatambua (majina tunayo) waliingia moja kwa moja dukani kwake na kumweleza kuwa wako katika operesheni ya kuteremsha bendera zote za Chadema zinazopeperushwa katika mji huo na kudai yalikuwa ni maagizo ya mgombea ubunge huyo.

  Aliongeza kusema kuwa baada ya kukataa kutekeleza agizo hilo, waliteremsha bendera hiyo na kuichanachana kisha kumcharanga kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake. Alisema kuwa alijitahidi kupambana nao huku akipiga yowe kuomba msaada. " Watu waliokuwa karibu na duka langu waliposikia kelele hizo, walifika na kuanza kupambana na watu hao kwa kutumia nondo, fimbo na mapanga na walizidiwa nguvu na hivyo kufanikiwa kutoroka wa kutumia magari hayo, " alisema.

  Aliongeza kuwa baadaye alikwenda Kituo cha Polisi cha Malampaka kutoa taarifa za uvamizi huo, lakini alielezwa na askari mmoja mwenye cheo cha Koplo kuwa hawawezi kwenda kudhibiti vurugu hizo kwani walikuwa wamebaki askari wawili kituoni hapo na wengine walikwenda kwenye majukumu mengine hivyo kukosa msaada wa kituo hicho.

  Mfanyabiashara huyo alisema majira ya saa 9:00 mchana gari la polisi lenye namba PT 638 lilifika likiwa na baadhi ya askari na kumkamata kiongozi wa vurugu hizo na kumuweka chini ya ulinzi katika kituo hicho.

  Hata hivyo, alisema kundi la watu wapatao 300 walivamia kituo hicho huku wakipiga kelele za kutaka mtuhumiwa huyo aachiwe ili waweze kumshughulikia.

  Alisema polisi waliwatawanya na kueleza kuwa hatua za kisheria zitachukua mkondo wake kwa watu wote waliohusika katika vurugu hizo na kuteremsha bendera za Chadema.

  Inadaiwa kuwa mmoja wa viongozi waandamizi wa chama kimoja alisema chama chake kitaendelea na operesheni ya kushusha bendera za Chadema.

  Polisi wilayani Maswa walithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kushikiliwa kwa mtuhumiwa aliyeongoza vurugu hizo kwa mahojiano zaidi.

  Tangu kuanza kwa kampeni za kuelekea Uchaguzi Mkuu, wafuasi wa chama kimoja wilayani Maswa wamekuwa wakituhumiwa kuwafanyia fujo wagombea na wafuasi wa Chadema.

  Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Kapteni mstaafu James Yamungu, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kulaani kitendo hicho. Yamungu alisema chanzo chake ni mfuasi wa chama kimoja kuchana bendera ya Chadema.

  " Nimewaagiza wafike ofisini kwangu na taarifa za tukio hilo nitazitoa baadaye.

  Viongozi wa Chadema wa Wilaya ya Maswa hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo kwa kile kilichoelezwa kuwa walikuwa katika shughuli za kampeni.

  Ofisa mmoja mwandamizi wa Jeshi la Polisi wilayani Maswa, jana alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukataa kuzungumzia kwa undani kwa madai kuwa si msemaji.

  Ofisa huyo alisema mtuhumiwa anayeshikiliwa huenda akafikishwa mahakamani leo kujibu mashtaka.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Daud Siasi, alipotafutwa jana kuzungumzia tukio hilo, simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.

  Source: Nipashe Oct 11
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  huu ugonjwa wa kuficha madudu ya ccm umeongezeka sana sasa.
  hata kwenye channel ten wakiwa wanaripoti vurugu au madudu ya ccm wanatumia neno hili CHAMA KIMOJA CHA SIASA. naona rushwa imeingia upande wa pili wa masikio sasa.

  Waandishi acheni uoga andikeni kuwa CCM wamcharanga mapanga fulani. Mbona mmeripoti kuwa aliyefanyiwa ni chadema?

  Wakuu wanajukwaa. mimi naside na mkapa kwamba bongo hatuna waandishi maana wengi ni waganga njaa big time.
   
 3. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Hakuna atakayeingia ikulu kwa mtanzania kumwaga damu
   
 4. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inakera sana, sasa wanaona kutaja moja kwa moja watakosa ulaji? hawajiamini, wanategemea makombo kutoka ccm, anataka ukuu wa wilaya ila shule, hawajui nini cha kufanya. Ngoja kisima kikauke tuone nani mchapa kazi na nani mkwapuaji tu.
   
 5. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 180
  NIPASHE acheni kuandika kwa woga. Iweje muogope hata kumtaja aliyekamatwa? Kuna siri gani?

  Naona tusubiri mwana JF wa sehemu hizo atuambie hapa Mbunge wa CCM aliyetajwa na hao majangili ni nani, na polisi wanamchukulia hatua gani.

  NIPASHE naona Dr. Slaa akishaanza kuongoza Tanzania mwezi ujao hatawapeni hata interview. Hamna ujasiri wa kutosha fani yenu.

  NIPASHE gani wasiothubutu KUWAPASHA CCM.

  PS: Aliyecharangwa mapanga aongezwe kwenye orodha ya wanaokomboa Tanzania kwa damu yao.
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Kikwete(akiwa Songea huku akicheka-cheka): "Msiwachague watu wanaotaka kuingia ikulu kwa kumwaga damu"
   
 7. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mbona Shimbo hakemei mambo haya?
   
 8. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Nulishangaa TBC kukwepa kuwaeleza watu kuwa ujumbe wa SMS uliosambazwa kwenye simu ulimchafua Slaa na kwamba hiyo ni siasa ya maji taka. Ingekuwa ni Kikwete na CCM wangesema wahusika waliochafuliwa. Hata TCRA hawakulaani kitendo hicho. Wajue wamwkalia kuti lililoliwa na mchwa. November hawana kazi. Wapo WaTZ wengi wanaoweza kuchukua nafasi zao na kuendesha hayo mashirika kwa ufanisi zaidi bila kujikomba.
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa mujibu wa kumbukumbu zangu, mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la maswa magharibi ni Robert Simon Kisena.

  Nipashe hawawezi kumtaja jina, bosi wao(Mengi) anaweza kuwafukuza kazi!!
   
 10. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hivi siku hizi CCM inaitwa chama fulani?

  Maana mkoa wa mara nao habari ni hiyo hiyo, stupid boys! Kama ndo uongozi unatakwa kwa nguvu hivyo nina doubt kama waongoza "operesheni" ni viongozi au magaidi
   
 11. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,550
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  Nipashe :
  Hivi huyu mwandishi ameweza kujua jina la aliyecharangwa mapanga, bendera iliyochanwa kuwa ni ya CHADEMA, lakini ameshindwa kutaja hata jina moja la waliofanya hizo fujo wala chama ambacho wanatokea... maana yake nini kama sio unafiki na uzandiki tu....
   
 12. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,550
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  Mween;
  Nilishangaa sana TCRA eti wanasema kwa sasa hawawezi kulifanyia kazi hilo la SMS, yaani kabisa huku akitabasamu!!! lakini nakuhakikishia ingekuwa message ile inamsema JK, ungesikia kuanzia TBC1 mpaka TCRA kila mtu ana laani na yangewezekana mengi sana!!!
  Haisaidii wakati ni ukuta.... kila kitu kina mwisho....
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Si wanasema CHADEMA watamwaga damu...nadhani the opposite is true
   
 14. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #14
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Generali Shimbo, UPO? Au kwa sababu unavaa magwanda ya kijani?

  Mi nawaomba wapenda haki wote waliopo huko, msipoteze muda na polisi. Dawa ya moto ni moto. Kwani mapanga yanauzwa bei gani...
   
Loading...