Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,456
- 872,092
walengwa watanielewa vema
Kila kitu kina mbadala wake kwahiyo hata kwenye hili isionekane ni jambo la ajabu sana
Kuna tiba za kizungu na Kuna tiba za kikwetu ambazo hutatua matatizo na mambo yaliyoshindikana kupata ufumbuzi kwa njia zilizozoeleka
Jamii imeumizwa sana na matatizo ya jinsi hii na imeumizwa kweli...
ni kutokana na uhitaji mkubwa wa tiba mbadala na kutatua matatizo kwa njia mbadala limejitokeza kundi ambalo aidha lina uwezo mdogo au halina kabisa bali hudanganya na kuwaibia wahitaji...watu wa hili kundi ni wengi sana
Ushauri wangu ni huu; epuka kabisa kushiriaka na mtu wa namna hii, anayetaka pesa mbele hata kwa kigezo cha pesa ya vifaa....unaweza kumpa kwakuwa una uhitaji na mazingira anayokujengea lakini ni vema kuwa makini sana
Epuka kusimulia mkasa mzima mwache kwa uwezo wake wa kiganga ayatambue matatizo na masahibu yako na mwisho wa siku afanye kazi atatue tatizo malipo yaje mwisho
Muhimu zaidi! Epuka tiba yoyote yenye kuhusisha damu hasa ya mnyama mkubwa kama mbuzi, unatengeneza maagano yatakayokuja kukugharimu sana, hizi ni tiba zenye side effects