Anthony Diallo abanwa kona zote nne

Anthony Diallo abanwa kona zote nne

Diallo alikuwaga team Lowassa kabla hajahamia team Membe,lazima akiwa Team Lowasa alifanyaga figisu kubwa mpaka naona hata favor hafanyiwi tena.JK njoo umuokoe Diallo atakufa kwa pressure.
Kweli yanaweza kutokea yaleyale ya Capt. Komba
 
Wana JF ingekuwa vyema tungepata kwanza burudani ya ile video clip ya wimbo wetu wa kuisoma namba wakati tukimkaribisha Dialo kwenye maisha ya ushetani. TAFADHALI MWENYE ILE CLIP ATULETEE HAPA JUKWAANI
 
Ukiona mtu kang'ang'ania CCM kwa kujipendekeza kutoa vimisaada CCM Kama alivyofanya Diyalo kwa kujifanya bwana huruma wakutangaza live mikutano yote ya kampeni ya Magufuli ujue kuwa mtu huyo siyo msafi kwa kuwa CCM ndipo mahali salama kwa watu wachafu.
Sasa kavuna ujinga wake na magufuli anajiandaa kwenda kumpima mkojo
 
Alijiona mjanja kumpa Bashite Airtime sasa leo ngoja afurahie matapishi yake
 
Alijiona mjanja kumpa Bashite Airtime sasa leo ngoja afurahie matapishi yake
Bashite Maliyamungu anamcheka sasa na hapokei Simu zake ndiyo kwanza ka mshauri Mtukufu malaika toka chato wampime mkojo kwanza
 
Kweli
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza Anthony Diallo yuko kwenye nafasi mbaya kisiasa, kimaisha, kibiashara na hata kimahusiano na jamii.

Baada ya kituo chake cha matangazo cha Star Television kutiwa kufuri za nyororo na TRA kwa kuidai kampuni yake zaidi ya shilingi 4.5bn, Diallo amefikwa na balaa jingine la pili baada ya benki moja ya jijini Mwanza kumshtaki kwa kushindwa kuilipa zaidi shilingi 600m alizoiomba benki hiyo iwe inawalipa mishahara wafanyakazi wa kampuni zake.

Pigo jingine la tatu ni hatua ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kuanza kutroti kuiwania nafasi yake ya uwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, nafasi ambayo kwa njia moja ilikuwa ikimkinga kidogo na bughudha ndogo ndogo za vyombo vya dola na taasisi za fedha.

Pigo jingine linalomuathiri bwana mkubwa huyu aliyewahi kuwa waziri wa wizara mbali mbali katika awamu mbili zilizopita na ambaye Rais Kikwete aliwahi kumwombea kwa Magufuli wakati wa kampeni za urais ampe upendeleo wa kibiashara katika shughuli zake, ni kitendo cha kutengwa na waliokuwa washirika wake wa vyombo vya habari MOAT kumtenga baada ya kuonekana kukiuka taratibu zao walizojiwekea.

Kwa kifupi hivi sasa Diallo kashika njia inayoelekea katika lango kubwa lililoandikwa OFISI YA MUFLISI.
Kweli njia ya mnafiki ni fupi, pamoja na kujikomba kote bado anaandamwa!
 
VISASI OYEE! DAH JPM BHANA, VISASI TU? HV WALIOMPGIA KURA WALIMTUMA KWA AJILI YA VISASI?

ANYWAY, DIALO AFILISIKE TU MANA TV YAKE NDO ILIYOTUFIKISHA HAPA, ALIONESHA LIVE MIKUTANO YOTE YA KAMPENI YA CCM.. SASA, HAPA KAZI TU.. HAKUNA KULALA, LAANA YA WANANCHI HAITAMWACHA DIALO SALAMA.. DIALO AKAPUUZA HAD AGZO LA MOAT?
 
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza Anthony Diallo yuko kwenye nafasi mbaya kisiasa, kimaisha, kibiashara na hata kimahusiano na jamii.

Baada ya kituo chake cha matangazo cha Star Television kutiwa kufuri za nyororo na TRA kwa kuidai kampuni yake zaidi ya shilingi 4.5bn, Diallo amefikwa na balaa jingine la pili baada ya benki moja ya jijini Mwanza kumshtaki kwa kushindwa kuilipa zaidi shilingi 600m alizoiomba benki hiyo iwe inawalipa mishahara wafanyakazi wa kampuni zake.

Pigo jingine la tatu ni hatua ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kuanza kutroti kuiwania nafasi yake ya uwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, nafasi ambayo kwa njia moja ilikuwa ikimkinga kidogo na bughudha ndogo ndogo za vyombo vya dola na taasisi za fedha.

Pigo jingine linalomuathiri bwana mkubwa huyu aliyewahi kuwa waziri wa wizara mbali mbali katika awamu mbili zilizopita na ambaye Rais Kikwete aliwahi kumwombea kwa Magufuli wakati wa kampeni za urais ampe upendeleo wa kibiashara katika shughuli zake, ni kitendo cha kutengwa na waliokuwa washirika wake wa vyombo vya habari MOAT kumtenga baada ya kuonekana kukiuka taratibu zao walizojiwekea.

Kwa kifupi hivi sasa Diallo kashika njia inayoelekea katika lango kubwa lililoandikwa OFISI YA MUFLISI.
yes..akubali kufilisika kwa ku file bankrupcy.
hapo itabidi ajiuzulu uenyeki wa ccm
maana ukiwa declared bankrupt huwezi baki kwenye uongozi wa umma na hata chama cha siasa.
 
Ila kusema ukweli Sahara media ilianza kuyumba siku nyingi. Haya tunayoona sasa ni hitimisho la safari ya mporomoko huo. Sahara media walikuwa na watangazaji classic kwa tanzania ... wakaanza kuondoka mmoja mmoja. Angalia ITV, Azam media, BBC, Deustche wote wamejichukulia talents za Sahara kiulaini. Media yoyote inaanza kupoteza audience inapopoteza presenters wazuri, na ikishapoteza audience maana yake watu hawawezi kulipia airtime tena, au utakuwa na makampuni ambayo watakuletea matangazo lakini watakusumbua kwenye malipo, au wanataka huge discount. Kwa hali hiyo, there is no way you can meet your operations costs.
 
hahahahhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh sasa mnam pressurize mpaka afe hizo 4bl mtazipata ? badala mumuambie afanye kazi usiku na mchana arudishe pesa mnaleta kukomoana kwa hali hii hatujengi maze tunabomoa acheni ushabiki wakijinga watanzania wangapi wanakuwa wamepoteza ajira kwa ujinga huu wa kufungiwa biashara kisa kodi kwani jamaa anahama wakae wayamalize walipane pole pole, watanzania wengi ni losers ndio maana mnashabikia ujinga mnaona sawa tu
POVU BILA YA SABUNI. MBONA YEYE ALISAIDIA KUWATUPIA MAWE UKAWA, ALISAHAU KUWA ANAISHI KTK NYUMBA YA KIOO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufa kwa Star TV,Radio free ni kufa kwa Ccm. Matajiri waliokuwa wanaibeba Ccm wanajiengua taratibu.
 
Diallo hajawahi kupatana na Lowassa maisha yake yote. I know them well. Tangu akiwa Naibu waziri chini ya Lowassa akiwa maji na baadae waliposuguana kwenye maliasili alipojaribu kumtimua ukurugenzi wa wanyamapori bwana Severe mkwe wa Lowassa na Severe alimwapia Diallo kuwa angeondoka yeye maliasili na kweli aling'olewa.

Ugomvi wa Diallo na Lowassa ni wa siku nyingi ila Diallo alikosea sana kumwingiza Lowassa ktk biashara zake.... chuki za Lowassa hakupaswa kuziingiza kwenye biashara kama media matokeo yake baada ya 2015 kampuni zake zimepoteza mvuto sana!

Post sent using JamiiForums mobile app
Uko sahihi. Akaingizwa kwenye scandal ya magogo.
 
Wewe,Diallo na Lowassa walishawahi kuwa marafiki wewe,tena wakaanzisha community airlines,wewe hao walikuwa wanamtandao wewe.Diallo alikuja kugeuka akaingia Membe team.
Urafiki wa kimtandao. Hawakuwa marafiki wa kiukweli.
Kumbuka issue ya Maliasili. Waziri Diallo kateua maafisa Waziri mkuu katengua.
 
Na watakapoanza kushikwa makalio hao jamaa zenu msije humu kutubania pua kwamba sababu ni wapinzani.

Hiki kirusi ni zaidi ya kile cha "WannaCry"
 
Back
Top Bottom