Anthony Lusekelo: Haijawahi kutokea dunia kwa nchi kununua ndege nane kwa mpigo

Sugu alisema bungeni kuwa wapambe wa jiwe wanasifia mpaka wanapitiliza hadi asifiwaye anashtuka na kuchukia
Naomba muamini kama haijawahi kutokea nami narudia haijawahi kutokea. Mashirika na Nchi zoote ukisikia wamenunua ndege huwa ni some kind of lease na si cash kama ilivyofanya serikali. Wametowa cash wakati kawaida huwa ni mkataba unalipa kidogo kidogo na riba ipo. Yuko sahihi labda kama hamtaki kumuelewa.
 
Nafikiri lengo kubwa la press conference lilikuwa kuwaonyesha kuwa yeye yupo na ni mzima wa afya sababu kuna wazushi walizusha kafa wengine wakasema hatavuka mwezi wa tano.Hayo mengine aliyoongea ni mazungumzo baada ya habari
Kapicha tafadhali ka jana ka huyu kada mzee wa praise and worship team
 
Wee umekariri vibaya ni kuwa alikuwa anamfagilia magufuli na kusema kuwa haijawahi tokea nchi yoyote dunia kwa kununua ndege hizo 8 kwa pamoja akasema ni tanzania pekee imeweza hivyo mh rais anatakiwa kupongezwa kwa hilo.na unavyosema hayupo sawa sio kweli maana hakuna swali hata moja aliulizwa na akashindwa kujibu.
Ndio sifa hizo ambazo hata Magufuli anakasirika maana si kweli kwamba hakuna nchi imewahi kununua ndege nane .
 
Iran aliagiza ndege 80 siyo mia, hata Uturuki kaagiza ndege 100 za kivita aina ya F35 kutoka Marekani japo wametofautiana na Marekan kuelekea kusitisha uuzwaji huo wa ndege hizo za hatari katika uwanja wa medani zenye teknolojia ya Stealth,baada ya Uturuki kutaka kuununua mtambo wa kujikinga na mashambulizi ya anga toka Urus aina ya S400.

Ila nilikuwa nakuunga mkono kuwa nchi nyingi zinanunua ndege nyingi tu kwa mpigo, sema Rais kajitaidi sana hata kuzinunua ndege hizo sita- nane,

Kazi ibaki kwa shirika kupambana kupata soko. Tulilia sana kuwa shirika limekufa,sasa Mh. Kalifufua Sema watendaji wa pale Shirikani akaze maana....
 
Ahsante mkuu kwa marekebisho
 
Wee umekariri vibaya ni kuwa alikuwa anamfagilia magufuli na kusema kuwa haijawahi tokea nchi yoyote dunia kwa kununua ndege hizo 8 kwa pamoja akasema ni tanzania pekee imeweza hivyo mh rais anatakiwa kupongezwa kwa hilo.na unavyosema hayupo sawa sio kweli maana hakuna swali hata moja aliulizwa na akashindwa kujibu.
Nilichosema ndicho ulichorudia, fikiri kabla ya kuandika. Ungekuwa unaishi duniani ungejua zipo nchi zinanunua ndege zaidi ya hamsini (50) kwa mpigo! Maswali ya waandishi wa habari Tanzania huwa hayajanona hivyo siyapendi.
 
Naomba muamini kama haijawahi kutokea nami narudia haijawahi kutokea. Mashirika na Nchi zoote ukisikia wamenunua ndege huwa ni some kind of lease na si cash kama ilivyofanya serikali. Wametowa cash wakati kawaida huwa ni mkataba unalipa kidogo kidogo na riba ipo. Yuko sahihi labda kama hamtaki kumuelewa.
Kwa hiyo huyo wa kwetu ni zumbukuku kwa kulipa cash sio?.Maana siamini hizo nchi zinazoagiza ndege zaidi ya mia,au zaidi ya 50,kama kweli hazina hela ya kuzilipa cash.Labda kama ni suala la uangalizi maalumu kwa hizo ndege,ikiwa pamoja na usalama wake,kabla ya kulipa cash.Pengine ndio sababu ya kulipa kidogo kidogo.
 
Jana Jumamosi kwenye kituo cha runinga cha Star TV ulioneshwa mkutano wa waandishi wa habari na mzee wa upako, mkutano huo ulikita kwenye siasa na kujitambulisha rasmi kuwa yeye ni kada wa CCM toka utotoni!

Lusekelo aliongea mambo mengi kuhusu awamu hii ya Magufuli yaliyokuwa na lengo la kumtonya amkumbuke na yeye huko aliko, hali si nzuri kwake. Mzee wa upako alielezea alivyo kuwa akiimba msitari wa mbele kwenye mikutano ya CCM ambampo kuthibitisha hill alitoa kibwagizo cha wimbo wa CCM.

Inaonesha wazi kuwa mambo hayaendi sawa kiasi cha muonekano wake kuwa si ule tuliouzoea kumuona, ucheshi haupo tena.
Clip tafadhali
 
Nilichosema ndicho ulichorudia, fikiri kabla ya kuandika. Ungekuwa unaishi duniani ungejua zipo nchi zinanunua ndege zaidi ya hamsini (50) kwa mpigo! Maswali ya waandishi wa habari Tanzania huwa hayajanona hivyo siyapendi.
Maswali yao yanakuwa kana kwamba yanamuongoza anayeulizwa kuyajibu vizuri.Hatuna waandishi wa habari ambao ni critical questioners
 
Kuhusu kukubaliana nae au kutokubaliana nae hilo ni suala la mtu binafsi maana yeye alikitoa kama mshangao wake kwa nchi kama tanzania kufanya hivyo,na kwa hapa tz tukilizunvumzia hili tangu huko tuliko toka hata mimi lazma niungane nae.
Ondoa mdomoni hiyo bangi ona sasa ulichoandika! Eti hakuna nchi duniani iliyowahi kununua ndege zaidi ya name kwa mpigo, hata hizo nane zimenunuliwa lini! Thibitisha hapa ama tulete kitabu cha manunuzi?
 
Nafikiri lengo kubwa la press conference lilikuwa kuwaonyesha kuwa yeye yupo na ni mzima wa afya sababu kuna wazushi walizusha kafa wengine wakasema hatavuka mwezi wa tano.Hayo mengine aliyoongea ni mazungumzo baada ya habari
Stress stress stress
 
Yuko sahihi kabisa huyo Lusekelo.
Ana dunia yake mwenyewe anayoifahamu yeye mwenyewe.
Yaani kimwenyewe mwenyewe.
 
Atakuwa hayuko sawa huyo hakika.Maradhi yashaanza kumtafuna.Ndege nane,wakati kuna nchi zinaagiza ndege zaidi ya mia moja kwa mpigo!!.Nchi kama Iran iliagiza ndege mia moja kutoka Airbus,achilia mbali kutoka Boeing.China wameagiza ndege karibia 60 kutoka Airbus, achilia mbali kutoka Boeing.Halafu anakuja mnywa konyagi mmoja na kutapika uharo.Mungu mnusuru mja wako Lusekelo
Mkuu huyu naye ni mjinga kama wajinga wengine,ndiyo unakuta msomi mzima unaenda kuabudu kwake,kama anaweza kupotosha haya ni Mara ngapi amewapotosha waumini wake kwenye neno la Mungu.

Mimi naamini kwenye uokovu siamini Manabii waongo kama huyu,wengi ni matapeli wa sadaka za waumini.
 
Hakika mkuu 🙏🙏
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom