Anna Kilango amlipua Maige; Atoa CD zinazoonyesha madudu yake

JUMANNE, JUNI 26, 2012 04:58

NA BAKARI KIMWANGA, DODOMA


*Atoa CD zinazoonyesha madudu yake
*JK, Dk Bilal na Pinda wapewa moja moja


MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM), amemlipua aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, kwamba alikuwa akishirikiana na watu kuharibu miti katika Msitu wa Shengena ulioko Same kwa ajili ya kuvuna dhahabu
Shutuma hizo alizitoa bungeni jana alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya mwaka wa fedha wa 2012/2013.

Ili kuthibitisha kauli yake, mbunge huyo alisema ameandaa CD maalum ambazo zinamuonyesha waziri ambaye hakumtaja jina akitoa maelekezo kwa watu hao kinyume cha sheria huku wananchi wakiendelea kuumia.

"Mheshimiwa Mwenyekiti, hali hii inasikitisha sana, wananchi wangu wanaumia sana kutokana na kunywa maji ya kemikali zinazomwagwa na majangili katika Msitu wa Shengena.

"Mara wanapozimwaga, miti hung'oka na wao kuchota dhahabu kinyume cha sheria na katika CD hizi, waziri huyo aliyekuwa Maliasili anaonekana waziwazi.

"Desemba 23 mwaka 2010, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alifanya ziara Same na kutembelea Msitu wa Shengena huku akiwa amefuata na watendaji wake zaidi ya 20.

"Kwa hali hiyo na kwa mujibu wa historia inaonyesha kuwa mwaka 1952 wana wa Meru walikwenda UN kudai ardhi yao na nina hakika hata Mheshimiwa mbunge wa sasa alikuwa hajazaliwa.

"Kwa hali hii na kule kwangu kuna mtu anaandaa harakati za kwenda UN, sasa ninamwambia mimi ndiyo UN na nitapambana kupigania haki za wana Same bila hofu.

"Kwa hali hii, nimeandaa sinema hii ikimuonyesha waziri pamoja na watendaji wake kwa sababu kila mara nimekuwa nikipigiwa simu na mtu mmoja anaitwa sijui Msusa, kutoka wizarani kunieleza hatua watakazochukua.

"Lakini mimi inanisaidia nini wakati ni kipindi cha miaka miwili wananchi wangu wanaumia kwa kunywa maji yenye kemikali.

"Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba CD hizi, moja iende kwa Rais aone jinsi huyo waziri na watu wake walivyokuwa wakifanya, nyingine iende kwa Makamu wa Rais kwa sababu anahusika na mazingira, nyingine iende kwa Waziri Mkuu na nyingine kwa Waziri wa Maliasili wa sasa," alisema Kilango bila kumtaja kwa jina waziri huyo.

Naye Mbunge wa Mbozi Mashariki, Gofrey Zambi (CCM), alisema haungi mkono bajeti hiyo ya Waziri Mkuu hadi yatakapotolewa maelezo kuhusu sakata la ununuzi wa kahawa mbichi.

Alisema kuwa, Serikali inatakiwa kutoa maelezo ya kina kuhusu hali hiyo huku akimlipua aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe, kwamba aliunda Bodi ya Kahawa kinyume cha sheria.

Alisema uteuzi wa wajumbe wa bodi hiyo ulifanywa kwa upendeleo kwani wajumbe wengi wanatoka katika kanda anayotoka waziri huyo.

"Mimi nikisema kuhusu jambo hili ninaambiwa kuwa nina maslahi, kwa hiyo, kama nina maslahi naomba nichunguzwe na ikibanika kweli ninataka ujumbe wa bodi niko tayari kuweka reheni ubunge wangu.

"Waziri alikuwa akikiuka sheria na kuzipitisha haraka haraka bila kufuata utaratibu, kwa hiyo, nasema mimi siungi mkono bajeti hii hadi hapo Waziri Mkuu atakapovunja bodi hiyo.

"Nawaomba wabunge wenzagu mniunge mkono ili tusiipitishe hadi hapo jambo hili litakapofanyiwa kazi," alisema Zambi.


stop lamenting mama fungua kesi na tumia hizi cd kama ushahidi watu wawajibishwe usitafute popularity za kijinga!!
 
Anne Kilango ni mpayukaji tu hana lolote.

Bado ana hasira za mumewe Mzee Malecela kuenguliwa kwenye kugombea Urahisi mwaka 2005. Hata hili swala analodai amelitengezea senema ni unafiki na upuuzi. Miaka yote hii alikuwa wapi kuleta hizo senema???Amesubiri mpaka CHADEMA walipoleta hoja ya kumng'oa PM kutokana na ufisadi wa Mawaziri hoja iliyopelekea kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri akiwemo Maige. Anachofanya ni just a comedy show.
 
stop lamenting mama fungua kesi na tumia hizi cd kama ushahidi watu wawajibishwe usitafute popularity za kijinga!!

Huyo yupo kwenye mashindano ya urembo,hana mpya mfano richmond alisema patachimbika lakini wapi.Kwenye miti hakuna wajenzi,ila tusiishie kulalamika tu JF bali kila mwenye nia ya dhati ya ukombozi afanye juhudi za ukombozi.
 
Back
Top Bottom