Ansbert Ngurumo: Roma 1,300, CCM 50 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ansbert Ngurumo: Roma 1,300, CCM 50

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUMBIRI, Jan 22, 2012.

 1. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Roma 1,300, CCM 50

  Na Ansbert Ngurumo,


  MWISHONI mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu, nimekutana na makundi mbalimbali ya watu waliokuwa wanajadili "mwisho wa CCM."

  Baadhi yao ni wana CCM wakongwe; wengine ni waasisi wa chama hicho. Wanajadili kifo cha chama chao kwa hoja za kihistoria.
  Wanasema kitakachoiangusha CCM ni serikali yake, na kitakachoiangusha serikali ni CCM hii.

  Kwao, kwa kuzingatia mfumo wa sasa ulivyo, udhaifu wa serikali iliyopo unatokana na udhaifu wa CCM.
  Si hilo tu. Miongoni mwao, wamo waliosema kuwa udhaifu wa CCM unatokana na uwezo mdogo wa serikali kufanya kazi na kutimiza wajibu wake.

  Ni wazi, viongozi wa CCM ndio hao hao wanaoongoza serikali. Waliotoa ahadi wakati wa uchaguzi, ndio hao wanaoshindwa kuzitekeleza leo wakiwa serikalini.

  Walioahidi umoja na mshikamano wa kitaifa, ndio hao wanaoshindwa kuleta umoja na mshikamano katika chama chao.
  Viongozi waliotuahidi maisha bora ndio hao wanaoshindwa kudhibiti mfumuko wa bei za bidhaa na huduma; ndio hao wanaoshindwa kudhibiti au kuondoa pengo linaozidi kuongezeka kati ya maskini wengi na matajiri wachache.

  Viongozi hao wanaokusanya kodi kubwa kila mwezi ndio wanaoshindwa kueleza chanzo cha ukata unaoikabili serikali, kiasi cha kutishia uwezo wa serikali kutimiza wajibu wake. Wale wale walioahidi wenzao kwamba wanajivua magamba ili wawe wapya na safi, ndio hao wanavaa magamba mapya na magumu kuliko ya awali.

  Historia imetufunza kwamba ukiona ufamle wowote unaishiwa pesa, ujue kuwa ufalme huo unakaribia kuanguka. Tunajua kuwa kupanda kwa gharama za maisha hakuwezi kuongeza mapenzi ya wananchi kwa watawala. Na katika mazingira ambamo huoni watawala wakiwa na mbinu mbadala za kuwakwamua wananchi wao dhidi ya ongezeko la bei kali za bidhaa na huduma, kinachoonekana pale ni dalili za anguko la ufalme huo. Hata maandiko matakatifu yanasema kwamba watawala wanaogawanyika katika makundi hasimu, hawawezi kupanga na kutenda kwa umoja. Hawawezi kumshinda yeyote anayeshindana nao; wataparaganyika na kuanguka.

  Serikali inayolipisha wananchi maskini kodi kubwa sana kwa wananchi maskini, huku ikiwaacha matajiri wachache kukwepa kodi na kutajirika kwa kasi, ni serikali inayoelekea kuanguka. Serikali inayovumilia rushwa na uonevu dhidi ya wanyonge, ni serikali inayochochea hasira za wananchi dhidi yake, na inakaribisha anguko lake.

  Hata Himaya Kongwe ya Roma, ambayo ilidumu kwa miaka ipatayo 1,300 – ilianguka kwa sababu iliishiwa pesa, kodi zilipanda sana, serikali ilishindwa kutekeleza majukumu yake, ufisadi uliongezeka na kukithiri, ukali wa maisha uliongezeka, matajiri walineemeka na umaskini uliongezeka, na haikuwa na pesa za kutosha kulipa masilahi ya wanajeshi.

  Dalili zile zile zinajionyesha kwa watawala wakongwe wa CCM, ambao kwa sababu ya ukata, wamelazimika kukopa mabilioni ya shilingi benki, ili kugharamia sherehe za miaka 50 ya "Uhuru." Tunaambiwa hadi leo serikali inakosa pesa za kufanyia kazi za maendeleo kwa sababu sehemu kubwa ya makusanyo inayopata yanaelekezwa katika kulipa deni hilo! Ndiyo maana serikali inakabiliwa na ukata, inachelewesha mishahara ya watumishi, inapunguza nafasi za ajira mpya, na inakata mafungu ya posho za uendeshaji wa shughuli za wizara na idara zake.

  Ndiyo maana wakubwa ndani ya CCM wanaogopa kuingia katika uchaguzi wowote mdogo baada ya Igunga, na sasa wanatafakari jinsi ya kubadili vifungu vya sheria ili kukiepusha chama chao na fedheha ya uchaguzi mdogo. Maana wanajua kuwa bila pesa hawawezi kulangua kura! Kwa kuwa hawako tayari kushindwa kwa kura, wanaona bora wasishindane kabisa. Na kwa wingi wao bungeni, wakiamua kubadilisha sheria yoyote watafanya hivyo, ilimradi inalinda masilahi yao. Serikali inaposhindwa kutekeleza ahadi zilizotolewa na wagombea wa CCM, inakihakikishiaje chama hicho kubaki madarakani kwa muda mrefu ujao?

  Serikali inayowanyonya wanyonge, inajihakikishiaje kuwa itakuwa kimbilio la wanaonyonywa na kunyanyaswa? Serikali inayokosa mvuto kwa vijana, ambao kwa takwimu zisizo rasmi ndio asilimia 40 ya Watanzania wa leo, inawekeza katika kizazi kipi kitakachokifanya chama tawala kiendelee kushika madaraka kwa muda mrefu ujao? Kwa msingi huu, wanaojadili mwisho wa CCM hawajakosea. Na wakubwa wenyewe wanajua.

  Ndiyo maana tunaona wakihaha na kujitapa kufanya mabadiliko makubwa katika uchaguzi ndani ya CCM mwaka huu, huku wakijitapa kutosana na kukomoana kuelekea 2015. Hizi ndizo dalili za anguko linalozungumzwa na wakongwe hao ninaowazungumzia.

  Kama wasemavyo wanahistoria, falme zote huwa zinaporomoka pole pole – hazianguki ghafla. Tumezoea usemi wa Kiingereza kwamba Roma haikujengwa kwa siku moja. Lakini pia haikuanguka kwa siku moja. Iliporomoka pole pole! Ikumbukwe kwamba Himaya ya Roma ‘ilikataa' kuwalipa vizuri wanajeshi wake; huku ikiendelea kuwategemea katika kazi nzito za ulinzi.

  Ndio hao ambao hawakuweza kuinusuru serikali hasira za umma zilipoamka; maana umma mzima uligeuka jeshi kubwa dhidi ya dola.
  Ukweli huu kuhusu Roma unaihusu CCM pia. Kwa ukali huu wa maisha, ukata na kushindwa kwa serikali, inatengeneza jeshi kubwa dhidi ya watawala. Kilichoitokea Roma katika miaka 1,300 ndicho ninachokiona ndani ya miaka 50 ya CCM. Je, huko tunakoelekea yupo anayeweza kuinusuru?

  Source:
  http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=32189
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kaandika kwa hisia zake af anasingizia kuwa ni watu wa ccm.yeye anapandikiza chuki zake kwa jamii baada ya kukosa ile nafasi ya mkugenzi wa habari ikulu kama alivotarajia.Ansbert Ngurumo ukimfahamu wala hakupi shida.
   
 3. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  As usual, unataka tum-discuss mtu (Ansbert Ngurumo) badala ya hoja (Kuanguka kwa CCM). And you also want to be called a GREAT THINKER... Think twice.
   
 4. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  MtamaMchungu umemjibu vema kabisa huyo anayejiita hojatete wakati hana cha hoja wala nini, again I repeat or paraphrase 'hapa tujadili hoja na siyo mtu au mleta hoja' tujadili content na maudhui

  Alich√łongea ngurumo hakika ndo ukweli wenyewe na hajakosea chochote, utawala huu wa kinyonyaji utak√∂ma siku moja na wala si mbali sana
   
 5. k

  kuzou JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo ccm na serikali zitakufa kwa sababu hazina hela? mwandishi kilaza jina linamlinda
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tekibir
   
 7. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Nimeipenda hii: "kitakachoiangusha CCM ni serikali yake, na kitakachoiangusha serikali ni CCM hii."

  Haya ni maneno mazito yaliyosheheni ukweli. Haijalishi yamesemwa na Ngurumo au kichaa fulani hivi kama Hojatete. Yanabaki na mshindo ule ule. Wenye hekima walionya sana kutenganisha majukumu ya serikali na chama wakazomewa. Matokeo yake ni kuwa kiongozi wa CCM akiwa fisadi, CCM yote inaitwa ya kifisadi


  na serikali yote pia.
   
 8. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  uelewa wako mdogo unakufanya ushindwe kujenga hoja na kuja na utetezi dhaifu kama huu. Uwe unasoma bandiko kwa makini ndio utoe mchango wako we nyang'au!
   
 9. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,891
  Likes Received: 1,649
  Trophy Points: 280
  ok. Lakin kwel anasema au?
   
 10. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,891
  Likes Received: 1,649
  Trophy Points: 280
  asante! Hiyo pin imemfikia kikwete ikulu! Yote ni kweli.
   
 11. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Sometimes natamani JF kungekuwa na entry exams. Tungepunguza taka taka kama hizi ulizoandika hapa.
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kitu pekee nimegundua unaweza kutueleza maendeleo ya msiba wa Mbunge wa CCM mbali na hapo wewe ni kama Nape .Jaribu kujibu hoja mara zote acha kumshambulia Ngurumo ni machine kubwa .Kichwa kile na kamwe huwezi kugusa .Kile kichwa cha Kipapalapa Seminary mkuu si madrasa.Kama huamini muulize Salva anavyo hangaika na Ngurumo kuanzia akiwa UK hata sasa .
   
 13. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Inabidi kuwa zezeta kwanza ndipo uitetee CCM na serikali yake ya sasa!
   
 14. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hata mwehu hawezi kutetea
  ccm, ni serikali iliyooza.
   
 15. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,861
  Likes Received: 2,786
  Trophy Points: 280
  Asilimia kubwa ya wa-TZ ni wavivu wa kufikri! Unataka tuanze kumjadili AN badala ya kujadili hoja aliyoileta? Ukweli ndo huo magamba hawatakwepa anguko linalowanyemelea!
   
 16. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha! Yani magamba utayajua 2 koz hata aibu hayaoni kwani yanaogopa CDM kuliko hata mungu. Shame on u all magambas! Nd BRAVO CHADEMA.
   
 17. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Huna aibu kutaka kumjadili mtu badala ya mada? Shame on you. Kuna mtu amependekeza entry exam humu na kama ingekuwepo usingetia mguu humu. Viva mada ya Ngurumo
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ukweli unauma sana tu, mwandishi ameandika habari inayoakisi mioyo ya watu, habari inapenya kama mshale ndani ya mioyo yetu, wenye kuumia wanaumia na wenye kufurahia nafasi ya anguko wanasababu.

  Ukiwa mwelewa wa kusoma mienendo ya historia hutachelewa kumwelewa mwandishi, ni kama wataalamu wa hali ya hewa wanavyotumia kudadafula kumbukumbu za matukio yaliyopita kuainisha na kuhusisha kwa yanayojilia kwa vile dunia ni mzunguko na yaliyojilia miaka kadhaa yatajirudia na hakuna kisicho na mwisho katika viumbe ndani ya tufe hili kwani tulipozaliwa tumeikuta na tutaiacha.

  Tunazaliwa dhaifu, tunapata nguvu, tunayamudu maisha, tunachoka, tunaishiwa nguvu, tunakufa na wapya wanaibuka kwa utaratibu huo huo, lakini dunia ni ile ile inabaki na mzunguko wake kuzuru jua lakini kamwe haifikii jua na kubaki kwenye orbit yake kutokana na mfumo wa maumbile ya nguvu ya mvutano wa asili.

  Wagombanapo mafahani wawili huwasahaulisha kinachowagombanisha huku hasira zimewajaa na muda unavyozididi ndivyo wanavyozidi kupandishana hasira na uwanja wa mapambano kuwa tifutifu. Mafahari wadogo wanatumia mwanya huo kutamalaki hazina wanazogombaniana hawa madume wakuu. Watakapositisha ugonvi walichogombaniana si chao tena maana mafahari wadogo wameshatamalaki. Tatizo la mapambano huwa hakuna nafasi ya kufikiria wanacho gombaniana,
  kadiri muda unavyozidi kuyoyoma ndivyo dhana ya kuonyeshana ubabe nani zaidi inavyozidi kupamba moyo.

  "HISTORIA NI MWALIMU"
   
 19. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #19
  Jan 22, 2012
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  "Argumentum ad hominen" is a problem to most contributors, .... needless to say Ndugai type! Always discuss topic facts and not the person who raised the idea.
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  CCM imezaliwa mwaka 1977. Hivi sasa ina miaka 35. Mwandishi anaueleza umma kuwa CCM bado itakuwa na nguvu kwa miaka mingine 15 mpaka itakapotimiza miaka 50. Si haba...
   
Loading...