Anthony Diallo abanwa kona zote nne

Anthony Diallo abanwa kona zote nne

Kuchanganya biashara na ukada WA chama haijawahi kumuacha mtu salama! Ni ngumu sana kuwa na sympath na mtu Kama Diallo. Wengi kama yeye waliingia kwenye siasa especially ccm kama chaka la kukwepa kodi na kununua influence. Alipe kodi za serikali. Hakuna namna.

Ukitaka kuishi kwa favour hayo ndo matokeo yake.
 
Ama hakika umetimia ule msemo WA mhenga mmoja kutoka chattle kuwa "matajiri wataishi kama mashetani" ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni
Diallo vuna ulichopanda 2015
Dialo alikuwa na Roho mbaya kipindi cha uchaguzi aliwandama ukawa sana kwa vijembe na Uzushi hakujua malipo ni hapa hapa Duniani sasa ngoja apate fundisho
 
Dialo kaajiri watanzania wangapi?

Anyway,hili ni funzo kwa wamiliki wengine wa vyombo vya habari na matajiri wa nchi hii kwa ujumla.

Mawaziri wa leo mna la kujifunza pia pamoja na wabunge mnaotunga sheria za nchi hii.
Biashara na siasa kamwa havichanganywi!!!!! Lazima ufilisike. Scandinavia iko wapi?????
 
Binafsi huwa sikubaliani na TRA kufunga biashara kwa sababu za madeni ya kodi. Kitendo hicho huwa ni "lose-lose" kwa pande zote na kwa uchumi pia.
 
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza Anthony Diallo yuko kwenye nafasi mbaya kisiasa, kimaisha, kibiashara na hata kimahusiano na jamii.

Baada ya kituo chake cha matangazo cha Star Television kutiwa kufuri za nyororo na TRA kwa kuidai kampuni yake zaidi ya shilingi 4.5bn, Diallo amefikwa na balaa jingine la pili baada ya benki moja ya jijini Mwanza kumshtaki kwa kushindwa kuilipa zaidi shilingi 600m alizoiomba benki hiyo iwe inawalipa mishahara wafanyakazi wa kampuni zake.

Pigo jingine la tatu ni hatua ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kuanza kutroti kuiwania nafasi yake ya uwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, nafasi ambayo kwa njia moja ilikuwa ikimkinga kidogo na bughudha ndogo ndogo za vyombo vya dola na taasisi za fedha.

Pigo jingine linalomuathiri bwana mkubwa huyu aliyewahi kuwa waziri wa wizara mbali mbali katika awamu mbili zilizopita na ambaye Rais Kikwete aliwahi kumwombea kwa Magufuli wakati wa kampeni za urais ampe upendeleo wa kibiashara katika shughuli zake, ni kitendo cha kutengwa na waliokuwa washirika wake wa vyombo vya habari MOAT kumtenga baada ya kuonekana kukiuka taratibu zao walizojiwekea.

Kwa kifupi hivi sasa Diallo kashika njia inayoelekea katika lango kubwa lililoandikwa OFISI YA MUFLISI.

Kama kuna mtu aliwekeza kwenye media Tanzania hii Anthony Diallo ni wa mfano. Unaweza ukawa sehemu very remote ambapo hata community FM stations za eneo hilo hasisikiki ,lakini ukakutana na RFA very powerful. Kwa kweli alifanya kazi ambayoni nzuri. Kuna wakati nilikuwa natafakari na kujisemea investiment iliyofanywa na Diallo ilitakiwa kuwa imefanywa na TBC, au serikali ingeshirikiana naye kutumia network yake ili matangazo ya TBC Taifa yasikike nchi nzima. Pia tukumbuke ndiye mtanzania pekee aliyethubutu kuwekeza kwenye teknolojia ya matangangazo kwa vingamuzi- "continental" hawa akina Azam ni Asians. Matatizo kwenye biashara ni jambo la kawaida, i think badala ya kufurahia mwenzetu anaangamia tungesikitika na kumpa mawazo positive.
 
Diallo alikuwaga team Lowassa kabla hajahamia team Membe,lazima akiwa Team Lowasa alifanyaga figisu kubwa mpaka naona hata favor hafanyiwi tena.JK njoo umuokoe Diallo atakufa kwa pressure.
Hayo yote yanamkuta sababu ya makundi ndani ya CCM,kwani tokea huko nyuma hio deni lilikuwa limejificha wapi?
 
Ukiona mtu kang'ang'ania CCM kwa kujipendekeza kutoa vimisaada CCM Kama alivyofanya Diyalo kwa kujifanya bwana huruma wakutangaza live mikutano yote ya kampeni ya Magufuli ujue kuwa mtu huyo siyo msafi kwa kuwa CCM ndipo mahali salama kwa watu wachafu.
 
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza Anthony Diallo yuko kwenye nafasi mbaya kisiasa, kimaisha, kibiashara na hata kimahusiano na jamii.

Baada ya kituo chake cha matangazo cha Star Television kutiwa kufuri za nyororo na TRA kwa kuidai kampuni yake zaidi ya shilingi 4.5bn, Diallo amefikwa na balaa jingine la pili baada ya benki moja ya jijini Mwanza kumshtaki kwa kushindwa kuilipa zaidi shilingi 600m alizoiomba benki hiyo iwe inawalipa mishahara wafanyakazi wa kampuni zake.

Pigo jingine la tatu ni hatua ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kuanza kutroti kuiwania nafasi yake ya uwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, nafasi ambayo kwa njia moja ilikuwa ikimkinga kidogo na bughudha ndogo ndogo za vyombo vya dola na taasisi za fedha.

Pigo jingine linalomuathiri bwana mkubwa huyu aliyewahi kuwa waziri wa wizara mbali mbali katika awamu mbili zilizopita na ambaye Rais Kikwete aliwahi kumwombea kwa Magufuli wakati wa kampeni za urais ampe upendeleo wa kibiashara katika shughuli zake, ni kitendo cha kutengwa na waliokuwa washirika wake wa vyombo vya habari MOAT kumtenga baada ya kuonekana kukiuka taratibu zao walizojiwekea.

Kwa kifupi hivi sasa Diallo kashika njia inayoelekea katika lango kubwa lililoandikwa OFISI YA MUFLISI.
Mwache avune alichopanda, na namba ataisoma awamu hii
 
Back
Top Bottom