Apata kipigo kwa kumuandalia chakula baba mwenye nyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Apata kipigo kwa kumuandalia chakula baba mwenye nyumba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dr. Chapa Kiuno, Nov 2, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Monday, November 02, 2009 10:42 AM
  MSICHANA WA kazi za ndani aliyefahamika kwa jina moja la Sakina [22] mkazi wa Mabibo Hostel amejikuta akiwa kwenye wakati mgumu wakati alipomuandalia chakula baba mwenye nyumba, alipoona mkewe amechelewa kurudi nyumbani kwake hapo.

  Chanzo cha habari hii anayeishi karibu na lilipotokea tukio aliiambia NIFAHAMISHE kuwa msichana huyo alipigika kutokana na kitendo chake cha kumuandalia bosi wake wa kiume chakula.

  Alidai kuwa wakati anaanza kazi kwa dada huyo miezi mitano iliyopita bosi wake wa kike alimwambia kuwa afanya kazi zote ila mambo yanayomuhusu mume wake asiyaingilie kabisa ikiwemo na kumuandalia chakula na kufua nguo za mume wake huyo.

  Alidai siku ya tukio Jumamosi majira ya saa 3 usiku, msichana huyo alikuwa amepika chakula na kula na mtoto wake anayemlea mwenye umri wa miaka minne, na wakati huo bosi wake huyo wa kike alikuwa ametoka na kuchelewa kurudi na bosi wake wa kiume huyo alikuwa amerudi kwenye majira ya saa moja jioni.

  Hivyo msichana huyo alipoona mama yake huyo amechelewa kurudi hadi majira ya saa 3 na nusu, aliona ni vyema amuandalie chakula bosi wake huyo kwa kuwa mama yao alikuwa amechelewa.

  Alidai alimuandalia chakula hadi alipomaliza kula mama yake huyo alikuwa hajarudi na yeye aliingia ndani kulala.

  Ilidaiwa kuwa mama huyo aliporudi ambapo ilidaiwa alikwenda kwenye sherehe ya Kitchen Patry aliingia nyumbani kwake hapo kwenye majira ya 4 na nusu usiku, na kuingia jikoni kumuandalia chakula mume wake ili waweze kula kwa pamoja.

  Wakati alipomaliza kuandaa chakula na kumkaribisha mume wake huyo kipenzi asogee mezani wapate chakula kwa pamoja ndipo mume wake huyo alipomjibu “ He mbona mimi nimeshakula zamani Sakina alishaniandalia endelea tu mke wangu mi nishakula”

  Baada ya kupata majibu hayo kwa mume wake huyo moja kwa moja aliingia kwenye chumba alicholala msichana huyo na kumuamsha na kumuuliza baba alishakula na msichana huyo kujibu ee alishakula nilimuandalia”

  Bila kutarajia mama huyo alianza kipigo kwa msichana huyo na kumwambia “nilikwambiaje wewe si nilikwambia kazi hiyo uniachie mwenyewe kwa nini ulimuandalia kwani yule mume wako? huku akiendelea kumpa kichapo cha nguvu

  Kipigo kilivyokuwa cha nguvu ndipo msichana huyo uzalendo ukamshinda na kuanza kupiga kelele hadi baba huyo kukimbilia chumbani huko kuuliza imekuwaje ndipo msichana huyo alimwambia kuwa ananipiga kwa kuwa nilikuandalia chakula alishanikataza nisiwe ninakuandalia.

  Alianza kumkemea mkewe kwa kumsihi sio kitendo kizuri na baba huyo kurudi chumbani kwake kulala, mama huyo alipooona amepata upenyo aliendelea kumpiga msichana huyo kwa hasira na msichana huyo kukimbilia nje huku akilia na ndipo majirani wa karibu walipokimbilia na kumsihi mwenzao huyo amsamehe.

  NIFAHAMISHE siku iliyofuata ilitembelea eneo la tukio na kukuta msichana huyo akilalama akitaka mshahara wake ili aweze kurudi kwao na kudai anamdai dada huyo mshahara wa miezi mitatu nyuma.

  Alipomwambia bosi wake huyo dhamira ya kutaka kuondoka kwao alimwambia asiondoke na kudai kuwa alikuwa na jazba na alimwambia alikuwa anamuonya kwani kuonywa ni kawaida akikosa.

  Msichana huyo aliiambia nifahamishe kuwa anabaki hapo akisubiri kuandaliwa mshahara wake na akiupata ataondoka kwao.


  Na Pilly Kigome, Dar

   
 2. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  makubwa haya
   
 3. October

  October JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tabia nyingine za ajabu sana, Huyu mama anajifanya ana upendo sana kwa mumewe au ni ushamba ndo unaomsumbua????
   
 4. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  mahaba gani haya wajameni?hivi huyu mama hajui siku hizi hawa wasaidizi wanatakiwa wanyenyekewe sana,sababu hata kuwapata ni bahati mno,sasa atakapoondoka ndio ataona cha mtema kuni!!!
   
 5. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  ee mambo mengine wakina mama cjui tunayafanya tukifikiria nini?
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Huuu ni WIvu wa kijinga sana
   
 7. s

  siyajui Member

  #7
  Nov 2, 2009
  Joined: Sep 4, 2009
  Messages: 26
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hivi wewe mama vipi? si ungewahi kurudi toka kwenye hiyo kitchen party yako ? ovyoooooooo!
   
 8. M

  Msindima JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu sidhani kama ni wivu,huyo mama nahisi ana vitabia flani hivi kwa hiyo kwa vile yeye yuko hivyo anahisi mume wake akiandaliwa chakula na house maid labda jamaa atarusha karata kwa haouse maid,huyo mama ni mwizi kwa hiyo anahisi watu wote wezi kama yeye,tena wala asijidai anampenda mume wake,maana angekua anampenda mume wake wala asingekaa kwenye kitchen party mpaka muda huo,kwa hiyo mume wake angemsubiri mpaka saa nne ndo aje apike wale? Wanawake wengine hovyo sana.
   
 9. M

  Msindima JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  October,ushamba unamsumbua wala hana upendo kwa mume wake anazuga tu huyo.
   
 10. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa mkuu. Housegirl ni mtu wa kuonyeshwa upendo sana kama mtoto wako vile. Mtu huyu ukimkorofisha naye akakubali kutumiwa na shetani anaweza kuwateketeza nyumba nzima. Maana ndo anayewaandalia chakula, ndo anayekaa na watoto wenu muda mwingi kwahiyo ni muhimu kukaa naye kwa upendo na ni ki-MUNGU pia. Nilishawahi kusikia kisa kimoja mahali fulani housegirl aliamua kumbanika (Kum-bake) mtoto wa tajiri wao baada ya kuteswa na kunyanyaswa mara kwa mara. Mama aliporudi nyumbani siku hiyo akahisi harufu nzuri kama ya nyama imeokwa safi kwenye oven. Kuingia ndani hakumkuta housegirl na kufungua kwenye oven akakutana na mtoto wake mchanga akiwa ndani ya oven. Soooo sad. Kwahiyo akina mama kaeni kwa akili na kwa upendo na housemaids wenu.
  Mbarikiwe.
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hawa ndio wanawake wanaotaka usawa hawa, au hili kabila jengine?
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  mi mama ya namna hii ipo mingi na huw inatabia za kijinga na ni mijizi kwa waume zao. Lakini ngekuwa mimi ndo mme wake hapo ndo ingekuwa imekula kwake huyo mama.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Huyo mama ana tatizo la insecurity linalosababisha paranoia. Inabidi amuone tabibu mapema.
   
 14. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Kama mume ni mlafi na kila sketi ikipita anaitaka hata umuandalie chakula na kumlisha haitasaidia. mtu umekwenda kitchen party masaa kadhaa unajua ulipotoka huku nyuma kiliendelea nini? ladies tujiamini kidogo itasaidia sana na kuepusha viroja kama hivi
   
 15. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hilo ni tatizo la kujidai kupenda, kumbe hata kusaidiwa na hg angemshukuru na kama anampenda mumewe amwombe samahani kwa kulate kiasi cha yeye kushindwa kumuandalia msosi, mara nyingi thinking capacity ya wanawake inapokuja kwa mabo ya namna hii huwa chini.Kupata house girl kazi sana, mimi natafuta sana hg kwa sasa ni 4th month sijapata, na sijui ntapata lini
   
 16. M

  Msindima JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  rmashauri umenena mkuu,ni kweli kabisa tunapaswa tuishi nao vizuri kama vile ambavyo tunaishi na watoto,ndugu,jamaa zetu,na tusiwafanye wao kama watumwa.
   
 17. K

  Konaball JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Nina wasiwasi huyo mama kabla ajaolewa alikuwa HG wa huyo jamaa sasa anaogopa yasimkute kama alivyofanya yeye hapo zamani!!!
   
 18. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sio wivu ni kushindwa kwa limbwata la huyo mama fedhuri
   
Loading...