Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Huo si ukweli zile pesa zilipoondolewa Serikali ilisema zimewekwa BoT na hadi hii leo hajatamka lolote kuhusiana na pesa zile zinavyomuika. Na matokeo yake ya kuondoa 5 trillion kwenye mzunguko wa pesa benk zimepungukiwa pesa za kutoa mikopo na hivyo kusimamisha kutoa mikopo ya kibiashara etc kwa watu binafsi na pia makampuni mbali mbali nchini. Huyo Waziri wa Fedha au Ganava wa BoT hawajasema chochote kuhusu pesa zile kutumika katika miradi. wewe umekurupuka na hili bila ya kuwa na ushahidi wowote. Deni la Taifa liko Trillioni 67 unapunguza kwa 900 billion unajipigia makofi wakati huo huo waziri wa fedha yuko China na Korea kwenda kuomba mikopo mingine? Hiyo 900 billion kwenye deni la 67 trillion ni sawa na tone la mvua kwenye Indian Ocean.

Halafu wakati mnajipigia makofi kulipa bilioni 900 wakati huo huo mnaficha ukweli wa Magufuli kulipaisha deni la Taifa kwa 55.8% zaidi ya 24 Trillion ndani ya miezi saba tu ya kuwepo madarakani. Ukweli kwenu uko nusu nusu wakati mwingine uko robo robo. Unaongeza deni la Taifa kwa zaidi ya 24 trillion hutii neon unapiga kimya tu, unalipa bilioni 900 unajipiga kifua ili dunia nzima wajue huku mkitaka Watanzania tuamini deni la Taifa ni 51 Trilioni wakati ukweli ni kwamba deni limefikia trilioni 67 na si ajabu kuongezeka hadi trilioni 100 kabla ya July 2017.

Nani kakuambia ziko idle huko BOT? Serikali inazitumia kwenye miradi ya maendeleo na kulipa mishahara ya watumishi....kwa hiyo zinarudi kwenye mzunguko bila serikali kwenda CRDB kuzikopa kwa riba....hakuna pesa inayokaa idle, juzi serikali wamepunguza deni la Taifa unafikiri hizo pesa wamezitoa mbinguni?
 
Kesho litatoka taamko toka kwa Management ya CRDB ya kwamba uchumi wa Wa Bank Yao ipo vizuri na zile. Figure za hasara watu wazipuuze
 
Jamani usomee kwenye mikorosho au Mzumbe/oxford/mlimani wewe taja tu, lakini ukweli ni kwamba uchumi hutegemea mzunguko wa pesa.

Yaani kifupi ni hivi - Benki kuu- Mabenki ya biashara- Mwananchi/makampuni.......... Huu ndio ufupi wake, ukianza kufikiri kuwa mimi nacheza na pesa uliyonipa juzi ndio nakata cha juu halafu kinachobaki unanirudishia, ukaliona hilo ndio kosa, umepotea. Au ukaniona mimi tapeli kwa kufanya hivyo nakuonea huruma, kwa sababu pote duniani uchumi ndivyo hivyo unavyokwenda.

Ukadhani kuwabania mabenki hizo njia zote ndio umeyaweza mabenki, hakika nakwambia hiyo itakula kwako. Zingatia maneno yangu na yatunze ili yakufae kesho.

Tunapokwenda (kiuchumi) ni kubaya sana, kuna uwezekano wa kuiona Tanzania yenye mfano wa Zimbabwe. Yangu macho. Toka faida ya 37 bilioni mpaka hasara ya 2 bilioni, bado mnashangilia kweli watanzania ni magwiji wa siasa.
 
We nadhani hua hautembelei benki yoyote nchini; financial statement za mabenki yote nchini hua zipo tu kwenye notice boards zao, wala hua sio suala la siri; usilinganishe yaliotekea sehemu zingine (kama migodi ya barrack/acacia) na mabenki.
Ukiacha hayo mabenki financial statements na cash flow zinapikwa sana
 
Mkuu, mambo ambayo yalikuwa yakitendeka hapa nchini ni mambo ya hatari sana kuhusu uchumi wetu yaani haukuwa uchumi wa Tanzania, ulikuwa ni uchumi wa kigeni ulotawaliwa na dola na shilingi yetu ilifika hadi tshs 3800 kwa UGP 1! Yaani ilikuwa ikielekea Tshs 4,000!
Kweli mkuu.. Unajua Diamond amenizindua Kitu ananunua nyumba Africa kusini na haizidi milion Mia nne.. Nyumba mzuri.. Wakati hapa bongo huwezi kununua nyumba kama ile hata kwa milion miatano
 
Taasisi bhana wakiwa wana submit report zitakazotumika na m amlaka za kodi wanaonyesha wanapata hasara au faida kiduchu, lakini hao hao wakiwa wanataka mikopo wanaonyesha wanapata faida kubwa, ukitaka mwanao awe jizi la kutupwa mruhusu abobee kwenye hii kada
Kodi ya 30% haitozwi kwenye hiyo accounting profit inayoonekana kwenye financial statements. Inatozwa kwenye tax profit ambayo inakuwa adjusted from accounting profit. Kwa hiyo accounting profit inaweza ikawa kubwa(ndogo) halafu tax profit inaweza ikawa ndogo(kubwa)
 
Kodi ya 30% haitozwi kwenye hiyo accounting profit inayoonekana kwenye financial statements. Inatozwa kwenye tax profit ambayo inakuwa adjusted from accounting profit. Kwa hiyo accounting profit inaweza ikawa kubwa(ndogo) halafu tax profit inaweza ikawa ndogo(kubwa)
Vip umeshachukua Cpa
 
Tanzania bana.

Kila mtu ni mjuzi wa uchumi mpaka wengine wanapinga hata kinachoongewa na wataalam wa uchumi ambao wanafahamika kitaaluma.

Wale walisema half knowledge is worse than ignorance hawakukosea.
Mzee, wewe nadahni ukiamua kutema sumu hata Big November Crusade inaweza ikatawanyika! Umenichosha,...., half knowledge....
 
Kuna wakati kuishi kwa matumaini ni jambo jema maana hupunguza msongo wa mawazo. Nothing is on the ground to guarentee good economy for Tanzania in the near future.

Yaani mkuu, ka kifupi ni kwamba inatengenezwa "concept" ambayo inabidi ieleweke wazi.

Kama una shughuli rasmi inayokuingizia kipato basi huwezi kuwa una kiasi kikubwa cha fedha kwenye akaunti kinaingia kila wiki au kila mwezi, unafanya shughuli gani?

Je, kama una shughuli yoyote imesajiliwa?

Je, unayo TIN number na biashara yako imesajiliwa rasmi?

Je, unalipa kodi stahiki?

Kuna ishara fulanifulani kwamba mkulu anawashirikisha wataalam wa kutoka nje pia wanamsaidia kwenye masuala mbalimbali khasa haya ya kudhibiti uchumi.

Na wengine wanatoa ushauri wa kitaalam kuhusu namna ya kujenga mifumo mipya ya malipo iwe TRA au miamala ya ulipaji. ambayo ni imara.

PK amefanya hivyo kule Rwanda na amefanikiwa kwa haraka kwasababu yeye ana watu si zaidi ya milioni 3

Tusubiri January 2017 mambo yatakuwa mswano.
 
Kodi ya 30% haitozwi kwenye hiyo accounting profit inayoonekana kwenye financial statements. Inatozwa kwenye tax profit ambayo inakuwa adjusted from accounting profit. Kwa hiyo accounting profit inaweza ikawa kubwa(ndogo) halafu tax profit inaweza ikawa ndogo(kubwa)
Au sio mhasibu? Hizo degree zenu za kudesa shida sana.
 
Hapa kazi tu!

Jamaa anahifadhi fedha za taasisi zake za serikali Benki Kuu ambayo kimsingi haifanyi biashara ya fedha Bali kusimamia monetary policy. Matokeo yake money circulation nchini imedorora, na commercial banks zinalazima kukopa Benki Kuu.

Hii imesababisha interest rates against loans kupanda sana. Wakopaji wanashindwa kukopa, hivyo investments nazo kudorora. Kwa mwenendo huu kwa nini nchi isiingie kwenye recession!

Tuendelee kuimba " Hapa kazi tu" kiushabiki lakini kwa bahati mbaya uchumi haujui "ushabiki"
Ni ujinga kujifanya mabenki yako vizuri kumbe yanatunza hela za TRA, TANESCO, n.k bila serikali kupata faida. Mabenk yanatakiwa kutafuta mitaji na kufanya kazi na wafanya biashara kama wajenzi wa barabara, majumba, viwanda, nk ambavyo mwisho wa siku TRA watachukua kodi na TANESCO wataongeezea wateja na kuuza zaidi umeme. Kama walitegeme kutunza kodi za serikali, hela za mishahara ya watumishi wa serikali, mikopo ya wanafunzi, yote hiyo ni serikali, hawajikiti kutafuta wateja sekta binafsi kwa kina mengi, bakhresa, wachina, nk ili wakafie mbali huko
 
Karibu 5 trilioni imeondolewa kwenye mzunguko wa pesa nchini imelala pale BoT idle tu haifanyi kazi yoyote ile! wakati hii pesa ingekuwa kwenye mabenki ya biashara ingekuwa inazunguka kwa namna mbali mbali ikiwemo mikopo n.k. Hivyo benki za biashara zinafaidika na nchi pia inafaidika kwani watu wanakopa pesa wanafanya mambo mbali mbali ikiwemo kuinvest kwenye biashara mbali mbali, kufanya ujenzi etc. Wewe Rais hujik lolote kuhusu uchumi una washauru wa mambo ya uchumi lakini unakurupuka na kuondoa 5 trilioni shillings kwenye mzunguko wa pesa nchini.
wewe ndo hujui uchumi na si Raisi wako . alicho fanya ni sahihi kabisa ile competition ya mabank iwe sawa. na si bank moja iwe na hela zabure wakati nyingine zinateseka kua na hela. wacha mabenk yote yakope kwausawa .
 
20161031_142605.jpg
 
Tatizo siyo 2 bilion ila ulikuwa unatengeneza 30 bl sasa una loss ya 2 bilion.inamaana umepoteza faida 3o bilion na ukapata na hasara,ikiendelea kwa kiwango hicho loss itakayo fuata ni kubwa zaidi kwa sababu umetengeneza panic watu wataanza kutoa pesa kwa hofu na uwekaji utashuka unaweza kisia kuanzia hapo.
Benki kubwa kama CRDB profit au loss ya biioni 2 inatakiwa kuwa mahesabu ya siku au wiki.

Inaonekana kama loss ni kubwa zaidi wana i minimize.

Wahasibu wana tricks zao za kucheza na balance sheets, profit and loss statement etc.

Inanishangaza kuona CRDB inashindwa kupata 2 bilion quarter nzima ku break even.

Hata kama hilo ni kweli, hapo kuna lack of drive inaonekana viongozi hawaendeshi benki vizuri.
 
BOT ineshidwa kufanya kazi yake ya kuwa mkopeshaji wa mabenkiya kibiashara na hivyo kufanya mikopo iwe ghali zaidi kutokana na gharama za amana ambazo benki hizi zinaingia kupata amana.
Pia kwa serikali kuhamisha pesa zote kwenye mabenki kumeatbiri ukopeshaji ili kuanzisha shughuli mpya za kiuchumi au kuendeleza zile za zamani. Importers wanategemea mikopo katika biashara zao huwezi kuangiza mzigo ukauuza same day i uweze kuagiza mwingine matokeo yake yanaenda kugusa sekta nyingine kama Bandari.
Kupata hasara katika mabenki kama nilivyosema hapo mwanzo biashara nyingi zimesimama uwezo wa kulipa mikopo ya wafanyabiashara hasa wadogo umekuwa mgumu hivyo mikopo imekuwa mibaya sheria za uendeshaji wa mabenki chini ya usimamizi wa BOT inazitaka benki kufuta mikopo mibaya kwenye vitabu vyake kupitia faida ili kuendelea kuwadai wakopaji wakati tayari wameifuta na pale wanalipa basi inaongezwa kwenye faida ya mwaka mkopaji huyu anapolipa.
Hii unaweza iona katika vitabu vya CRDB wamefuta mikopo mibaya ya almost 38billion ambayo ni wazi imepunguza faida kwa 38billion lakini hii inavifanya vitabu vyake kuwa safi na kutengeneza mkakati mpya. Jambo kama hili lilitikea miaka miwili iliyopita kwa NBC ambao walipata hasara ya kama 2billion kwa mwaka huo tofauti na Crdb wao bado kwa majumuisho ya kipindi cha robo tatu bado wanafaida ya zaidi ya 100 billion na uwezekano wa kupata faida zaidi kwa mwaka 2016 ni mkubwa kwasababu tayri sehemu kubwa ya mikopo yake mibaya ambayo inakula faida amekwisha ifuta kwenye vitabu vyake na kuwa deni la kawaida kwa wakopaji.

Ushauri:
1. Serikali kuzipa nafasi mabenki kutumia pesa wanazokusanya kutoka a maduhuri ya serikali kubaki huko ili waweze kukopesha au

2. BOT kufanya kazi ya kuyakopesha manenki ili nayo yaweze kukopesha kwa riba nafuu kwa wananchi na kukuza uchumi.

Tahadhari;
Kwa mabenki kushindwa kuwa na amana za kutosha kwa serikali kukimbizia makusanyo yote (ambayo commericial benki ndo wakusanyaji) itaua uwezo wa mabenki na hivyo ukusanyaji wa mapato ya serikali ukawa mgumu kwa vile BOT hawana matawi nchi nzima.

Pia serikali itambue mabe ki ni mshirika wake katika kujenga uchumi na hatua zizote za kudhoofiisha sekta hii ni kuua uchumi.

Mwisho kodi inaongezeka kwa kuwa na uwekezaji mpya hivyo serikali inatakiwa kuhamasisha uwekezaji binafsi i kuweza kuvuna kodi la sivyo tukimaliza kukusanya hizi Tax arrears tunatabaki hatuna cha kukusanya (hili limeanza kujitokeza utaona malengo ya umusanyaji wa mwezi October yatavyofikiwa kwa mbinde)


Labda hii hasara inatokana na mikopo waliopewa wafanyakazi hewa 17,500 ambao wamegundulika na serikali ya Magufuli.
 
Huo si ukweli zile pesa zilipoondolewa Serikali ilisema zimewekwa BoT na hadi hii leo hajatamka lolote kuhusiana na pesa zile zinavyomuika. Na matokeo yake ya kuondoa 5 trillion kwenye mzunguko wa pesa benk zimepungukiwa pesa za kutoa mikopo na hivyo kusimamisha kutoa mikopo ya kibiashara etc kwa watu binafsi na pia makampuni mbali mbali nchini. Huyo Waziri wa Fedha au Ganava wa BoT hawajasema chochote kuhusu pesa zile kutumika katika miradi. wewe umekurupuka na hili bila ya kuwa na ushahidi wowote. Deni la Taifa liko Trillioni 67 unapunguza kwa 900 billion unajipigia makofi wakati huo huo waziri wa fedha yuko China na Korea kwenda kuomba mikopo mingine? Hiyo 900 billion kwenye deni la 67 trillion ni sawa na tone la mvua kwenye Indian Ocean.

Halafu wakati mnajipigia makofi kulipa bilioni 900 wakati huo huo mnaficha ukweli wa Magufuli kulipaisha deni la Taifa kwa 55.8% zaidi ya 24 Trillion ndani ya miezi saba tu ya kuwepo madarakani. Ukweli kwenu uko nusu nusu wakati mwingine uko robo robo. Unaongeza deni la Taifa kwa zaidi ya 24 trillion hutii neon unapiga kimya tu, unalipa bilioni 900 unajipiga kifua ili dunia nzima wajue huku mkitaka Watanzania tuamini deni la Taifa ni 51 Trilioni wakati ukweli ni kwamba deni limefikia trilioni 67 na si ajabu kuongezeka hadi trilioni 100 kabla ya July 2017.
Mkuu BAK

Tunaongopewa pesa ipo BoT lakini ni uongo!! Bwana mkubwa amefanya expenditure ya ajabu ktk kulipa madeni ya nje na ununuzi wa ndege!! Mapato yamepungua na serikali imeelemewa na madeni!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom