Uchaguzi 2020 Angalizo Uchaguzi wa Mwaka huu; NEC/ZEC msicheze na sanduku la kura ni 'Bomu'

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Kwa hali ilivyo uchaguzi wa mwaka huu wa Oktoba ni kama bomu linalosubiri kulipuka, usipoendeshwa kwa tahadhari Tanzania inaweza kuandika historia mpya.

Navikumbusha Vyombo vya Dola, Msajili wa vyama, Tume ya Uchaguzi ya Taifa NEC na viongozi wote wa vyama vya siasa na serikali kuepuka maneno na viashiria vyovyote vinavyoweza kuonyesha upendeleo kwa chama au mgombea fulani.

Naziasa hasa NEC na ZEC kutumia busara ya hali ya juu yaacheni maamuzi ya wapiga kura yaheshimiwe, kitendo chochote cha upendeleo kama kilichofanywa na Jecha 2015 kinaweza kusababisha historia ya nchi yetu kuandikwa upya.

Wagombea wa safari hii na wapiga kura wao wako serious na maisha yao kama nyie mlivyo serious na kazi zenu.

Please, NEC/ZEC, Don't temper with the ballot box, handle with care it's an explosive device.
 
Mkuu, kwa maoni yangu itakua kama juzi kama jana. Hakuna kitakachobadilika, hakuna kitakachofanywa, hakuna kitakachotokea, hakuna atayeleta resistance, HAKUNA

Itakua ile slogan maarufu ambayo huzungumzwa hadharani tena mchana kweupee
"Tunachukua, tunaweka, waaaa". Shika sana hili neno la mwanzo, tena kotekote, Bara na Visiwani
 
Mimi nimetoa angalizo tu, siku ya siku ikifika nitakukumbusha uzi huu.
 
Safari hii wajaribu kuingiza mabox yao kwa kutumia police pia wajaribu kuzuia mawakala wa CDM hadi saa nne tano ili wafanye yao...

Hatumwi mtu sokoni...!! CCM Weka ugoko CDM weka chuma..dadadeq...hutaki futa uchaguzi tujue moja kama Somalia vile.
 
CCM wanategemea wafunge bao la mkono, ni hapo tu ndio panawapa matumaini hakuna kingine.
 
Wapinzani mkijipanga, mkaweza kumalizana/kudhibiti makundi ya CCM ya kuhujumu uchaguzi kila jimbo, mtafanikiwa kushinda, kinyume na hapo, sahau ushindi.

Tena anzeni siku 2 kabla ya uchaguzi, watafuteni waambieni ukweli kuwa ni ama zao ama zenu. Msitanie maana sio wengi ila wana kinga kubwa, hivyo msiwapeleke popote hamtafanikiwa, malizaneni tu
 
Kwa hali ilivyo uchaguzi wa mwaka huu wa Oktoba ni kama bomu linalosubiri kulipuka, usipoendeshwa kwa tahadhari Tanzania inaweza kuandika historia mpya.

Navikumbusha Vyombo vya Dola, Msajili wa vyama, Tume ya Uchaguzi ya Taifa NEC na viongozi wote wa vyama vya siasa na serikali kuepuka maneno na viashiria vyovyote vinavyoweza kuonyesha upendeleo kwa chama au mgombea fulani.

Naziasa hasa NEC na ZEC kutumia busara ya hali ya juu yaacheni maamuzi ya wapiga kura yaheshimiwe, kitendo chochote cha upendeleo kama kilichofanywa na Jecha 2015 kinaweza kusababisha historia ya nchi yetu kuandikwa upya.

Wagombea wa safari hii na wapiga kura wao wako serious na maisha yao kama nyie mlivyo serious na kazi zenu.

Please, NEC/ZEC, Don't temper with the ballot box, handle with care it's an explosive device.
Wapinzani tunajua hamna jeshi la kupambana na sisi.
Isitoshe urais wa zanzibar kwa mara ya kwanza haukupatikana kwenye sanduku la kura hivyo msitegemee tutawapa nchi kupitia sanduku la kura, kama mna ubavu tunisheni misuli yenu kama hamuwezi tulieni tuliiiiii kama maji mtungini.

Magufuli baba lao
Ccm oyeeeèeee

Chadema juu zaidi
Lisu ni yeyeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom