FMES,
..mimi nimeelewa kuwa Mama K anapendekeza kuwe na wagombea Uwaziri ambao watazunguka nchi nzima kama ambavyo mgombea Uraisi wa Jamhuri hufanya na baadaye kupigiwa kura na wananchi.
..mfumo wa Marekani nauelewa, ndiyo maana nikasema kwamba alichoelekeza mama Kilango sicho kinachofanyika Marekani. na pia ndiyo sababu nikatilia mashaka kuhusu uwajibishwaji wa mawaziri hao waliochaguliwa moja kwa moja na wananchi kama Raisi wa Jamhuri.
..Mapendekezo yangu ni tofauti na Mama K, lakini yanafanana zaidi ya jinsi Wamarekani wanavyoteua mawaziri wao. binafsi napendekeza Waziri asiwe Mbunge wa kuchaguliwa. pia napendekeza ateuliwe na Raisi, lakini uteuzi wake uidhinishwe kwa kura za wabunge.
..mama K anapendekeza mawaziri wapigiwe kura moja kwa moja na "wananchi", siyo na "wabunge."
..zaidi napendekeza kiwekwe kipengele kitakachozuia Mawaziri wasigombee Ubunge kwa miaka 5 baada ya kuacha nafasi zao za uwaziri. Wabunge nao wasiteuliwe kuwa mawaziri kwa kipindi cha miaka 5 baada ya kuacha nafasi ya ubunge.
..pia napendekeza mawaziri wasiwe na chama kama ilivyo kwa watumishi wa ngazi za juu wa serikali. hiyo itawasaidia wabunge wasipige kura kwa kusukumwa na mapenzi au ushabiki wa chama anachotoka waziri.
NB:
..mama K angesema tufuate mfumo wa "KIMAREKANI" na kuishia hapo tungemuelewa anachopendekeza. lakini yeye amekwenda mbali na kufafanua huo "mfumo wa Kimarekani" anaopendekeza bila kumtaja RAISI kama mamlaka inayopendekeza jina la waziri, au BUNGE kama mamlaka inayopiga kura kuridhia uteuzi huo.