Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Sina hamu na mikopo ya HESLB nimesha omba mara 2 na ku appeal mara 2 bila mafanikio yoyote. Ashukuriwe mungu nipo mwaka wa 3 sasa nategemea kumaliza degree yangu ya Logistics and Transport managemnt mwezi wa 7. Japo nimesoma kwa shida na kudhikika kwa kiasi chake lakini nashukuru namaliza salama.
 
Nina maanisha hivi nina mdogo wangu anasoma conas (UDSM) na kasoma shule za kata from kindergarten to university levels yupo mwaka wa kwanza just mwaka huu anasoma kwa kuunga unga since anakaa na dada yake anayemaliza mwaka huu sasa sjajua n vigezo gani vinahuska kuwapa watu mikopo maana walisema sciences wote watapata mikopo.... Na watoto n wa wakulima na sio wafanyakazi wa selikali. Nawasilisha kwa kufanyia marekebisho.
 
Watanzania wengi ni maneno na porojo tu hawana nia ya kuwasomesha Watanzania wenzao. Wamekalia majungu na kutafuna pesa za walipa kodi. Kazi kubwa tuliyonayo Watanzania ni kufahamu kwamba hakuna kitu cha bure, then kila mtu lazima alipe kodi, na wale ambao ni wezi wa pesa za walipa kodi ambao ni dada zetu, shemeji zetu wake/waume zetu na watoto wetu tusiwaonee aibu. Tuwafikishe kwenye vyombo vya dola wachukuliwe hatua kwa sababu tunawafahamu. Jinsi tunavyowachelewesha ndio jinsi tunavyochelewa kuendelea, msumeno lazima ukate kila upande usichague. Tukiwashughulikia wezi wa ndani tutaweza kumsomesha kila Mtanzania.
 
Hata mimi nilikuwa kimya kwa lengo la kuweka mikakati sawa, kukutana na wadau mbalimbali na kuona uwezekano wake kila eneo. Watu wengi wanaunga mkono. Tuanze mara tangazo litakapotoka wiki hii.
Kwa upande wangu najivunia sana we we, Tanzania ingepata watu watano au kumi kama wewe tungekuwa mbali sana. Watu wengi sana wanajua kucritisize tu na kuongea ili wao waonekane bora kuliko wengine, hawajui kuwa sufuria masizi ni asili yake, hata ukisugua kesho yanarudi tena. Ww umeonyesha kitu cha tofauti sana, badala ya kulalamikia serikali kumekuja na njia ya kuwawezesha. We proud of u kwa niaba ya wanafunzi wenzangu. Mungu akubarki sana mama.
 
Huu mpango uwe ni mfuko endelevu wa Vizazi na vizazi, kila mtanzania atakaeguswa achangie na michango iwe ni enedelevu pia, ili taifa letu liweze kusonga mbele kielemu pamoja na kutimiza ndoto za vijana wetu, Mwenyezi mungu ajalie Kheri ndani yake
 
Ni kweli elimu haina mwisho na haina madaraja katika utoaji wake. Kila mwenye nia ya kupata elimu ya kiwango chochote ni budi aipate, kwa hali na mali. Tuombe mfuko uanze mapema, ili tujue una nguvu kiasi gani na unaweza kufanya kiasi gani.
 
Huu mpango uwe ni mfuko endelevu wa Vizazi na vizazi, kila mtanzania atakaeguswa achangie na michango iwe ni enedelevu pia, ili taifa letu liweze kusonga mbele kielemu pamoja na kutimiza ndoto za vijana wetu, Mwenyezi mungu ajalie Kheri ndani yake
Amina. Ndilo ombi na lengo letu pia.
 
Wazo zuri sanaa asante kwa kutoa progress, huu uzi ungekua wa kuikejelii serikali zingekua page 1000plus za replies lakini cha ajabu kitu cha msingi kwa taifa letu watu wanapita tuu
Hakuna tatizo. Tuendelee kujadili. Watu wameonesha mwamko sana hata kama hawachangii hapa, watachangia mara utaratibu utakapokaa vizuri.
 
Nnd
Nndondo, una haki ya kutoa maoni yako, na mimi nina haki kushirikisha ualinacha wangu. Ndivyo tulivyo. Walioitikia wakichanga ndipo tutajua kama inawezekana ama la. Ni kweli kuwa elimu inatakiwa kulipiwa kwa kodi zetu, lakini ni kiasi gani hizo na ziko wapi? Mpaka sasa imesaidia wangapi, kama Bodi tu inachukua hao wachache? Kama iko njia ya kuhakikisha kodi zinatosheleza kulipia elimu bure kwa wote, itakuwa vizuri kuipata. Kama hatujaileta hiyo njia tujaribu zingine kwa sababu wanaokosa wanajua walichokosa.
 
Hslb kumejaa rushwa tupu yaaan mpaka uhonge ndo upate mkopo
, maana hakuna cha vgezo wala baby ake na vigezo
 
kuchanga tutachanga ila unakumbuka hela ya tetemeko mama yangu ?
Nakumbuka sana Miss ...ila angalia pia kuwa huu utakuwa mfuko wetu sis wananchi, sisi na watoto / vijana wetu/ sisi na kila anayetaka kujiongeza kielimu lakini anashindwa kwa kukosa hii nyenzo ya malipo yake. Mpaka sasa wamejitokeza wanafunzi wengi ambao hawana mkopo, wanataka mkopo warudi chuo, waongeze maarifa, waongeze kasi yao katika taifa. Ninamini kila mpenda maendeleo wa nchi hii na hata nje ya nchi ataona nia na lengo letu.
 
Naam Tumeanza na hatua zinakuja japo kwa mwendo pole. tuvumiliane. Wanafunzi wengi wamejitokeza baada ya kusikia. Tutatangaza tarehe ya kuzindua....
Wazo zuri sana mfuko uitwe Anna Mghwira Education Support Trust Fund( AESTF) nitawaambia rafiki zangu pale kwa Mfalme kule redsea[/QUOTE
 
Mpaka sasa tunatembea nalo! Tukaze nia mfuko uanze kufanya kazi. Tuombe pia Mungu abariki juhudi hizi. Tangazo linachelewa kiufundi. Likiwa tayari kila kitu kitakaa hewani. Asanteni sana.
UOTE="dudus, post: 19835488, member: 38243"]Wazo zuri sana Mama Mghwira. Ila angalizo, kuna wale ma-plagiarists wazoefu ataibuka RC mmoja (safari hii anaweza kuwa mwingine); ataliteka wazo; litaenezwa kwa propaganda kali halafu mwisho wataliharibu na kujisifia chama cha wanyonge kimejaribu! Kuweni makini na hawa majamaa japo manasema maendeleo hayana itikadi au vyama lakini wao ni mabingwa wa kutafuta sifa kupitia migongo ya wengie japo wazoefu wa kuharibu.[/QUOTE
 
Kweli kabisa Joel, tusaidie kujenga tanzania mpya bora! Twendeni na mfuko huu kupunguza tatizo. Halmashauri zitakazochukua zitapunguza sehemu nyingine nk. Tupanue wigo, tusifunge njia.
 
 
Asante ! Tuendelee tusonge mbele, inawezekana!
 
Elimu bure kutoka Darasa la kwanza mpaka Kidato cha nne, lakini ukifika hapo juu hakuna mikopo sasa hii elimu bure ina maana gani kama siyo danganya toto Maana ya elimu bure ni kupunguza gharama za kusomesha watoto lkn hapo juu mikopo inazuiliwa sasa hapo jamii imesaidikaje kupunguza gharama za kusomesha wakati elimu ya juu ndo gharama kuliko hapa chini basi hapa chini gharama zirudi ili wapate fedha za kukopesha, Tuseme ELIMU bure wamekurupuka...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…