Anthony Diallo abanwa kona zote nne

Anthony Diallo abanwa kona zote nne

Tenda wema nenda zako,Kama ccm walimlipa basi nayeye alipe kodi Kama hawakumlipa basi wanye hesabu wamlipe ili na yeye alipe,lakini inavyo onekana ccm ilimlipa hela nyingi sana ndoo maana raisi anataka angalau alipe kodi na hiyo hela iwezekana ameweka nje ya nchi,

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Lakini unawapongezaje wakati wanafanya kazi bila kutumia akili? Taasisi kubwa Kama ile inao watumishi wengi sana ambao ajira Yao ndio maisha Yao. Wanashindwa nini hao TRA kudhibiti mapato ya Sahara na kukata sehemu ya deni Lao kidogo kidogo kulifidia huku maisha ya Watanzania waliopo pale yakiendelea?
Sikatai Diallo ali mess up kuchanganya siasa zake na kituo cha habari na wengi walichukizwa na jambo hilo, lakini hakuna Sababu za kuingiza chuki ya kuumiza maisha. Mambo ya chuki na visasi waachiwe ccm ambao wameshaonyesha kuwa hiyo ndio sera Yao hasa awamu hii.
SAHARA MEDIA kwa uwekezaji ilio nao ingejisajili DSE na kuuza share zake ili kuchanganya wamiliki na taaluma mpya ingeingia hasa katika management tofauti na sasa ambapo ni yeye mwenyewe na undugu ndio umeshika kasi. Au jingine Diallo aachane kabisa na siasa afanye biashara tuu.
Ninachofikiria ni kwamba wamembeba muda mrefu imeshindikana sio la kushabikia ila halijakaa vizuri sana maana lina adhari Kubwa kiuchumi .

Kikubwa ni kwamba itauzwa ili wenye mtaji waiendeshe hamna jinsi nyingine .

Pia hatuwezi kushabikia swala kama hili labda tu kama hatuelewi maisha kwa ujumla wake Star media ni kampuni Kubwa sana kufungwa na kufilisiwa.
 
Dialo kaajiri watanzania wangapi?

Anyway,hili ni funzo kwa wamiliki wengine wa vyombo vya habari na matajiri wa nchi hii kwa ujumla.

Mawaziri wa leo mna la kujifunza pia pamoja na wabunge mnaotunga sheria za nchi hii.
Hamna watz aliwaajiri bali wasukuma tu
 
Ndo si raia?? Arudi kwao,anamambo ya kishamba sana acha waibuke matajiri wengine walosafi. Alitumika uchaguzini kueneza hâta vya uongo
 
Ndo si raia?? Arudi kwao,anamambo ya kishamba sana acha waibuke matajiri wengine walosafi. Alitumika uchaguzini kueneza hâta vya uongo
Wewe jamaa mbona unaropoka ropoka nan kakwambia dialo sio raia au umelogwa

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Afu kwel yule mmasai anaweza kununua pesa ipo pale wale sahara mitambo yao ina nguvu balaa

Lakin si nasikia na yeye anawa dai ccm pesa za kipind cha kampeni alikuwa anarusha mubashara mikutano ya ccm

Ila ccm wajiangalie sana siku za mbelen huko watapata ugumu sana kuja kupewa airtime na hiv vyombo vya habari rejea ya shigongo, sasa dialo wao wanatumia tu kulipia hawataki

Wengine mjifunze biashara isimame kama biashara ukichanganya ukada na biashara lazima ile kwako naona dialo analia tu

Ila mwisho nasema alipe tu kodi
Wanasema hakuwa na mkataba wowote na CCM, ila ukabila na ukada
 
Watu wanamjadili Diallo kwa kumuona magazeti.Diallo ni habari nyingine kabisa atapeta tu
 
Ukiwaalika watu wengine kufanya interview ktk Kituo chako wanatia nuksi. Rejea bashite interview

Post sent using JamiiForums mobile app
 
[HASHTAG]#Vyumavimekaza[/HASHTAG] heshima imerudi mtaani...
 
Kwa jinsi Diallo alivyosimamia zoezi LA kuuchafua upinzani mwaka 2015 mwache akomeshwe labda 2020 Mungu akimjalia atakumbuka suala LA Media Social Responsibility

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Ila watanzania hatupendani sana
Siyo kweli, watanzania tunapendana ila kuna watu walifanya CCM ni chaka la wakwepa kodi. Kwa nini wengine walipe halafu CCM wasilipe? 4.5bn unaona ndogo?Kila siku muuza mchicha anakimbizana na mgambo wajiji alipe kodi. Sizonje hataki ujinga .
 
Diallo alikuwaga team Lowassa kabla hajahamia team Membe,lazima akiwa Team Lowasa alifanyaga figisu kubwa mpaka naona hata favor hafanyiwi tena.JK njoo umuokoe Diallo atakufa kwa pressure.
Ok, hapo nishaunganisha dots tayari!
 
Uzembe wake kwakweli...

Lakini mbona yeye tu... Vituo viko vingi nchini.. Vinalipa kodi!?
 
Lowasa akanunua sahara kama itauzwa kwa mnada...wanavifaa vyenye nguv sn
 
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza Anthony Diallo yuko kwenye nafasi mbaya kisiasa, kimaisha, kibiashara na hata kimahusiano na jamii.

Baada ya kituo chake cha matangazo cha Star Television kutiwa kufuri za nyororo na TRA kwa kuidai kampuni yake zaidi ya shilingi 4.5bn, Diallo amefikwa na balaa jingine la pili baada ya benki moja ya jijini Mwanza kumshtaki kwa kushindwa kuilipa zaidi shilingi 600m alizoiomba benki hiyo iwe inawalipa mishahara wafanyakazi wa kampuni zake.

Pigo jingine la tatu ni hatua ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kuanza kutroti kuiwania nafasi yake ya uwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, nafasi ambayo kwa njia moja ilikuwa ikimkinga kidogo na bughudha ndogo ndogo za vyombo vya dola na taasisi za fedha.

Pigo jingine linalomuathiri bwana mkubwa huyu aliyewahi kuwa waziri wa wizara mbali mbali katika awamu mbili zilizopita na ambaye Rais Kikwete aliwahi kumwombea kwa Magufuli wakati wa kampeni za urais ampe upendeleo wa kibiashara katika shughuli zake, ni kitendo cha kutengwa na waliokuwa washirika wake wa vyombo vya habari MOAT kumtenga baada ya kuonekana kukiuka taratibu zao walizojiwekea.

Kwa kifupi hivi sasa Diallo kashika njia inayoelekea katika lango kubwa lililoandikwa OFISI YA MUFLISI.
Never ever hung around With fake persons, you might be building your fake future!

If you know your enemy than yourself you shall never suffer a defeat
 
Acheni kuingiza siasa kwenye masuala ya kodi. Walichofanya TRA Ni kujitenga na siasa na kufanya kazi waliyosomea, wanatakiwa kupongezwa na sio kubezwa
Sio siasa....kinachotupa raha ni kuvuliwa nguo kwa wazee tuliohisi watu b4.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza Anthony Diallo yuko kwenye nafasi mbaya kisiasa, kimaisha, kibiashara na hata kimahusiano na jamii.

Baada ya kituo chake cha matangazo cha Star Television kutiwa kufuri za nyororo na TRA kwa kuidai kampuni yake zaidi ya shilingi 4.5bn, Diallo amefikwa na balaa jingine la pili baada ya benki moja ya jijini Mwanza kumshtaki kwa kushindwa kuilipa zaidi shilingi 600m alizoiomba benki hiyo iwe inawalipa mishahara wafanyakazi wa kampuni zake.

Pigo jingine la tatu ni hatua ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kuanza kutroti kuiwania nafasi yake ya uwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, nafasi ambayo kwa njia moja ilikuwa ikimkinga kidogo na bughudha ndogo ndogo za vyombo vya dola na taasisi za fedha.

Pigo jingine linalomuathiri bwana mkubwa huyu aliyewahi kuwa waziri wa wizara mbali mbali katika awamu mbili zilizopita na ambaye Rais Kikwete aliwahi kumwombea kwa Magufuli wakati wa kampeni za urais ampe upendeleo wa kibiashara katika shughuli zake, ni kitendo cha kutengwa na waliokuwa washirika wake wa vyombo vya habari MOAT kumtenga baada ya kuonekana kukiuka taratibu zao walizojiwekea.

Kwa kifupi hivi sasa Diallo kashika njia inayoelekea katika lango kubwa lililoandikwa OFISI YA MUFLISI.
Wahenga walisema hakuna marefu yasiyo na ncha

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom