Ansbert Ngurumo: Wabunge wadhalilishwe, DC alindwe??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ansbert Ngurumo: Wabunge wadhalilishwe, DC alindwe???

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by M-mbabe, Sep 18, 2011.

 1. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,742
  Trophy Points: 280
  Another objective masterpiece from Ansbert Ngurumo.....READ ON!

  ================================================


  • Wabunge wadhalilishwe, DC alindwe?  Ansbert Ngurumo


  TUSEME ukweli. Yaliyompata Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, akiwa kwenye "uhalifu wa kisiasa" juzi si mazuri hata kidogo.

  Lakini ni vema ukweli wetu uvuke hapo. Tumtazame kama kiongozi wa serikali katika eneo lake, na tumuulize: alijiingizaje katika siasa za vyama vya watu?

  Alitarajia akisaidia hujuma za Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya wapinzani, wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wangemshangilia na kumpaka mafuta?

  Mikakati ya ushindi wa CCM ilikuwa inamhusu nini? Hakujua kuwa kwa kitendo cha kujifungia ndani na makada wa CCM, alikuwa anahujumu haki na kuhatarisha amani yake na wengine?

  Na kama alitaka kuwahujumu CHADEMA, ilikuwa lazima awafuate katika eneo walikokuwa wamepangiwa mkutano wa hadhara? Haiwezekani ameponzwa na ubabe na jeuri ya cheo na ukada usio mahali pake?

  Kama alikuwa katika mkutano halali wa kikazi, kama watetezi wake wanavyodai, yeye kama mwakilishi wa rais katika eneo husika, kwanini hakuwa na ulinzi wowote hadi vijana wa CHADEMA walipomwokota na kumpa kibano?

  Kama alivyohoji mtu mmoja jana, kama DC huyo asingewafuata CHADEMA huko walikokuwa, wangemtoa wapi "kumdhalilisha"? Na kama wao wangekuwa wanatendewa haki huko nyuma, na hata katika uchaguzi wenyewe wa Igunga sasa hivi, wangepata wapi hisia na sababu za kuhoji kazi aliyokuwa anafanya kwenye mkutano wa ndani, na hata kumtia mbaroni?

  Bila kujadili uhalali au uharamu wa hatua waliyomchukulia vijana hao, nilipoona picha magazetini, DC akiwa ameshikiliwa kama mwizi, huku akiangua kilio hadharani, na baadhi ya wananchi wakishangilia, kumbukumbu zangu zilinipeleka katika tukio la aina hiyo Januari 5, mwaka huu mkoani Arusha.

  Na baada ya kusikia viongozi makada, wanachama na mashabiki wa CCM wakilalamika kwamba Fatuma amedhalilishwa; na hasa baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kujiapiza jana kwamba "sasa liwalo na liwe, na kitakachotokea wasilaumiwe," nikalazimika kukubaliana na usemi wa wahenga kwamba mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.

  Katika tukio la Arusha, polisi – mbali ya kujeruhi kwa risasi na kuua raia watatu – waliwatendea vibaya baadhi ya washiriki wa maandamano, wakiwamo wabunge na wake za watu.

  Kwa mfano, polisi wa kiume walimpiga ngwara Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya, akadondoka na kudunda kichwa chini kwenye barabara ya lami. Hakuna mwana CCM hata mmoja aliyeguswa na udhalilishaji huo.

  Walimtwanga vitako vya bunduki dereva wa mbunge mwingine, Grace Kiwelu, wakavunja vioo vya gari na kumshambulia tumboni na kifuani.

  Askari wa kiume walimshika vibaya na kumshusha suruali kwa nyuma, Josephine Mushumbusi, mchumba wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa. CCM walishangilia matukio hayo kwa sababu aliyedhalilishwa hakuwa mwenzao!

  Leo polisi Igunga wanahaha kusaka waliomshughulikia DC, lakini hawajamtia mbaroni polisi hata mmoja aliyemdhalilisha Lucy na Josephine miezi minane iliyopita.

  CHADEMA walipolalamikia unyanyaswaji huo, na mengine ya kukamatwa kwa wabunge wao wengine, CCM wakasema huo ni ulalamishi tu.

  Nina hakika, kama DC angekuwa kwenye kazi halali, hata angetaka kuhudhuria mkutano wa hadhara wa CHADEMA, wasingemdhuru. Hata katika uchaguzi mkuu mwaka jana, wenzake kadhaa walifanya hivyo, wakapewa heshima kama viongozi wa serikali.

  DC huyu amepatwa na masaibu haya kwa kuwa alijiingiza katika kampeni za kuibeba CCM; na bahati yake mbaya amenaswa katika mazingira yenye utata, akiwa na makabrasha yanayoonyesha dalili za hujuma za kisiasa dhidi ya wapinzani wa CCM.

  Kwa watu walioonewa kwa muda mrefu, hakukuwa na hatua mbadala isipokuwa kumtia mbaroni na kumwondoa katika eneo husika. Yaliyoambatana na hatua hiyo ni mjadala mwingine ambao utatafutiwa nafasi yake.

  Hoja hapa ni kwamba vijana wa CHADEMA wamepata ushahidi wa kuonyesha kwamba malalamiko yao ya siku nyingi si kulalama tu. CCM inataharuki kwa sababu aliyechukuliwa hatua ni kada wao.

  Jeshi la Polisi linamwaga FFU mjini Igunga, kwa maelezo ya kulinda amani, lakini iwapo vijana watagundua nalo halitendi haki, hiyo amani haitalindika kirahisi – maana lazima wanaolindwa waone haki katika ulinzi huo.

  Uhalifi hauchagui cheo cha mtu. Unaweza kufanywa na DC, polisi au wafuasi wa vyama. Na katika kauli hizi za "tusilaumiane kwa yatakayotokea," ni dhahiri kwamba dalili za amani ya Igunga haziko karibu.

  Lakini haya ni matukio yaliyoasisiwa zamani na watu wale wale waliokuwa wanashangilia matukio ya Arusha, huku wakibeza wanaolalamika.

  Hawakuona ubaya wabunge "kudhalilishwa" lakini sasa wanaona haifai kwa mkuu wa wilaya kudhalilishwa. Nadhani, kama hawakumtuma, wangepaswa kumhoji kabla ya kumtetea.

  Alikuwa anafanya nini katika siasa za wenye vyama vyao, yeye akiwa kiongozi wa serikali inayopaswa kutoa haki kwa vyama vyote?

  Na sisi tunajiuliza, kama Nape ana huruma na anajali utu na heshima wanayostahili waheshimiwa hawa, kwa nini hakujitokeza Januari 5, kuwatetea wabunge waliodhalilishwa na polisi?

  Na hili jeshi la vijana wa CCM wanalotaka kuliondoa kambini na kulimwaga mitaani dhidi ya CHADEMA, huku FFU wakiwa tayari wanarandaranda mitaani; lina hakika kwamba litalinda amani iwapo CHADEMA nao watatunisha misuli kwa nguvu waliyonayo ambayo hatujui mapana yake? Ndiyo amani na utulivu tunaoimbiwa?
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nimeandika allmost the same piece of article nimeitundika ila naona Moda bado wanaifanyia Edit. Makala Nzuri sana
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Haachi nini?
   
 4. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,742
  Trophy Points: 280
  ...hatoacha until maybe (just maybe) uhuru part 2 utakapopatikana!!
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mtu akizungumzia kipigo walichokifanya jeshi la polisi Arusha siku ya tr 5 januari, ananitonesha kidonda ambacho hata kukauka imekuwa ngumu.
  Kuhusu swala la DC nakubaliana kabisa kwamba ni issue ya mkuki kwa nguruwe! Ni ccm tu wanalalamika.
   
 6. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Nadhani Ngurumo amekosea kidogo, kusema kwa nini wabunge wadhalilishwe amekuwa too general!! sio wabunge wote wanaodhalilishwa, bali ni wabunge wa vyama vya upinzani tu na sio wa CCM.
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  asante sana kwa bandiko lako limeenda shule..Nape 'a jeshi lako karibuni
   
 8. bi mkora

  bi mkora JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 262
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa umewamaliza. safi sana.
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  iko siku tutapoza machungu yetu..
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Inaitwa magamba aka ccm mambo yao niyakukurupuka tu
   
 11. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  kwenye katiba mpya jambo la msingi ni kufuta maDC NA MaRC..Kama ni lazima wabaki basi wachaguliwe na wananchi ama waapply kwenye halmashauri na manispaa husika
   
 12. saliel

  saliel Member

  #12
  Sep 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thanx 4 ur commet
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa kuongezea, kwenye toleo la leo (Jumapili 18/09/11) la Tanzania Daima kuna nukuu toka kwa Nape Nnauye akiwatangazia wananchi kupitia vyombo vya habari kuwa CCM wameamua kupeleka vijana wake Igunda ili kulinda viongozi wa ccm. Hawa ni wale vijana waliokuwa wanapata mafunzo 'maalum'. Sijui nini hasa tafsiri ya Nape kuhusu 'kulinda viongozi.

  Kama Nape au mtu yeyote mwenye power toka CCM anasoma hapa jamvini ningetaka kuwakumbusha hatari wanayoikaribisha. Serikali iliyo madarakani ni ya ccm, na kwa siasa/mazingira ya Tanzania mwenyekiti wa chama tawala ndiye huyo Rais wa nchi. Kwa maneno mengine ccm ndio wana jeshi, silaha za kuangamiza binadamu wakati huo huo ni serikali hii ya ccm ina jukumu la kulinda rai wate na mali zao kwa mujibu wa sheria. Sasa kitendo cha chama tawala kinachoongozwa na Rais (kama mwenyekiti) kupeleka vijana kambini kwa ajili ya kitu kinachoitwa 'kulinda' viongozi nje wa mfumo unaokubalika kikatiba ni hatari kubwa sana. Wanawalindaje viongozi? Na kwa nini wapekeleke vijana kambini wakati wa chaguzi?Kazi ya polisi ni nini? Hawa vijana wana tofauti gani na Janjaweed wa Sudan? Na ccm hawawezi kuja na visingizio kuwa vyama vingine navyo vina vijana. Hatakubalika kwani ccm/serikali kazi yake ni kuzuia huu utawala 'binafsi. Hivyo kwa 'vyama vingine' kuwa na utawala binafsi ni ishara kuwa serikali inatelekeza majukumu yake na ndio watu wanatafuta utaratibu wa kujihami.

  Ikitokea leo hii hawa vijana wa ccm wakasababisha machafuko kama yale ya Kenya (Mungu apitishe mbali) Nape Nnauye atakuwa mshitikiwa namba moja kwenye mahakama ya kimataifa kule Hague. Kwa hali ilivyo sasa Nape hana namna ya kujinasua maana tayari kesha-kaririwa na vyombo vya habari akitangaza kuanza kwa kutumika kwa MALITIA waliopata mafunzo (He is on record). Anachotakiwa kufanya Nape ni kuomba mungu usiku na mchana ili hao vijana wasilete machafuko maana hawezi kukwepa. Sijui kwa nini watu hawajifunzi? Kenya sasa hivi wapo kwenye saga ya Ocampo 6, Kibaki na Odinga wako mtaani, hivyo Nape asifikiri kuwa anaweza kuja na porojo za 'nilikuwa natekeleza maagizo'. Sijui nani anawashauri hawa ccm, sijui. Ila huu ni ujinga wa viwango vya juu.
   
 14. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tena huyo ilitakiwa atandikwe kama mwizi vile, bado alitoka salama wanalaumu? kunya anye kuku akinya bata kaharisha. Kwanza jina lenyewe tu halina hadhi ya kuwa mkuu wa wilaya anaonaekana ni waswahili walewale. kweli nchi yetu imeuzwa kwa hawa waswahili watz tutajuta sana kwa uongozi huu kuliko wakati mwingine wowote. Bora hata CCM ya Mkapa.
   
 15. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #15
  Sep 18, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mbinu za kuhadaa wapiga kura na za kuiba kura za CCM sio ngeni katika nga za siasa za Tz. Kuwatumia viongozi wa serikali, polisi na wanajeshi bila kusahau tume ya uchaguzi ni jambo lililozoeleka. Sijui ni nani waliasisi mbinu hizi lakini kwa sasa zinaonekana kuanza kupitwa na wakati na kuzidiwa na wapinzani.

  Plan B inayoasisiwa na akina Nape ndiyo hiyo ya 'kuzipa nguvu' mbinu hizi chafu, kama kuamua kuwalinda viongozi wakati wanapofanya kazi ya kuibeba CCM. Sijui kina Nape wamewazaje, lakini kwa haraka haraka naweza kusema hii imeshindwa kabla haijaanza, tena imeshindwa vibaya. they have to do their blood homework again...
   
 16. C

  Concrete JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  @Kuna haja ya Vyombo vya dola kumkamata na kumuhoji Nape Nnauye, kwa hii kauli yake ya kusema; "Sasa CCM imeamua kutumia vijana wake waliokuwa kambini wakipata mafunzo maalum kwenda kuwalinda viongozi wao, na liwalo na liwe,wasije wakalaumiwa kwa lolote." Inabidi kila mpenda amani ailaani kauli hii maana inaashiria shari kubwa kwa watanzania wapenda amani. @Naamini hata baadhi ya wanaCCM wapenda amani hawawezi kuunga mkono kauli hii ya Nape. Na sasa nimeamini bora Yusuph Makamba kuliko Nape Mnauye!
   
 17. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Namchukia Nape kuliko kinyesi
   
 18. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  CCM ccm tutawashtaki mbele ya HAKI, asanteni kwa kuivuruga amani ya Igunga na Tanzania kwa ajili ya kulinda maslahi yenu!
   
 19. T

  Topical JF-Expert Member

  #19
  Sep 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Habari ya kishabiki zaidi..inafaa sana ingeandikwa na John Mnyika (public relation officer wa Chademu..lakini kuandikwa na mwandishi wa gazeti linalojibaragua kuwa huru..ni upotofu mtupu

  Amendika matope ya ushabiki
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Sep 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ukimpiga mtu yeyote ili upate haki na wewe utapigwa ili ujifunze...kuwa kupiga si namna sahihi ya kupata haki

  Utaratibu wetu wa kutafuta haki tuliojiwekea usipofuatwa na kusimamiwa tutakuwa taifa la wapumbavu..

  Chademu acheni jazba na bange kupiga wanawake ebo!
   
Loading...