- Mkuu Pasco, mbona swali linaeleweka sana kwamba vipi jinsi hiyo mihimili inavyofanya kazi katika taifa letu? Ya integrity na IQ ni vitu viwili tofauti sana naona vinakuchanganya mkuu, maaana yake sio moja na haina anything to do na mihimili minne uliyoisema inatumika na taifa letu,
- sasa ndio maana nikakuomba wewe mwenye IQ kubwa kama ambavyo umekua ukidai,
- I mean ya IQ na Integrity hilo wala sina tatizo nalo kwa sababu records zetu hapa ziko wazi nani ni nani!
Asante FMEs,
Naanza na angalizo, sio kweli kuwa mimi nimekuwa nikidai nina IQ kubwa, kuna issues huwa zinabishaniwa humu ndani, that just needs an avarage IQ kuzielewa, zinakuwa hazieleweki kwa baadhi yetu na sometimes, they are blown beyond proportions for nothing, ndiyo hiyo inayopelekea baadhi yetu kuanza kuquestion uwezo wa uelewa wa baadhi yetu. Huu uelewa ndio IQ yenyewe ninayoizungumzia.
Let me be very honest, I don't belong kwa wenye I.Q kubwa ndio maana I can afford to spend time kujibu haya, wenye I.Q kubwa wamejinyamazia maana wakijibishana na type yetu, watazidi kutuchanganya kama sio kutupoteza kabisa, kama issues ndogo tuu kama hizi zinasumbua, kubwa si zitatupasua vichwa kabisa!.
- Again nitashukuru sana kama utaiweka vizuri hapa tukala elimu jinsi hiyo mihimili inavyofanya kazi Tanzania, maana mimi binafsi sijawahi ku-experience that huwa naona Rais ana nguvu ya kufanya analotaka bila kujali mhimili wowote, tuelimishane jinsi hii mihimili inavyofanya kazi, is it too mucha to ask mkuu? au?
Respect.
FMEs!
.
Mihimili 3 ya Dola ambayo inatakiwa kufanya kazi kwa uhuru na wakati huo huo kuweka mipaka mihimili mingine isivuke mipaka, checks and balance ni Bunge, Serikali na Mahakama. Bunge linatunga sheria, Mahakama Inazitafsiri hizo sheria na serikali inasimamia utekelezwa wa hizo sheria kwa mujibu wa katiba.
Vyombo vyote hivi vitatu, vinawekwa na sheria mama ambayo ni katiba au mkataba wa watawala na watawaliwa.
Bunge likitunga sheria ambayo siyo ama inayokwenda kinyume cha katiba, mahakama, inaifutilia mbali. Serikali nayo ikitenda ndivyo sivyo, inapelekwa mahakamani na inaadhibiwa. Serikali hairuhusiwi kuingilia utendaji wa bunge wala mahakama. Bunge linaisimamia serikali kwa kuishauri na sio kuamuru.
Rais wetu ndiye mkuu wa serikali, wakati huo huo ni sehemu ya Bunge, akiwa na nguvu za kulivunja bunge at his pleasure, na kila sheria inayotungwa, lazima iidhinishwe na rais ili iwe sheria, hakuna time frame lazima awe amesaini by lini, hivyo anaweza kuikalia atakavyo.
Rais wetu pia ni sehemu ya mahakama kwa kuteua kuanzia Jaji Mkuu na majaji lakini hana uwezo wa kuwafuta kazi. Capital punishment haitekelezwi bila rais kusaini, ndio maana kuna watu walihukumiwa kifo miaka ya 60, adhabu zao hazikutekelezwa mpaka walipojifia wenyewe.
Kutokana na mfumo huu, the principle of separation of powers iko njia panda.
Bunge ndilo lililotakiwa kuisimamia serikali yetu, ili spika awe na nguvu ya kweli, alitakiwa awe total independent, spika wetu ni mjumbe wa NEC na pia alipotaka benzi 500 S-Class new model ya 2009, sambamba na nyumba ya hadhi inayomstahiki Sitta, alipiga magoti kwa JK kuomba aidhinishe, na JK kwa kujua nguvu ya spika ndani ya bunge, akasema mpeni kila anachotaka. Leo Spika ana guts za kuliongoza bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali?!, wote wamwage unga na kukosa ulaji ilhali ni wachumia tumbo?.
Mawaziri ambao ni wabunge, walitakiwa wawe wawakilishi wa wananchi kuiwajibisha serikali bungeni, leo wao ndio waserikali, wameukwaa ulaji watajiwajibisha vipi?. Ndio maana nimesisitiza tangu mwanzo msimama wa Mama Super K kuwa mawaziri wasiwe wabunge ili wawajibike kwa bunge. Wapendekezwe na rais na kuidhinishwa na bunge, wakishindwa kazi, bunge linawapiga chini. Tofauti na mama ni hili tuu la mawaziri kuchaguliwa kama rais. Bado mpaka sasa nampa benefit of doubt kuwa amekuwa mis quoted.
Huu mfumo tumeukumbatia toka kwa Muingereza, ni mfumo wa kikoloni ambao sisi tunaukumbatia na kujikolonise wenyewe. Lengo la mfumo huu ni kiinimacho cha separation of powers wakati infact tuna rais mwenye dictatorial powers akiamua kuzitumia to the fullest, anakuwa yeye rais, mkewe waziri mkuu, shemeji spika, mjomba jaji mkuu, shangazi mkuu wa polisi, kaka mkuu wa majeshi, wakuu wa taasisi zote za umma aweke kabila lake, washikaji wake wote awape ukuu wa mikoa na ukuu wa wilaya zote aweke vimada wake, katiba haikuspecify criteria ya presidential apointees, na hata akifanya hivyo ndio kwa mujibu wa katiba.
Mimi naungana na wanaharakati katika kilio cha kutaka katiba mpya itakayoweka level playing ground tupate ushindani wa haki vinginevyo mwenye mpini atatawala milele!.