Anne Kilango ataka mawaziri wachaguliwe na wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anne Kilango ataka mawaziri wachaguliwe na wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MaxShimba, Jan 13, 2010.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  MBUNGE wa Same Mashariki, ameponda mfumo wa kuwapata mawaziri na kupendekeza kuwa wachaguliwe na wananchi kama ilivyo kwa rais.

  Soma habari kamili hapa:

  MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ameponda mfumo wa kuwapata mawaziri na kupendekeza kuwa wachaguliwe na wananchi kama ilivyo kwa rais.

  Wakati Kilango akisema hayo kwenye uzinduzi wa ripoti ya kujipima kwa kutumia vigezo vya utawala, mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa amesema nchi itavurugika kutokana na muswada wa sheria ya udhibiti wa fedha za uchaguzi unaoandaliwa kuwasilishwa kwenye mkutano ujao wa Bunge.

  Kauli ya Kilango inatokana na ripoti hiyo ya Mfumo wa Kupima Utawala Bora wa Umoja wa Afrika (APRM) kutaja kwamba mchanganyiko kati ya Bunge na serikali unakinzana na kanuni.

  Ripoti hiyo iliyozinduliwa juzi na Naibu Spika Anna Makinda katika hafla iliyohudhuriwa na wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge jijini Dar es salaam, imeeleza mafanikio, mapungufu na mpangokazi wa kuyaondoa mapungufu hayo.

  Tathimini ya ripoti hiyo iliyofanywa kuanzia mwaka 2007 hadi 2009 imesema: "Mchanganyiko kati ya mhimili wa Bunge na Serikali unakinzana na kanuni zinazotaka mamlaka hizi zitenganishwe kuhakikisha wabunge hawawi sehemu ya utawala, kwa maana kuwa wabunge wasiwe mawaziri wala wakuu wa mikoa."

  Akizungumza mara baada ya kuwasilishwa kwa ripoti hiyo, Kilango alifafanua kwamba mfumo wa sasa wa upatikanaji wa mawaziri haukidhi haja na tija ya Watanzania kwa kuwa unatofautiana na ule wa kumpata rais.

  "Tuukatae mfumo wa upatikanaji wa mawaziri ambao ni wa Commonwealth (Jumuiya ya Madola) kwa kuwa hauendani na ule wa kumpata Rais," alisema Kilango.

  Kilango, ambaye ni mbunge wa jimbo la Same Mashariki, alifafanua kwamba mfumo wa kumpata rais nchini ni wa Kimarekani ambao rais anachaguliwa moja kwa moja na wananchi tofauti na mawaziri ambao huteuliwa na rais baada ya kuwa wabunge.

  "Ni muhimu sasa kwa mawaziri nao wakachaguliwa moja kwa moja kutoka kwa wananchi, kwa kuwa mfumo wa kisasa wa utawala unaonekana kuegemea na kufuata mfumo wa Kimarekani ambao mawaziri huchaguliwa moja kwa moja na wananchi hivyo ni wakati muafaka mfumo huo ukatumika kuwapata mawaziri nchini," alisema Kilango.

  Naye Makinda alisema mifumo yote miwili ni mizuri na ina faida na hasara zake.

  "Kikubwa itabidi tuangalie na tujadili kwa kina ni mfumo upi una faida na tija zaidi kwa Watanzania, lakini mifumo hii inatofautiana kwa kuwa mfumo mmoja unamruhusu waziri kuwepo bungeni moja kwa moja na mwingine unamtaka aingie bungeni wakati kunapokuwepo suala au hoja inayohusu wizara yake," alisema Makinda.

  Mbali na suala hilo, ripoti hiyo inayohusu utawala bora imeeleza kwamba kuwepo kwa mapungufu ya kutojulikana mahali fedha za kugharamia uchaguzi zinakotoka kunahatarisha uwepo wa ushindani katika uchaguzi.

  Hivyo imependekeza kutungwa kwa sheria za kusimamia fedha zinazotumiwa katika chaguzi mbalimbali pamoja na kutoa elimu ya uraia na elimu ya wapiga kura ili kuondoa rushwa katika uchaguzi.

  Akichangia hoja hiyo, mbunge wa Ukerewe, Dk Getrude Mongela alisema rushwa ya kisiasa ni hatari na inaweza kuchochea vita.

  "Watu wanajua kwamba rushwa ipo na wanaiona lakini hawaikemei. Na ningependa nisema kuwa rushwa ya kisiasa ni hatari, italeta mfarakano wa kitaifa," alisema Dk Mongela.

  Akizungumza na Mwananchi kuhusu hoja hiyo, katibu mkuu wa Chadema, Dk Slaa alisema kupitishwa kwa sheria ya kuweka wazi watu wanaochangia vyma vya siasa pamoja na kiasi, itasababisha vurugu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.

  "Mantiki ya sheria hii ni nzuri katika ulinzi na usalama wa taifa, lakini dhumuni la kutungwa sasa kwa sheria hii ni tofauti na kuna mashaka makubwa hivyo uchaguzi utavurugika zaidi," alisema Dk Slaa.

  Dk Slaa alifafanua kwamba kuvurugika huko kutatokana na utofauti mkubwa wa uwiano wa vyanzo vya mapato baina ya vyama vya siasa.

  Alisema kutokana na hilo vyama, hasa vya upinzani ambavyo kwa kiasi kikubwa vinategemea michango ya wanachama wao wenye uwezo mdogo wa kipato, vitakuwa katika wakati mgumu.

  "Ukweli ni kuwa CCM ina vyanzo vingi vya mapato na hasa kutokana na kuwa na matajiri wengi na wakubwa tofauti na vyama vya upinzani, hivyo kutakuwa na wakati mgumu katika uchaguzi huo,"alisema Dk Slaa.

  Katika hatua nyingine ripoti hiyo imeeleza kuwa kutotekelezwa kwa uamuzi wa kuruhusu mgombea binafsi, kunanyima haki ya msingi ya mtu kuchaguliwa.

  "Ili kuweka hali hiyo sawa ni muhimu kupitiwa upya kwa sheria za uchaguzi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na ya Zanzibar," imesema sehemu ya ripoti hiyo.

  Tayari serikali imetangaza nia ya kwenda mahakamani kupinga suala la kuwepo kwa mgombea binafsi nchini baada ya Mahakama Kuu kubatilisha sheria inayokataza mgombea binafsi kwa kuwa inakiuka katiba ya nchi.

  Akizungumza na Mwananchi kuhusu mgombe binafsi, Makinda alisema; "Tusubiri muda utafika na kila kitu kitakuwa sawa."

  Katika hatua nyingine, ripoti hiyo imeeleza kwamba kamisheni za uchaguzi, Tanzania Bara (Nec) na upande wa Zanzibar (Zec), hazina uhuru wa kutosha na pia kuna ufinyu wa kupata haki za kisheria nchini.


  CHANZO: MWANANCHI
   
 2. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sijui kwanini amependekeza hivyo. Labda mtoa hoja ungeelezea zaidi, ingesaidia sana.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Jan 13, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Si wanachaguliwa kuwa wabunge na wananchi kisha wanateuliwa na Rais kuwa Mawaziri? Na kama wakichaguliwa na wananchi moja kwa moja Rais hatakuwa na mamlaka ya kuwawajibisha! Hii kitu haitakuwa sawa, mama Kilango amechemsha!
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,556
  Likes Received: 18,268
  Trophy Points: 280
  Huyu ni mama yetu, she is genuine na ni mwanamke wa shoka, ila kwa hili, amechemsha.

  Naungana na vision yake wasichaguliwe na rais, ila pia sio wananchi. Mfumo safi ni wa US, mawaziri sio wabunge, na wanapendekezwa na rais na kuwa vetted na bunge.

  Huu mfumo wetu wa mawaziri wabunge unakwenda contrary to the principles of separation of powers.

  Vyombo vitatu vya Excecutive, Legistlature na Judiciary lazima viwe independent for checks and balance.

  Mbunge aliyeteuliwa waziri anaweza vipi kuiwajibisha serikali? Sanasana ni kujipa upendeleo wa maendeleo kwenye majimbo yao hali iliyopelekea wabunge kuwajia juu mawaziri.
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Jan 13, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  ..mawaziri wa Marekani wanateuliwa na Raisi, na baada ya hapo Bunge[Senate] huwahoji na baadaye kuridhia au kukataa uteuzi huo.

  ..I hope mwandishi amemnukuu vibaya Mama Kilango. vingenevyo nitapenda kupata ufafanuzi zaidi wa jinsi huo mfumo anaopendekeza utakavyofanya kazi.
   
 6. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Watanzia Tunahitaji mawaziri ambao ni wataalamu na wawe sio wabunge wa majimbo ila wataingia bungeni kwa kofia ya uwaziri tu.
  Wachaguliwe na rais na wakapige kura na wabunge hiyo nayo ni nzuri sana.
   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mimi napingana na Mama Kilango kuwa Mawaziri wachaguliwe na wananchi kuna hoja nyingine itakuja how? kama ni kwa kura kama za ubunge hiyo itaturudisha kule kule kwenye mambo ya kisiasa. Naungana naye kuwa wasiteuliwe na rais ila rais awapendekeze tu apeleke sifa zao bungeni zichujwe then waidhinishwe na bunge, kwa maana hiyo mbali ya mawaziri kuwajibika kwa rais wawe answerable pia kwa bunge.
   
 8. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mawaziri wasiwe wabunge itakuwa sawa na haki

  Mawaziri wawe vetted na bunge itakuwa kama wameridhiwa na wananchi kupitia bunge la wananchi

  Ifike mahali all presidential appointment iwe vetted na bunge ili kupata ridhaa ya kuhudumia wananchi na siyo chama au rais.
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Jan 13, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  ..labda itasaidia tukiwa na habari kamili kama ilivyoandikwa na gazeti la Mwananchi.   
 10. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mimi nigeona ni vema kama mama Kilango angeshauri kwamba mameya wa miji na madiwani wote wachaguliwe na wananchi.

  Baada ya ya hapo mabaraza ya madiwani yote yataweza kuwa na nafasi (kwa wakti wao) kutafuta "management" za kuendesha manispaa zao.

  Mifumo hii ya uendeshaji wa nchi kwenye ngazi za manispaa ndio inayoleta maendeleo kwa kila mwananchi na sio porojoporojo za kila siku.
   
 11. m

  mzawahalisi JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Hivi kwani nilazima kuiga kila kitu kutoka kwa mabwana hawa wakuu ie common wealth n USA? Mfana "ninge tawala", uwaziri ningeitangaza kama nafasi ya kazi na kutoa vigezo mf: utaaluma wa wizara unayoomba, proven leadership skills, na proposal ya angalau mwaka mmoja wa mkakati wa wizara anayoomba, plan hiyo ilenge kufanikisha sera zangu, kwa kutumia budget ya mwaka uliopita! Kisha usalama watapitia kwa kina taarifa za waombaji, screening ya nguvu, kisha pres'da, makamo 2 na Pm tuna wachuja na kuwapeleka bungeni kwa kuwapitisha. Wange wajibika ipasavyo.
   
 12. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #12
  Jan 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwa mawazo yangu.
  mfumo wa kupata mawaziri kutoka kwenye makundi ya wabunge naamini ni mtindo wa hovyo unaoshawishi rushwa na ulaji kwenye chaguzi maana kwa kila mbunge anatamani siku moja awe waziri hata kwa gharama ya kuroga Bagamoyo ama Sumbawanga. hii imetuletea viongozi wa hovyo sana.
  wabunge kuwa mawaziri imewafanya baadhi ya wanannchi kuukosa uwakilishi wa moja kwa moja wa mbunge wao katika shughuli za bunge...hapa protocal na maadili huzingatiwa.
  uwaziri mara kadhaa imetumika kama dawa ya wabunge wapiga kelele na wapenda mabadiliko. ukiwa msemaji sana bungeni unazawadiwa uwaziri kisha mdomo unafungwa rasmi.
  naamini kama rais wa Jamuhuri angekua makini angeweza kutupatia mawaziri kumi boa kabisa kutoka kada za watendaji katika nyanja mbalimbali, fikiria raisi ana nafasi kumi za kuteua wabunge, nilitaraji hapa ndipo pangekua mahala pekee pakutuletea watu timamu katika kusukuma gurudumu la maendeleo la nnchi yetu, kinyume chake anamteua Kingunge kua mmbunge kisha waziri, jamani kuna umakini hapo, akamteua Kwaygir kwey....kuwa mmbunge, huyu ni yule mama mlemavu wa ngozi ambae mara kadhaa taasisi za wenye ulemavui zimekua zikilaani uteuzi wake haukua makini na si muwakilishi halisi wamakundi la wenye ulemavu, uteuzi ukaendelea, akateuliwa Mwang'onda Thomas ili kulipa fadhila za babae ambae inadaiwa alimsaidia sana JK kufika hapo...mambo ni mengi kifupi tunahitaji kuufumua huu utaratibu kwa kubadili katiba yetu.
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0

  - Mkulu sana Pasco, huko US mawaziri hupendekezwa na Rais, halafu kukubaliwa au kukataliwa na wananchi through wawakilishi wao kule Senate, na ndiyo hoja ya Mbunge hapa Mheshimiwa sana Mama Super K,

  - Baraza la Senate, maana yake ndio wananchi wenyewe wanaosemwa hapo, ambapo kwetu Tanzania ni bunge, yaani Rais apendekeze mawaziri kama anavyompendekeza Waziri Mkuu, halafu wananchi yaani bunge ndilo linaamua kukubali au kukataa.

  - Kama huna uhakika na hoja iliyoko mezani, sometimes inasaidia sana kuuliza wengine, badala ya kuruka na hukumu ambazo ni nje ya mada, katika siasa bunge au Senate, wanawakilisha the people! Kama ninakuelewa ulivyomuelewa ina maana Mawaziri hawawezi kuchaguliwa na wananchi, meaning kwamba tutakuwa na chaguzi za wabunge, Rais, Madiwani, Mayors, halafu mawaziri it does not make a sense na Mheshimiwa Mbunge wa Same East, sicho alichoshauri.

  Respect.


  FMEs!
   
 14. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2010
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kila mtu ana uwezo wake binafsi wa kufikiri na hayo aliyoyarai ndiyo uwezo wake halisi wa kufikiria. Sioni haja ya kumlaumu sana bali ni wakati wenu muhimu wa kuwapima hawa wawakilishi uwezo na vision zao.
  Mtu mwerevu anakujia huku akifahamu vizuri kabisa kuwa wewe ni mwerevu halafu akakupa ushauri wa kijinga na ukauchukua...
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ameponda mfumo wa kuwapata mawaziri na kupendekeza kuwa wachaguliwe na wananchi kama ilivyo kwa rais.
  Wakati Kilango akisema hayo kwenye uzinduzi wa ripoti ya kujipima kwa kutumia vigezo vya utawala, mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa amesema nchi itavurugika kutokana na muswada wa sheria ya udhibiti wa fedha za uchaguzi unaoandaliwa kuwasilishwa kwenye mkutano ujao wa Bunge.

  Ndugu FMES,

  Nadhani tunapishana hoja,labda kama mwandishi kaandika kivyake lakini Mama K amesema kama ilivyo rais,basi ina maana wapigiwe kura kwenye ballot box,senate huidhinisha na si kuchagua.

  So Much Respects!
   
 16. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #16
  Jan 14, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mawaziri ni timu ya juu sana inayomsaidia Raisi katika utawala wake. Kuchaguliwa na wananchi maana yake ni kuliingiza taifa katika mitafaruku isiyo na maana. Sijasikia nchi yoyote duniani yenye mfumo wa Kilano.

  Ila nakubaliana naye kwamba kuna haja ya kubadili njia za uteuzi huo ili kuleta tija zaidi kwa taifa. Zaidi, kwamba wakuu wa wilaya na mikoa wanaweza kuchaguliwa na wananchi, hapo kwa kweli pananikuna. Uwakilishi wa kitaifa ubaki dhamana ya Rais, lakini mikoa na wilaya na kata wangechaguliwa kama wafanyavyo Marekani, maana mkuu wa mkoa atawajibika kwa waliomchagua ili achagulike tena, kadhalika mkuu wa wilaya na kata. Kwa sasa watu wanapewa zawadi ya ukuu wa wilaya na mkoa na hukalia kutukana matusi wananchi wao wanaowaongoza badala ya kiukwelikweli kuwahamasisha waendelee kiuchumi na kimaisha.

  Leka
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ni muda muafaka wizara zikawepo KIKATIBA ili kutomwachia Rais wetu mwanya kuunda baraza kubwa la mawaziri ambalo linakuwa mzigo kwa Taifa letu masikini na tija haionekani.
  Raisi mwenye wapambe/washirika/wafadhili/marafiki wengi anapata taabu kuunda baraza hili kama ilivyomtokea JK.
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Jan 14, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Eti Westminster system.Kwani lazima tuiige?Hatuwezi kuanzisha ya kwetu?
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,556
  Likes Received: 18,268
  Trophy Points: 280
  Mkuu FMEs, kwenye jibu langu hii iko wapi ?.'Kama huna uhakika na hoja iliyoko mezani, sometimes inasaidia sana kuuliza wengine, badala ya kuruka na hukumu ambazo ni nje ya mada'. 'Kama ninakuelewa ulivyomuelewa ina maana Mawaziri hawawezi kuchaguliwa na wananchi, meaning kwamba tutakuwa na chaguzi za wabunge, Rais, Madiwani, Mayors, halafu mawaziri it does not make a sense na Mheshimiwa Mbunge wa Same East, sicho alichoshauri'. Kwa mujibu wa andiko, hicho ndicho alichomaanisa ambacho wote mimi na wewe tunakubaliana, mimi nimesema kachemsha, wewe umesema it does not make sense. Unless Mama amenukuliwa vibaya na gazeti, na aliongea pengine kufafanua kuwa hicho unachosema wewe ndicho alichomanisha. Kama jibu langu limetokana na lile andiko, na jibu lako likatokana na andiko hilo hilo, them hicho alichomaanisha ambacho hakijaandikwa utakuwa umekipata wapi? unless you are thinking for her, ndio maana nikasema 'Naungana na vision yake wasichaguliwe na rais'. Hii ya kuwa vetted na bunge, sio kuchaguliwa ni kupitishwa tuu unless vetting ndio uchaguzi Mama aliomaanisha?.
   
 20. W

  WildCard JF-Expert Member

  #20
  Jan 14, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Pasco,
  Kwa FMES huyu mama ni kama vile huwa hakosei, hatelezi na wakati mwingine anafikiri na kuamua kwa niaba yake!
   
Loading...