Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Ninaikumbuka vema kauli ya mama Salma Kikwete kuwa nanukuu: " Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako." Leo watoto wa wenzetu wameingia tatizo la kukosa mikopo ya elimu ya juu; tuwasaidie kama watoto wetu.

Ninapenda kuwaomba akina mama wote nikianza na Mhe mama Salma Kikwete aliyeasisi usemi na hatua hii, tushirikiane kunusuru maisha ya elimu ya watoto walioko vyuoni wenye sifa ya kuwa na mikopo lakini hawakufanikiwa kupata mkopo. Tuwahamasishe vijana waliobakia mitaani na majumbani kujiunga na vyuo vikuu kuanua akili zao changa kukidhi ushindani wa sasa kimaisha.

Naomba akina mama wote viongozi, wazazi, walezi, wafanya bishara, waajiriwa, wanaharakati bila kujali itikadi zetu za aina yoyote tusimame kama wanawake wazazi wenye nia kuejnga taifa la watu walioelimika tuunde mfuko wa kuwasiadia watoto wetu wafanikiwe kumaliza masomo yao kwa ujenzi wa taifa letu.

Nikitoka na mama Kikwete ninaomba wake za marais wote waliopita kuanzia na mama Karume (mzee marehemu na Rais aliyemaliza mda wake) mpaka mama Janet Magufuli anayenivutia sana kwa kuonesha moyo wa amani sana kwa taifa letu.

Baada ya hao nimuombe mama Anna Makinda na wabunge wanawake wote waliopo na waliomaliza tangu uhuru wa nchi yetu tuungane kumsaidia kila mtoto wa Tanzania mwenye uwezo wa kusoma asome.

Kisha kwa niaba ya wanawake wafanya bishara niombe kitengo cha wanawake cha TCCIA, Baraza la Biashara la wanawake...tukubali wito huu: Tuungane kama wazazi na walezi chini ya kauli mbiu: Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako...tuunde mfuko wa elimu kwa ajili ya vijana wetu.

Niombe vyama vya wana-taaaluma: waalimu, madaktari, wahandisi, watumishi wa umma, mabenki, makampuni yote ya ndani na ya kigeni, asasi za kiraia za ndni na za kimataifa, balozi zetu zote, tuungane kuunda chombo hiki kuwasaidia vijana wetu.

Nimeguswa sana na mahangaiko ya vijana wa vyuo vikuu. Ninawashukuru wachache waliofika kwangu kueleza changamoto zao. Mmenihamasisha kuchangia kidogo elimu yenu lakini ninaomba hili liwe suala la kitaifa.

Ninaomba wanawake wenzangu popote tulipo tuwasiliane tuunde umoja huu kuwaimarisha na kuwapa tumaini vijana na janga la kukosa elimu ya juu kama wana sifa za kuipata.

Tuweke kando siasa, dini, kabila, ukanda ama aina yoyote ya kigezo kufanikisha jambo hili. Ninawashukru sana. Kesho kuna wanafunzi watashindwa kufanya mitihani kwa kukosa ada kidogo tu ya laki kuanzia 5-8. Mfuko wa mama Salma, Mfuko wa mama Mkapa wa Fursa sawa kwa wote, Taasisi ya Benjamini mkapa, Taasisi ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Mwalimu Nyerere, na zingine, tusaidiane kukamilisha azima hii. Na mimi nimeanzisha Taasisi ya Mama Anna Mghwira kwa ajili ya kushughulikia masuala ya aina hii.

Nitawashukuru sana kwa niaba ya vijana wetu, tuenzi elimu yao kwa kuunganisha nguvu zetu hivi. Mnisamehe kwa kuandika mtandaoni. Nimejaribu njia za kawaida za simu sikufanikiwa sana. Hapa ninajua kila moja atapata taarifa. Mapungufu yangu yasizuie jambo hili kutendeka. Jinsi tulivyo changia madawati, sasatuchangie elimu ya juu.

Niombe wizara na Bodi ya mikopo ya wanafunzi kutoa ushirikiano tutakapouhitaji utaalamu muwe nasi bega kwa bega.

Mungu atubariki wote, aibariki Tanzania.

Asanteni tena, ni mimi mama Anna Mghwira
Habar ya asbh wana jm! Kuhusu hili suala jaman Naona kimya kimekuwa kirefu. Hili muhimu sana kwa kufanikisha ndoto za wengi, tumuunge mkono mama yetu.
 
Kididimo, hiyo ndiyo roho ya nia hii...hakuna zaidi wala pungufu.!
Ninashukuru kwa kulifanyia kazi wazo langu. Post yako imewezeshwa "kuwa sticky thread".Tutaweza kuiaccess kwa wepesi katika kutoa michango yetu. Tutaomba mrejesho wa kila hatua. Ubarikiwe
 
Asante sana. Kwa sasa tunaandaa tangazo la kuweka mtandaoni. ninaomba maoni ya wadau lini tuanze kuchangia? tunawasiliana na mitandao ya simu tupate namba maalum za michango.
Tangazo litasaidia walengwa kuleta majina yao licha ya wale tuliopokea awali. Tukianza kuchangia na kusaidia wanafunzi wachache ndipo tutaweka tarehe ya uzinduzi rasmi.
 
Tangazo litasaidia walengwa kuleta majina yao licha ya wale tuliopokea awali. Tukianza kuchangia na kusaidia wanafunzi wachache ndipo tutaweka tarehe ya uzinduzi rasmi.
Hii ni fursa pekee kwa wanajamii forum kuonesha njia katika jambo hili kisha wengine wafuate. Asanteni sana na Karibuni sana. Nilitingwa kidogo na mukitano ndio sababu nilipotea lakini tupo vijana wanaandaa tangazo kisha mchakato uanze.
 
Hata mimi nilikuwa kimya kwa lengo la kuweka mikakati sawa, kukutana na wadau mbalimbali na kuona uwezekano wake kila eneo. Watu wengi wanaunga mkono. Tuanze mara tangazo litakapotoka wiki hii.
 
Aliepo madarakan kila siku anazid kuongeza vigezo vya kupata mikopo ili mrad wanafunz wng wasiipate hyo mikopo...
 
Hata mimi nilikuwa kimya kwa lengo la kuweka mikakati sawa, kukutana na wadau mbalimbali na kuona uwezekano wake kila eneo. Watu wengi wanaunga mkono. Tuanze mara tangazo litakapotoka wiki hii.
Hongera mama mungu yupo pamoja nasi kwenye hili....
 
Asante Kitukuu. Katika kuendelea kupata mkono wa umma nimeendesha vipindi vya luninga azam, chanel ten na star tv. Mwitikio ni mzuri. Ninaomba tangazo likitoka tuanze kutoa si
Habar ya asbh wana jm! Kuhusu hili suala jaman Naona kimya kimekuwa kirefu. Hili muhimu sana kwa kufanikisha ndoto za wengi, tumuunge mkono mama yetu.

Ndugu Mkwepa Kodi, naona umekwepa na maneno sasa. Sijui kama wengine wamekuelewa. Mimi nimetoka kapa.
Kna dogo masoma y kata Tena science yupo udsm.. Conas... Hana hata v0%
 
Asante Kitukuu. Katika kuendelea kupata mkono wa umma nimeendesha vipindi vya luninga azam, chanel ten na star tv. Mwitikio ni mzuri. Ninaomba tangazo likitoka tuanze kutoa si

Ndugu Mkwepa Kodi, naona umekwepa na maneno sasa. Sijui kama wengine wamekuelewa. Mimi nimetoka kapa.
Maoni ya ziada: Baada ya kupata muda wa vipindi na Luninga za Star, Azam,Ch Ten, mwaoni ya wadau yanaomba tuangalie pia kada la kundi la chini lililo kubwa zaidi na ambalo madhara yake kwa jamii ni makubwa zaidi: Kidato cha 4, 6, na hata darasa la 7 wasio na ujuzi wowote. Wadau / wasikilizaji wa vipindi waliomba tuliangalie hili kwa jicho tofauti. Ni vizuri kuweka rekodi sawa ili tutakapoanza tusisahau jambo hili. Asanteni
 
Ila mama Ndalichako ujue una wanao huku nyuma umewakanyagia chini bila huruma na misingi yao n mizuri tu,,fikiria Mara mbili mbili Tafadhali sana angalia hata mashuleni na mavyuoni pia angalia na uwezo wa familia,,,kwanini OD umeamua kuibagua!?
 
Mngekuwa mnakuja na hoja hizi majukwaani mngekuwa mmeshashika dola kitambo ila kwa siasa za matukio na kuwa vigeugeu, upinzani mtakesha.
 
Hata mimi nilikuwa kimya kwa lengo la kuweka mikakati sawa, kukutana na wadau mbalimbali na kuona uwezekano wake kila eneo. Watu wengi wanaunga mkono. Tuanze mara tangazo litakapotoka wiki hii.

Mama, asante na hongera kwa wazo hilo la kujenga. Mimi ninaomba nitoe ombi langu mahsusi kwako/kwenu kama taasisi, katika utoaji wa hiyo mikopo, muwaangalie kwa jicho la huruma pia na wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu kwa sifa linganifu (equivalents). Kwa kweli imekua ni vigumu mno kupata mkopo toka bodi kama umetokea diploma, imekua ni kana kwamba kuwa na diploma maana yake una ajira tayari au una hela tayari, ninakuomba sana katika vigezo vyenu visibague eti tu kwa sababu mtu katokea diploma ndio asipate mkopo. Ninaongea kama mhanga niliyekwama kuendelea na masomo na ninawajua wenzangu wengi mno waliokumbwa na kadhia hiyo.
Kila la heri, Mungu atalisimamia hili na ninaamini litafanikiwa.
 
Wazo ni la kialinacha,haya mambo yaliwezekana kwenye vyama vya ushirika vya uchagani na haikuwa bure bali kwa members against makato yao.pia kwa watoto wenye akili sio mabumbumbu, waulize kina mengi, sasa huyu anna anataka mimi nikachangia watoto.wawatu kwa uchungu gani wakati tayari nakatwa.kodi? Hawa ndio wanataka kuongoza nchi kwa misingi ya ujamaa karne hii? Eti huyu mama ndio awe.fund manager wetu, deci? Pole anna this is a daylight.dream, anather project failure, cont me out
 
Maoni ya ziada: Baada ya kupata muda wa vipindi na Luninga za Star, Azam,Ch Ten, mwaoni ya wadau yanaomba tuangalie pia kada la kundi la chini lililo kubwa zaidi na ambalo madhara yake kwa jamii ni makubwa zaidi: Kidato cha 4, 6, na hata darasa la 7 wasio na ujuzi wowote. Wadau / wasikilizaji wa vipindi waliomba tuliangalie hili kwa jicho tofauti. Ni vizuri kuweka rekodi sawa ili tutakapoanza tusisahau jambo hili. Asanteni
Wazo zuri sanaa asante kwa kutoa progress, huu uzi ungekua wa kuikejelii serikali zingekua page 1000plus za replies lakini cha ajabu kitu cha msingi kwa taifa letu watu wanapita tuu
 
Back
Top Bottom