Anna Kilango kutorudi bungeni...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anna Kilango kutorudi bungeni...?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MtazamoWangu, Jun 24, 2010.

 1. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kweli nguvu ya mafisadi imeonekana jimbo Same mashariki, na ukiona Mama Ana kilango analalamika kiasi kile bungeni basi AMINI ni masikitiko kutoka moyoni kwake....hali yake jimboni ni mbaya sana na hata watu wake wa karibu wamemshauri hali ni ngumu sana, fitina zilizopandwa ndani ya jimbo na pesa zilizomwaga basi zimefanya hata wale wananchi waliokuwa wakimpenda kujenga chuki nae.....
  Utafiti uliofanywa unaonyesha Mama Ana kilango huenda asirudi tena bungeni kwani upinzani ni mkubwa ssana, na kutokana na muda muwa mfupi kazi itakuwa kubwa kubadilisha matokeo....
   
 2. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwani yeye amemilikishwa?Mwambie aache unyerere kwamba same mali yake!
   
 3. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hiyoo ni demokrasia, tena wabunge wa sasa (ukiondoa wale wa upinzani) hawastahili kurejeaa bungeni kuendelezaa majunguu na unafikii wao...
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,925
  Trophy Points: 280
  Wananchi wa Same wasipomchagua(kama ni kweli hajawafanyia chochote)basi wananchi hao hawana haki ya uduma ya uongozi wa mama huyo and vice versa.
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jamani kwani Anne kilango alizaliwa awe mbunge!!!! na kama anahujumiwa yeye anashindwa nini kuhujumu hajui hiyo ndio siasa. Ukijengewa jungu na wewe pika lako it is the survival of the jungle. Mie nauliza kwanini asijiwekee mikakati ya kutetea jimbo lake badala ya kutaka sympathy from the public.
   
 6. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Aaache uvuvuzela kama Same Mashariki wanamkubali atapeta tu.....ila ajue hakuna mwenye hatimiliki ya jimbo ?
   
 7. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wanajamii, kama kuna mtu anamfahamu Anne Kilango au watu wake wa karibu, basi wamshauri asome (kama hajawahi kusoma) the damned book "Lo Prince" by Machiavelli ili ajuwe siri ya politik! That book gave the politcian an advice about what he/she should do to persevere and to promote in his/her position badala ya kulialia. Alitakiwa kujua by now kwamba politiks is a dirty game. There is no definite rules. Siasa ni kama ile PRO-WRESTLING ya zamani (late 80s); you can use everything near you: kick, punch, slap, na ukiweza ua kabisa.
  Laiti kama hayawezi haya, basi jibu lake ni rahisi; leave the dirty game to the dirty players and stop crying!:A S 20:
   
 8. T

  Taso JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Jungle halihitaji ku survive, litakuwepo tu, waishio kwenye jungle ndio wanahitaji ku survive.
   
 9. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Wakuu mmenena, si kawaida kwa siasa za ushindani kuendeshwa bila mikakati yenye hujuma. Mzigo ni kwa mshindani kuwa macho. Penye jinai basi achukue hatua stahili. Penye ujanja naye ajitahidi kuzidisha kete. Hulka ya wananchi wenzetu kununulika kwa vijisenti imejengeka sana nchini jambo ambalo kwa namna moja au nyingine limepewa promosheni nzito kinyemela na chama chake. Pengine hiki ndio kitakuwa kichocheo cha kurekebisha uozo humo ndani ya chama.
   
 10. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Kizazi kilichokwisha kata tamaa... kizazi kinachohalalisha ufirauni uwe ushujaa... kizazi kilichojaa ubinafsi.... kizazi kilichopotoka...... nani wa kukinusuru? Inashangaza watu tumefikia hatua ya kufurahia mbunge anapochoguliwa kitapeli na wale wanaotaka fair play tunawaona sio wajanja.... Afrika tuna kazi
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,099
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mafisadi bado wameshika hatamu ndani ya CCM na Serikalini hivyo watafanya kila wawezalo na kwa kutumia mabilioni yao ya kifisadi kupambana na wabaya wao na kuhakikisha hawarudi tena Bungeni baada ya uchaguzi. Bongo bila ufisadi inawezekana, mimi nakataa kauli hii umefisadi umeota mizizi kila pembe na vigumu mno kuushinda.
   
 12. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  shida ni kuongozana na Simba huku una harufu ya Swala,
  ni jambo gumu sana kuwa mbuzi katikati ya kundi la Chui
   
 13. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Nafikiri tumtafute mama kilango adhibitishe haya madai yako kwanza
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,925
  Trophy Points: 280
  Bubu;Tuko all the way pamoja....Isipokuwa tuliwaambia toka nyakati zile especially mama alipodai "Hapatakalika" "Patachimbika" nk...Tulisema ondokeni humo nyie mnaojiita wapiganaji,naona bado wanabisha,sasa kama hoja zao dhidi ya ufisadi ni kwenda kinyume na matakwa ya chama watamlaumu nani zaidi yao wenyewe?Tunasikia ccj hivi wapiganaji vile lakini hakuna action.

  Ok lets say wananchi hawajui umuhimu wa ufisadi nk,unataka kusema hakuna alilowafanyia kabisa hao wakazi wa same?Ndiyo maana nikasema kama kuna alichowafanyia,halafu na wao bado hawamtaki,then hawana haki ya kupata huduma ya uongozi bora wa mama huyo....Na adhabu yao itaendelea kuwa kubakia kwenye umasikini.

  Hizi ni issue ambazo walitakiwa wazifikirie long time ago na wajipange,inavyoonekana hawana long term strategies...yeye pamoja na wapiganaji wengine,unless upiganaji wao ni kujipanga tu kwa maslahi yao binafsi ndani ya ccm na si wananchi.
   
 15. K

  Keil JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Siku zote "wapambanaji" wamekuwa wakidai kwamba JK yuko upande wao, sasa kwenye hizi nominations ndiyo watajua rangi halisi ya JK. It is too late kwa kuwa watachezewa rafu na bado hakuna kitakachofanyika.

  Mkuu JMUSHI1 ninakubaliana na wewe, hawa watu walikuwa wakijidanganya kwamba JK yuko upande wao, juzi nimesikia wanaomba kuonana na JK. Hata kama wataonana nae sidhani kama atawasaidia kwa kuwa JK ni uzao wa UFISADI, hawezi kucheza mbali na mafisadi wenzake.

  Wameishalalamika kwa Makamba, haikusaidia. Wakahamia kwa Mkuchika akawa kimya, sasa wamehamia kwa Waziri Mkuu na kutishia kwamba damu itamwagika. Nani wa kumwaga damu? Hawa watanzania ninaowafahamu? Mbona CCM wakicheza rafu mbaya sana huwa hatusikii vitisho vya kumwaga damu?

  Wapiganaji wajilaumu wenyewe, kama kweli walikuwa serious na vita ya ufisadi wangejitenga na JK na kumuwekea ngumu. Kama CCM ingewafukuza uanachama, ndio wangekuwa wamepata kete nzuri ya kurudi mjengoni maana wangekuwa wamedhihirisha kwamba ni wapambanaji wa kweli. Sasa hivi ni ngumu sana kuwaelewa.
   
 16. N

  Ngala Senior Member

  #16
  Jun 25, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wanalia nini sasa maana walikuwa na mtaji wa kuwamaliza kabisa hao mafisi ufisadi???? leo hii wangekua wanahangika na kesi zao mahakamani katu hawangekua na muda wa kusumbua majimbona. nawauliza nani aliwatuma kuondoa rich mondulu mjengoni???? wasilie na wawe wapole walipaswa kujua hilo mapema. walitegwa wakaingia king kiulaiiiiiini
   
 17. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Enzi zile wapinzani walipokuwa wakilalamika rafu za majimboni CCM walikuwa wakichekelea waliona kama ngonjera za Mjomba sasa inakula kwao wanagombana wanyewe kwa wenyewe na bado tutaona mengi wakati wa kura za maoni.

  Ushauri kwa mama Anne Kilango, kama anaona mtumbwi unazama anachotakiwa ni kutoka ndani yake lakini kama ataamua kuendelea kukaa basi na avumilie mawimbi asitupigie kelele ajitahidi kuchota maji ayamwage nje hadi mawimbi yatakapotulia.
   
 18. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Kwani huyu mama ni lazima agombee kupitia ccm????
  Kama kweli anakubalika kwa wapiga kura wake na anaona anazongwa na mafisadi ndani ya ccm kwa nini asihamie vyama vingine ambavyo havina mnuko wa ufisadi??????? Au alikuwa amezoea tamu ya asali na ikamlewesha kiasi kujisahau anastuka alfajiri na kugundua kuwa wenzake tayari wako juu ya mti wakiwa kwenye harakati za kurina naye kwa kujihami anapiga makelele ya mwizi akitarajia wasamaria watajitokeza kumsaidia???????????????
  A LUTA CONTINUA DEMOKRASIA
   
 19. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa nini baadhi ya wana JF wanajifanya wanademokrasia lakini hapo hapo itokeapo mgombea pendwa anapata mpinzani tayari huyo mpinzani atahusishwa na ufisadi??? acheni kudharau wapiga kura kwani wao ndiyo wanaejuwa nani anafaa katika mazingira yao [It up to the voters to decide] Kabla ya mama huyu kulikuwa na mbunge mbona alivyobwagwa hakupiga kelele kama hizo?????
  Mimi sitoki jimbo la huyu mama hivyo basi pengine humu ndani mtuelimishe [kwa wanaotoka jimboni ] hali ikoje huko???? kwa nini mama analialia na kupakaza mara damu itamwagika mara mafisadi hivi kunani huko??????
   
 20. b

  bangusule Senior Member

  #20
  Jun 26, 2010
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Abunuwasi,

  ni kawaida ya anna kilango kutoa matamshi ya vitisho, kwa wanaomfahamu wala hawashangazwi na kauli za hivi karibuni. kama anna kilango ametishiwa kuuwawa kama anavyodai, kwanini haendi kushtaki polisi, badala yake anakwenda kushitaki kwa yussufu makamba? anna kilango alitumia mbinu chafu katika uchaguzi wa 2005, kwa kuanza kampeni za ubunge tangu mwaka 2000, na pia kumwaga fedha wakati wa kura za maoni za maoni na uchaguzi mkuu.

  kinachomtatiza anna kilango sasa hivi ni rekodi yake kama mbunge wa same mashariki. anna kilango ameshindwa kufuatilia ahadi ya raisi ya kujengwa kwa kiwango cha lami barabara ya mkomazi-ndungu-same. jimbo la same mashariki, na wilaya ya same, imeendelea kushika mkia mkoani kilimanjaro katika mitihani ya kitaifa na juhudi za mbunge katika suala la elimu hazionekani. kuna ufisadi wa kutisha katika uvunaji holela wa miti, na uharibifu wa vyanzo vya maji ktk jimbo la same mashariki, lakini mbunge haonyeshi kukerwa na ufisadi huo.

  kazi aliyoifanya anna kilango ni ndogo na hairidhishi. ukweli huo ndiyo unaosababisha akabiliwe na upinzani jimboni kwake.tayari amejitokeza naghenjwa kaboyoka "mama maendeleo" na dr.michael kadeghe kumpinga katika kura za maoni za ccm.

  soma jinsi hali ilivyokuwa tete mwaka 2005 baada ya anna kilango kumfanyia mchezo mchafu naghenjwa kaboyoka. wananchi walikuwa wanapeperusha bendera za ccm nusu mlingoti!!

   
Loading...