Ngoma ikivuma sana hupasuka na mwenye kiburi akishupaza sana shingo huvunjika mara
Tuwe na tuo tuwe na tafakuri kwenye maneno yetu...mtu anayejisifia rohombaya wazi wazi sio kwamba hana tu hekima lakini pia hana saburi na hatafakari matokeo ya kauli zake..huyu ni mwovu
Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri, bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu, huchochea ghadhabu huchochea visasi chuki na ubabe....dhima ya kiongozi ni kuleta umoja na maridhiano sio kuchochea chuki na visasi

Kiongozi mwenye hekima kamwe hawezi kuongea karaha..karaha huleta simanzi na majonzi, mtu wa karaha hana ogofyo lolote, ni kiburi na kiburi chake ni anguko
Nuru ya mtu mbaya huzimika ghafla bila tahadhari bila taarifa...mtu wa hekima hutengeneza patano kwa njia ya mashauriano
Je tunatengeneza ama tunabomoa?
Je tunahubiri amani ama visasi?
Je tunaeneza ustawi au anguko?
Je Tunafundisha hekima au upuuzi?
-hakuna kitu kibaya kama kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi