Angalizo: Usitafute mchumba kanisani

Ushauri mwema Heko!
 
Inategemea kupata mke mwema unaweza kumpata sehemu yoyote.
Inaweza kuwa kanisani au la!

Tatizo watu wakimuona mtu anakwenda kanisani wanakuja na fallacy of generalizations kwamba huyo mtu nimtakatifu.

Unahitaji kujitahidi kumjua mke unaetaka kumuoa vyema ndio sababu ya kupewa akili na utashi havikutolewa kwa bahati mbaya.

Naona makanisa ya Kiroho huwa kunakosekana ukaribu wa wachumba kuna katabia kakupenda kuuziana mbuzi kwenye gunia na baadae yanaanza majuto na yakianza majuto ukienda kwa mchungaji anakwambia hilo ni jaribu lako.

Sema tu ndoa nyingi za siku hizi zina matatizo ambayo kiroho tunaita majaribu ila mtaani tunaita matatizo.

Akili na utashi ni lazima vitumike sawasawa ukitumia vionjo na akili ya mchungaji lazima ulizwe.

Shida inakuja mke unaetaka kumuoa hamsali pamoja inakua ni ngumu kukubaliwa hata awe yuko vizuri vipi.

Hili linasababisha limited choice na mtu kumuomba Mungu amuonyeshe mke ila anampangia Mungu tena huyo mke lazima awe ameokoka na wanasali wote.

Mungu hapangiwi huenda mke mnaeendana nae ni kahaba na unapaswa kumbadili lakini wewe umeng'ang'ana lazima mkeo atoke kanisani unaposali ndio mchungaji akubali.
 
Mkuu, umenikumbusha enzi ya miaka ya 90 katika sherehe za Idd Pemba na Unguja, tulishauriwa si vema kumtongoza msichana ukimkuta kwenye viwanja vya sherehe. Eti anakuwa na uzuri wa dukani.
 
Hata ' bar ' mkuu????
 
Wanaotafuta wachumba kanisani ni madomo zege au wapenda kitonga au na wao ni disgraces, yaani waliochokwa na jamii kwahiyo wanakimbilia church.
 
Makanisa ya kilokolee ndo usime, one day nimeenda kwenye moja wapo ya hilo kanisa.
Aiseee acha kabisa kumbe wanawake na waume wanaosali pale 70% wana matatizo makubwa mengine ayafai kusimulia.
 
Yes hata Bar kuna watu walikutana na wake zao bar na wanaishi kwa amani.
Kikubwa kuendana na mke unaemuoa hata umtoe wapi kama hamuendani litakua ni tatizo tu
Pia tambua kuna ' mme ' na mwaume vile vile ' mke ' na mwanamke.
 
nadhani hujamuelewa sawia mleta mada
 
Safi sana. Maanake naona maadui wa kanisa wanajitahidi kupotosha.
 
Kweli kabisa, hii ni furahisha genge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…