Anyang'anywa Uraia Baada ya Kuoa Mke wa Pili

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
4531766.jpg

Pasipoti ya Uswizi Wednesday, May 26, 2010 1:38 AM
Mwanaume wa Uturuki ambaye alipata uraia wa Uswizi baada ya kuoa mwanamke wa Uswizi amenyang'anywa uraia baada ya kuoa mke wa pili kwa siri. Mturuki huyo ambaye alipewa uraia wa Uswizi baada ya kumuoa mwanamke raia wa Uswizi, alinyang'anywa uraia na mahakama ya Uswizi jana baada ya kugundulika ana mke mwingine nyumbani kwao nchini Uturuki.

Mturuki huyo alikuwa akiishi maisha ya ndoa na mke wake wa Uswizi kwa miaka 26 lakini wakati huo huo alikuwa na mke mwingine nchini Uturuki ambaye amezaa naye watoto wawili, limeripoti shirika la habari la Uswizi, ATS.

Mwaka 2003 alipewa uraia wa Uswizi kutokana na ndoa yake na mwanamke huyo raia wa Uswizi.

Mke wake aligundua kuwa mumewe ameoa mke mwingine nchini Uturuki lakini alikaa kimya hadi hivi karibuni ikiwa imepita miaka mitano alipoamua kupeleka malalamiko wizara ya uhamiaji.

Wizara ya uhamiaji iliamua kumnyang'anya uraia Mturuki huyo ambaye aliamua kwenda mahakamani kukata rufaa.

Mahakama ya rufaa ya Uswizi imetoa uamuzi jana na kuamua Mturuki huyo anyang'anywe uraia na pasipoti ya Uswizi aliyopewa.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=4531766&&Cat=2
 
Sasa wale jamaa wanaopenda uroda kwa kuoa wake wengi inamaana hawatakiwi Uswisi? Au kosa lake ni kuficha ndoa yake ya Turkey?
 
mbona jk hajafikuzwa kwa kuoa mke wa pili kinyemela?????????????????????
au katiba yetu inaruhusu????
 
mbona jk hajafikuzwa kwa kuoa mke wa pili kinyemela?????????????????????
au katiba yetu inaruhusu????

Mkuu JK ni raia!!! hawezi kufukuzwa uraia wake. Huyu Mturuki alipewa uraia kwa kuwa alioa kule but not a Swiss native!! Sana sana huyu bi yetu mdogo kama ana uraia wa Oman na akawa ameukana ili apate wetu (sijui kama Oman wana dual citizenship) na wakiachana na Mkulu hapo sijajua sheria zetu za uraia zinasemaje au pengine ni hiari yake kubaki na uraia wetu au ni lazima aukane tena!!! Watu wa uhamiaji kama wapo hapo watuelimishe kwa upande wa Tz iko vipi?

 
Wakuu wangu sheria za Ulaya Mke ni mmoja ndie anae tambulika hata hapo kwa huyo jamaa Uturuki Serikali yake inamtambuwa Mke Mmoja ingawa Waturuki Karibu wote ni Waislam Serikali yao haifuati Mambo ya Dini. Mwanzilishi wa Uturuki Mzee Mustafa Kemal Ataturki ndie alieanzisha hiyo sheria ya kuowa Mke Mmoja ingawa waweza kuowa Mke wa pili kwa njia ya Dini ingawa Serikali ya Kituruki haitomtambuwa huyo mke wako uliye muowa kwa njia ya Dini lakini Mwenyeezi Mungu anamtambuwa kwa njia ya Dini ya Kiislam sasa huyo jamaa alimuowa Mke wa Uswizi ili apate Makaratasi sasa amechomwa jamaa zake ndio maana siri yake imegundulikana kuwa alikuwa na Mke Mwengine kwao Uturuki na ndio maana Serikali ya Waswizi wameamuwa kumnyang'anya Uraia wake pamoja na Passport yake Uswizi hizo ndio sheria za wazungu kazi kweli ipo. Nauliza Swali ndugu zangu Wakuu Je Kwetu sheria kama hizo zipo?
 
wamemkomesha, naye amezidi uzinzi.....kuoaoa wake wawili dini ya aina gani iyo? dini inayosapoti uziinzi?
 
Back
Top Bottom