Angella kuvuliwa mataji yote?!!

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
976
47
Angella kuvuliwa mataji yote?!!

Ni baada ya kukiuka mkataba wa kurudisha taji la balozi wa Redds alilotunukiwa katika fainali za kumsaka mrembo wa Tanzania 2008 ndani ya viwanja vya Leaders club

Habari zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam zinasema kuwa Angela ambaye pia anashikilia taji la Miss Temeke 2008 na lile la Chang’ombe 2008 anashutumiwa kukiuka makubaliano baina yake na Kamati ya Miss Tanzania.

Inaelezwa kuwa kabla ya kushiriki shindano la Miss Tanzania, Kamati ya shindano hilo chini ya Mkurugenzi wake Hashim Lundenga, huwa inawakabidhi warembo wote mkataba na kukaa nao kwa siku moja ili wausome na kuuelewa, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wazazi au walezi wao na ndipo wausaini.

Katika mkataba huo kipengele kinachosema kuwa mrembo yoyote ni lazima akubali kufanya kazi zozote za wadhamini wa shindano hilo, ilimradi tu kamati ya Miss Tanzania iridhie.

Angela, akiwa kama mmoja wa warembo waliowania taji la Miss Tanzania mwaka huu, pia alisaini mkataba huo kabla ya kuanza kambi. Mbali na hilo mrembo huyo alishiriki katika shindano la kumtafuta Balozi wa
Redd’s lililofanyika mkoani Mwanza.

“Atalazimika kuvua mataji yote, kanuni ni zile zile toka ngazi ya kitongoji, kanda hadi taifa, mtu huwezi kuvua Blauzi ukabaki na sketi, akitaka kuvua nguo, ni lazima avue zote, sio moja,” alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Miss tanzania. Endapo atavuliwa mataji yote, Angela atatakiwa kurudisha zawadi zote alizopata kuanzia ngazi ya kitongoji cha Cha’gombe kanda ya Temeke hadi taifa.

Wakati huo huo, Lundega alisema kuwa anatarajia kukutana na wajumbe wenzake ili kujadili suala hilo na kutoa uamuzi
 
Mhmm!! Wabongo huwa hatuna tabia ya kusoma mikataba, hata mawaziri wetu nadhani huwa hawasomi piaa. Pole Binti.
 
shule nayo inasaidia
kama alijua yeye mlokole alienda kufanya nini?

ingefaa zaidi akaadabishwa!!!
 
Yeye ni mlokole kulingana na kauli yake,labda atakemea kwa jina la Yesu ile kamati isimnyang'anye hayo mataji.Atakemea mapepo yote.
Huyu binti alijichanganya mno kwa kuachia taji la Reds,ukila ng'ombe mzima,malizia kabisa hadi mkia,kwato na mapembe yote.
Imani hiyo ilikuja baada ya taji la reds?aibu huko makanisani
 
Duh, kama ni wazazi ndio waliomshurutisha mbona itamuuma sana. Wawe wanafikiri kwanza kabla ya kutenda!
 
Uamuzi wa maana sana.
Ni vuziri unapofanya kitu ujiulize kwa nini utafanya na kitakusaidia nini.
Angella alitakiwa kusoma na kuelewa mkataba wa hayo mashindano ya umiss.
Big up kamati chini ya Lundenga.
 
Angella kuvuliwa mataji yote?!!

Ni baada ya kukiuka mkataba wa kurudisha taji la balozi wa Redds alilotunukiwa katika fainali za kumsaka mrembo wa Tanzania 2008 ndani ya viwanja vya Leaders club

Habari zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam zinasema kuwa Angela ambaye pia anashikilia taji la Miss Temeke 2008 na lile la Chang’ombe 2008 anashutumiwa kukiuka makubaliano baina yake na Kamati ya Miss Tanzania.

Inaelezwa kuwa kabla ya kushiriki shindano la Miss Tanzania, Kamati ya shindano hilo chini ya Mkurugenzi wake Hashim Lundenga, huwa inawakabidhi warembo wote mkataba na kukaa nao kwa siku moja ili wausome na kuuelewa, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wazazi au walezi wao na ndipo wausaini.

Katika mkataba huo kipengele kinachosema kuwa mrembo yoyote ni lazima akubali kufanya kazi zozote za wadhamini wa shindano hilo, ilimradi tu kamati ya Miss Tanzania iridhie.

Angela, akiwa kama mmoja wa warembo waliowania taji la Miss Tanzania mwaka huu, pia alisaini mkataba huo kabla ya kuanza kambi. Mbali na hilo mrembo huyo alishiriki katika shindano la kumtafuta Balozi wa
Redd’s lililofanyika mkoani Mwanza.

“Atalazimika kuvua mataji yote, kanuni ni zile zile toka ngazi ya kitongoji, kanda hadi taifa, mtu huwezi kuvua Blauzi ukabaki na sketi, akitaka kuvua nguo, ni lazima avue zote, sio moja,” alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Miss tanzania. Endapo atavuliwa mataji yote, Angela atatakiwa kurudisha zawadi zote alizopata kuanzia ngazi ya kitongoji cha Cha’gombe kanda ya Temeke hadi taifa.

Wakati huo huo, Lundega alisema kuwa anatarajia kukutana na wajumbe wenzake ili kujadili suala hilo na kutoa uamuzi

huyu mjumbe inaonyesha ni mzoefu wa kuwavua nguo mabinti zetu,angetumia neno lingine,isiwe haya ndio yaliomkimbiza angela?
 
Wrong choice of words,hivi pale miss tanzania hamna mtu wa public relations? kwa tuhuma na hisia mbaya walizo nazo watu, matumizi ya maneno kama haya yanazidi kuharibu
 
Back
Top Bottom