Anguko kuu la Kikwete na CCM, dalili zimeanza

Anguko kuu la Kikwete na CCM, dalili zimeanza

Status
Not open for further replies.
Maji yamewafika kushingo. Karibu watazama.
 
Kazi Ipo, Nikiangania next 5 years Naona Chenga chenga,
 
With six days left to vote, hii article bado inaresonate in my mind!
 
ukweli siku zote unaonekana tu, na wala hautungwi vigezo vyote ulivyo tumia viko wazi, kazi njema.
 
Baada ya mgombea wa Chadema, Dk Slaa kufanikiwa kufikisha ujumbe wa 'ukombozi wa Tanzania' kupitia mikutano yake ya kampeni na kwenye runinga, sasa ni dhahiri kwamba Watanzania wengi zaidi wapo tayari kwa mabadiliko, wanataka Tanzania mpya yenye neema. Mazungumzo kwenye daladala, vijiwe, maofisini na bar ni Dk Slaa na mabadiliko makubwa yanayayokuja chini ya utawala wake. Hakika sasa anguko la Kikwete ni dhahiri.
 
Ni kweli unachosema. Hata mie leo nilikuwa kwenye daladala nikitokea Mbagala kuja Ubungo. Jamaa mmoja alipandia kituo cha mtongani. Kwa kutaka kuwachokoza wananchi alisema "CCM oyeee" watu wote waliguna na wengi wao wakakunja uso na hawakutaka kumjibu chochote.

Tulipofika kwa zizi Ally akaropoka tena "CHADEMA oyeeee" watu walicheka na kushangilia, na hapo ndipo watu kwenye daladala walipoanza kuongea kila mtu akisema tunataka mabadiliko mwaka huu upuuzi hatutaki.

Hapo ndo nilijua kumbe Dr. Slaa watu wanamhitaji tofauti na CCM wanavyodai. Sikutegemea kama basi zima asipatikane hata mshabiki mmoja wa CCM kumuunga mkono jamaa aliyeropoka.

Hivyo basi usemi wako ni kweli kila kona watu sasa hivi mazungumzo ni Dr Slaa
 
Kikwete amekwisha shindwa uchaguzi pamoja na kwamba aturudi kukaa pale magogoni na kujiita Rais. second term president ukipata upinzani mkubwa namna hii ujue kuna jambo au mambo makubwa umekosea sana. kinachonitia mashaka makubwa ni hiki hapa, Je Kikwete anayo busara ya kukubali kuachia madaraka kama walivyofanya kina Kaunda? na kwenda kupumzika kwa amani? Je anajua kwamba akifanya hivyo ataheshimika sana Barani Afrika ? na hata haya mambo ya kifisadi yatafunikwa na hilo.
JIBU- kama ameshindwa kutumia busara zake(kama anazo) hasa kipindi hiki cha uchaguzi kujua kwamba kwenda Rombo kwa Mramba ni makosa, Lowasa, na hata Chenge hawatakiwi kuonenaka karibu na yeye wakati huu, hata kama ni washikaji wake, Je busara ya kuachia madaraka anayo?
 
Sisi tulishaanza kushangilia ushindi dhidi ya uovu wa CCM.:israel:

:israel:



:israel:
 
Jana nilikuwa nanunua k'moto sehemu - nikawakuta Madogo 3 wapo jikoni nikawaulza kwa uchokozi tu " Oyaa kilo moja bei gani? wakajibu 6500, Nikaguna wakasema Bro unaguna nini? Mchague tena kikwete ili ukirudi hapa utakuta bei ni sh 12,000/- huku mmoja aliyesema akicheka.

Nikawaambia Nyie mnaona nani anafaa? hamjui Kikwete kawasaidia hadi mnategeneza hiki k'mto kwa amani? Madogo wakacheka wakaniambia Bro hebu hakikisha kmoto yako kama ipo fresh tukutengenezee uondoke huyo JK ni wako kamchague wewe. Nikauliza Je mmejiandikisha? wakasema sisi tunasuburi 31st tufanye uamuzi wetu. Nika smile nikaondoka kuketi nikisubiri mlo wangu. nikajua mwaka huu ngoma nzito JK mwisha kazii.....
 
Kikwete anayo busara ya kuachia madaraka na nadhani alijua kuwa hilo la yeye kushindwa kwenye uchaguzi linawezekana na ndio maana akajitayalisha kwa kumalizia kujenga nyumba zake huko kwao Msoga na hapo Regent Dar!!Wapambe wake ndio nuksi kwani hawataki aachie ngazi hata pale wanapofahamu kuwa si tukwamba atakosa kura bali afya yake haimruhusu!!
 
Huku Arusha JK na mbunge wake Batilda walishapigwa chini mapema. mambo yote ni SLAA tu.
 
Mimi nilikuwa nawasiliana na jamaa zangu huko kijijini kuwahamasisha wasikose kwenda kupiga kura na kuwashawishi kuwa wampigie DR!! Wakanirudishia ujumbe kuwa nisiwe na shaka kijijini kwetu wote ni watu wa Slaa TU; nikafarijika sana.
 
JK kwa mujibu wa demokrasia kwisha habari yake. Kwa mujibu wa UDIKTETA atalazaimisha kurudi magogoni. Lakini hii ni 2010 sio 2005. Tumeendelea sana kimtizamo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom