Anna Kilango amlipua Maige; Atoa CD zinazoonyesha madudu yake

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
ni kuhusu misitu, majangili wanaovamia misitu na dhahabu,, kwenye msitu wa shengena jimboni kwake,,, ambapo amesema ametoa filam kwenye msitu huo,,
 
athari za uchimbaji madini jimboni kwake ,,, na ameomba kusimamaisha uharibifu unaofanyika shengena na kuurudisha msitu kwenye hali yake ya kwanza,, amesema kuwa watu wanasema yeye ni mkali na yeye ni mkali ,, kweli si mchezo na amejifananisha na united nations,, mbuge huyo wa same mashariki ametoa onyo na masikitiko kwa serikali,, kuhusu athari za machimbo na uhariifu wa vyanzo vya maji kwa wananchi wa same,, na amesema hiyo filamu inahusu athari za machimbo,, jimboni kwake na amesema sinema hiyo ataipeleka kwa rais wazir mkuu na spika
 
Mama Anne kilango malecela wakati anachangia jioni hii amesema "Nimetengeneza sinema" naomba wanaojua mama ametengeneza sinema ya nini atujulishe tuitafute madukani.
 
Hana lolote huyo, harusi yake imefadhiriwa na JEETU PETEL, mtuhumiwa muhimu kwenye kesi za EPA na baadhi ya fedha alisingizia kuibwa pale Morogoro. Kumbe siri ikafichuka kuwa amemuingiza mjini mzee wa MTERA. Siyo mimi ni kauli ya Sophia Simba, mwenyekiti wa Umoja wa ma... wa CCM.
 
Inaonyesha jinsi mazingira yalivyo alibiwa katika mstu wa shengena,lkn hajasema amemshirikisha nani kwenye senema yake.
 
Leo Mbunge wa Same mashariki ameiumbua serikali na watendaji wake ngazi ya mkoa Kilimanjaro na wilaya Same. Kwa kuendelea kukaa kimya huku mlima shengena ukiharibiwa na wawekezaji wanao chimba dhahabu na bauxite na kusababisha chemchem ya maji kuathiriwa na kemikali zinazotokana na madini hayo. Aidha amewasilisha DVD 3 ambazo ameziita cinema za uharibifu mazingira. Waziri mkuu alionekana kuduwaa wakati wote ambapo mama kilango alikuwa akiongea.
 
Tunasubiri yanayokuja, kuna watu kitaota mbawa. Nampongeza huyu mama kwa hatua aliyofikia.
 
naisubiri kwa hamu kubwa kushuhudia akiwapiga mateke ya mbavu maadui zake.itanikumbusha zile movie za mwanamama cythia rothrock miaka ile ya 90.:eyebrows:
 
Alot of pomporsity out of nothing,.......no new newz hapa.
 
Tunakushukuru mama kwa kufundisha kwa vielelezo na zana halisi.Wanafunzi wako watalielewa somo kwa urahisi!
 
Ametengeneza DVD zinazoonyesha wawekezaji wanavyochimba madini huko Same na kuharibu mazingira.
 
Back
Top Bottom