Anguko kuu la Kikwete na CCM, dalili zimeanza

Anguko kuu la Kikwete na CCM, dalili zimeanza

Status
Not open for further replies.
hana lake hakuna asiyejua hili

hatuwezi kuwa na mtu ovyo namna hii.
 
Baada ya mgombea wa Chadema, Dk Slaa kufanikiwa kufikisha ujumbe wa 'ukombozi wa Tanzania' kupitia mikutano yake ya kampeni na kwenye runinga, sasa ni dhahiri kwamba Watanzania wengi zaidi wapo tayari kwa mabadiliko, wanataka Tanzania mpya yenye neema. Mazungumzo kwenye daladala, vijiwe, maofisini na bar ni Dk Slaa na mabadiliko makubwa yanayayokuja chini ya utawala wake. Hakika sasa anguko la Kikwete ni dhahiri.

Mzee:

Utu ni taasisi pana! Taasisi ambayo ndio uti wa mgongo wa maendeleo ya mtu na jamii yake.

Alikuwa JK Nyerere peke yake na sasa, Dr W Slaa ... aliyekuwa anadhubutu Kuusemea Utu na kuuweka kama kigezo cha ustawi wa Taifa!

Bila Utu, ambao ndiyo asili ya Mtu, maendeleo yote hayana maana yoyote! Yanakuwa ni maendeleo ya vitu! Ni utu kwanza...uwe chimbuko la demokrasia na maendeleo ya Taifa.

Utu ni Uungu ndani mtu, hatuwezi kuusaliti tukabaki salama kama watu... lazima utu kutangulia kila nyanja ya jamii bila hivyo hicho kinachoitwa ustawi, maendeleo na demokrasia vinakuwa havina maana.

Maendeleo ya Utu ndio yatawale maendeleo na ustawi wa jamii na taifa, na si maendeleo ya vitu bila kuujali, kuujenga na kuuendeleza utu.

Kitaalam: Utu unanyaushwa, kuharibiwa na kuangamizwa na UFISADI.

Kiua Utu ni Ufisadi. Kauli mbiu ni Utu Kwanza na Si ufisadi Kwanza.

Utu unarutubishwa na haki, upendo, maadili ya uongozi bora, kuheshimiana, haki na usawa wa pato la taifa, matumaini, ukweli, ujasiri na si ukatili, uimara wa kusimamia na kutetea sauti ya umma, utambuzi wa dhana nzima ya utu na kuwaongoza watu kuelekea kilele cha utu wao kama ukombozi wa mwandamu.

Ni Kweli na hakika: CCM na Kikwete wameutupilia mabali Utu ulioasili ya Mtu na kukumbatia kwa kiwango cha kutisha cha Ufisadi. Nani mwenye utu kamili anabishia hili?

Baada ya CCM na Kikwete kusaliti asili ya mtu, kinachofuatia nchini ni Mgawanyiko na Matabaka kwa Taifa. Mgawanyiko na mtabaka hayo vinazaa Udini, ukabila, kuimarisha, ujinga, dhuluma, maradhi nk. Kisa? Utu umewekwa kando, tumeutwika Ufisadi na sasa tumeisaliti asili yetu kama binaadamu. Na kama utu haupo ...ina maana tunatawaliwa na kinyume cha utu...ambacho ni unyama ndani ya Mtu, yaani ufisadi... Na usiombe kuishi ndani ya jamii au Taifa kama hilo! Nani haoni kiama kinachoweza kufuatia hapo?

CCM na Kikwete wana Utu na misingi yake ya kujibu hoja hii? Labda kwanza wawafilisi Mafisadi Papa Kumi (Kumi na Moja) waliowekwa hadharani tayari… Vinginevyo wakati wa kuichai nchi ni sasa!

Kwa kuwa CCM badala ya kupunguza maadui wa ustawi wa maendeleo ya jamii ya watanzania kutoka kuwa wa nne, sasa wanawajenga na kufikia sita. Yaani Ujinga, Maradhi, Umasikini, Ufisadi(Dhuluma), Ukabila na Udini.


Tunahoji: CCM na Kikwete wanacha kujitetea kwenye hili? Mna Utu na Ubinaadamu wa kuhitaji kuliongoza kwa hekima, utulivu na amani Taifa hili kwa kipindi kingine cha miaka mitano? ... tuwasikie!!
 
Akiachia ngazi jk basi daima milele atakua shujaa wangu.
 
mtu mbishi hata awekwe kwenye chupa bado atanyoosha kidole

ndo kikwete
 
Watashangaa wiki ijayo matokeo yatakapotoka, tena halali kabisaa kwa JK kupata 70%.
Ni sawa, vijana wa mjini wanamuunga mkono Slaa na Chadema yake. Hata hivyo Wa Tz walio wengi wako vijijini ambako ndiko ngome ya CCM iliko.
Tujiandae kupokea matokeo ya ushindi wa CCM.
 
Nilimsikia akisema ana shamba lake kubwa la mananasi na anafuga ng'ombe wa kisasa. Ingekuwa jambo jema sana kama baada ya 31.10.2010 akakubali matokeo kwa tabasamu na kuamua kwenda kuendeleza mashamba yake na mmifugo.
Na sisi kwa uungwana huo tutaendelea kumlipa pension na kumtunza maisha yake kwa mujibu wa sheria zetu. Aweke pamba masikioni maana hao wapambe wake ndio wanampoteza kwa vile wanakiogopa kiama kitakacho wakuta baada ya Dr. kupigiwa mizinga 21. Wanajua mwisho wa majigambo na kebehi umefika na pengine sala zao ni JK awe Rais wa maisha maana ndiye walikuwa na uwezo wa kum drive wapendavyo.
 
Watashangaa wiki ijayo matokeo yatakapotoka, tena halali kabisaa kwa JK kupata 70%.
Ni sawa, vijana wa mjini wanamuunga mkono Slaa na Chadema yake. Hata hivyo Wa Tz walio wengi wako vijijini ambako ndiko ngome ya CCM iliko.
Tujiandae kupokea matokeo ya ushindi wa CCM.

Swala hapa sio ngome ni kwamba wananchi vijijini na mijini wamemchoka huyu jamaa.
 
Watashangaa wiki ijayo matokeo yatakapotoka, tena halali kabisaa kwa JK kupata 70%.
Ni sawa, vijana wa mjini wanamuunga mkono Slaa na Chadema yake. Hata hivyo Wa Tz walio wengi wako vijijini ambako ndiko ngome ya CCM iliko.
Tujiandae kupokea matokeo ya ushindi wa CCM.

Hapa unakubali kwamba CCM mtaji wao ni ujinga wa Watanzania. Na ndiyo maana hawakubaliki mjini maana mjini watu wamesoma , wametembea na huwezi kuwadanganya. Hivyo mtaji pekee wa CCM ni kuvuruga elimu ili watu waendel;ee kuwa wajinga na wasiweze kuinyoshea kidole.
Kazi kweli kweli.....
 
Kikwete asiwe na wasiwasi kwani nilimsikia Dk Slaa jana akisema atamlinda iwapo ataachia madaraka kwa amani na kwenda kuishi kama private citizen huku akiwa na heshima ya rais mstaafu.
 
Watashangaa wiki ijayo matokeo yatakapotoka, tena halali kabisaa kwa JK kupata 70%.
Ni sawa, vijana wa mjini wanamuunga mkono Slaa na Chadema yake. Hata hivyo Wa Tz walio wengi wako vijijini ambako ndiko ngome ya CCM iliko.
Tujiandae kupokea matokeo ya ushindi wa CCM.

Si Ajabu unaandika kutoka mlima fulani yani Meru, kwa taarifa yako Chadema ndio jibu
 
Si Ajabu unaandika kutoka mlima fulani yani Meru, kwa taarifa yako Chadema ndio jibu

Karibu loshoro na ngararumu Ndugu yangu Mang'ang'a. Niko Nturu wa Kyuta. Hata hivyo tunaomba kura yako usiipoteze kwa chama kitakachoshindwa. Mpe JK.
 
Avalanche ya Dk wa ukweli nani wa kuizuia? Sasa ni kama gari Moshi lililokatika breki, kusimama kwake ni mjengoni kule Magogoni.
 
Ni nani kati ya wantanzania wapatao takribani zaidi ya milion 40 aliyesadiki habari tulizozileta kuhusu anguko la chama cha mafisadi?
nao wakaja na maneno yao waliyoyatoa kwenye ngoma za mdundiko wakisema, hakika hatatokea mtu miongoni mwa watanzania atayethubutu kuichezea ccm. wakatoa kashifa nyingi na uzushi mwingi kuhusu maneno yaliyo tabiriwa na wanamapinduzi wa kweli.
Lakini kwa hekima na busara na welevu wa wanamapinduzi hakuna hata mmoja aliyefunua kinywa chake kubishana nao. leo hii wananchi wameamua kutoka rohoni mwao kukiacha chama cha majambazi na kuwapa fursa watu wenye nia njema na mapenzi mema na TZ, bado ccm mnataka kuzuia. Nasema hatuta nyamaza kusema. mkwere na hao jamaa zako acheni kulazimisha ushindi. na hata mkitunyamazisha kwa nguvu, basi hata mawe na milima yote itadai haki ya wananchi watanzania.
hatukuhitaji tena.

Hili ndo anguko lililonenwa. acha litimie
na ndio mwanza wa ukombozi wa watanzani
Nawakilisha
 
Kila baada ya tufani kuna anga zuri la dhahabu, nguvu ya umma itashida hata kama sio leo
 
Hata Kenya ilianza hivi.
Just before 2015 kutakuwa na mmeguko mkubwa wa CCM kwenda Chadema wakihofia kupoteza nafasi zao.
Eventually Chadema shall have grown strong na itachukua Kiulaini.
Unless rt now JK aamue kuunda serikali ya muungano to tame them.
Otherwise they should expect the worst.

Plan B..... (free advice to ccm) they should impress the people especially wale ambao hali zao ni ngumu na wamesahaulika...then they create an impression that they are doing better...(digging bore holes for pple in Same, tarmaking roads in Arusha, coming up with a cheap rural electrification scheme etc...etc)
this should be done within the first 2 years
Baada ya hapo they prepare a nice budget for buying back all the serious shots of Chadema
Watakuwa wame weza
NB: this is my personal analysis and the way i see thing.
 
Watu wenye hekima huwasha taa zao na kuziweka kwenye kinara ili zitoe mwanga, na wapumbavu huwasha taa zao na kuziweka uvunguni au huzifunika na pishi hivyo giza hutawala. Siku zote shetani ni baba wa uongo, yeye husema uongo, huwadanganya watu na baadae huwaaibisha. Katika aibu hii anguko kubwa hutokea na ushindi kawaida ni kwa Mungu aliye hai, Muumba mbingu na nchi alaaniye, uovu na kuwapilia mbali wanaomdharau huko ndiko kilio na kusaga meno hutawala.
 
Labda amchague Pombe Magufuli waziri mkuu, na amwache aiendeshe serekali kivyake yeye akila kuku USA kama kawaida. Hapo anakuwa kwa kiasi fulani amemwachia kukaimu urasi huyu Pombe wakati aki-strategize uraisi kamili 2015.
 
It's a matter of time, time will tell in due season coz we're really fade up with CCM, part of crooks, den of thieves and the list goes on. This part doesn't deserve to be in Tanzania at all, first it embarrasses tanzanians, it profits only certain group of selected people at the expense of tanzianian resourses. THIS part deserves to be purged, as for now i'm sure Nyerere in his grave is crying deeply and agonized with tanzanians badly.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom