Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 975
- 47
Angella kuvuliwa mataji yote?!!
Ni baada ya kukiuka mkataba wa kurudisha taji la balozi wa Redds alilotunukiwa katika fainali za kumsaka mrembo wa Tanzania 2008 ndani ya viwanja vya Leaders club
Habari zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam zinasema kuwa Angela ambaye pia anashikilia taji la Miss Temeke 2008 na lile la Changombe 2008 anashutumiwa kukiuka makubaliano baina yake na Kamati ya Miss Tanzania.
Inaelezwa kuwa kabla ya kushiriki shindano la Miss Tanzania, Kamati ya shindano hilo chini ya Mkurugenzi wake Hashim Lundenga, huwa inawakabidhi warembo wote mkataba na kukaa nao kwa siku moja ili wausome na kuuelewa, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wazazi au walezi wao na ndipo wausaini.
Katika mkataba huo kipengele kinachosema kuwa mrembo yoyote ni lazima akubali kufanya kazi zozote za wadhamini wa shindano hilo, ilimradi tu kamati ya Miss Tanzania iridhie.
Angela, akiwa kama mmoja wa warembo waliowania taji la Miss Tanzania mwaka huu, pia alisaini mkataba huo kabla ya kuanza kambi. Mbali na hilo mrembo huyo alishiriki katika shindano la kumtafuta Balozi wa
Redds lililofanyika mkoani Mwanza.
Atalazimika kuvua mataji yote, kanuni ni zile zile toka ngazi ya kitongoji, kanda hadi taifa, mtu huwezi kuvua Blauzi ukabaki na sketi, akitaka kuvua nguo, ni lazima avue zote, sio moja, alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Miss tanzania. Endapo atavuliwa mataji yote, Angela atatakiwa kurudisha zawadi zote alizopata kuanzia ngazi ya kitongoji cha Chagombe kanda ya Temeke hadi taifa.
Wakati huo huo, Lundega alisema kuwa anatarajia kukutana na wajumbe wenzake ili kujadili suala hilo na kutoa uamuzi