Angalizo kwa wana-chadema: Kamwe tusibweteke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalizo kwa wana-chadema: Kamwe tusibweteke

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Oct 4, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama kuna jambo kubwa ambalo Watanzania wengi limewaathiri kifikra ni utawala wa CCM. Monopolization chini ya CCM imewafanya watu wengi ndani ya Taifa hili kuwa na fikra tegemezi, kukosa muda wa kutafakari mara mbili, kuwa wepesi wa kuhukumu na kukubali kuishi kwa mazoea.

  Jambo hili bado limewaathiri hata wana-mageuzi nchini, wana-CHADEMA, baadhi ya wana-CDM wamekuwa wepesi kutekwa fikra zao, wepesi kuhukumu na kukubali kurudi kule ambako NCCR ya Mrema ilipotea.

  Wanafikiri kuwa na fikra na mitazamo tofauti ndani ya chama ni chanzo cha vurugu na misuguano. Wameshindwa kutafsiri maana halisi ya migogoro na kuhisi kwamba wako mstari wa mbele kuepusha migogoro na kusahau kwamba wanajenga migogoro, wamelewa na mafanikio ya ghafla.

  Wengi wanahisi kwamba wanaweza kuishi na kudumu nje ya demokrasia bila kuweka utaratibu wa kidemokrasia. Wamekataa kuishi kwa kudadisi bali wamekubali kuishi kwa kuhisi. Wamekataa kupima afya ya fikra zao na kutumia propaganda na maneno rahisi kuhalalisha agenda zao.Hatuwezi kamwe kufika kwa mtindo huu.

  Lazima kwanza wajifunze kuwekeza kwenye siasa za akili na maarifa na hivi ndivyo chama chenye demokrasia pevu hufanya. Ukikataa njia ya majadiliano chini ya hoja kinzani ni kuhalalisha udhaifu na uwezo mdogo wa kifikra.

  Zipo tofauti kubwa za kimtazamo na kifikra kati ya Mbowe, Dr.Slaa na Zitto lakini tofauti hizi haziwezi kuwa na athari iwapo zinafuata misingi na kanuni za chama. Leo ukiongelea kuhusu Zitto watasema umetumwa, ukitoa mapendekezo Dr. Slaa agombee uenyekiti wa chama watasema umetumwa, je nani ambaye atazungumza kuhusu Zitto na watasema hajatumwa.

  Zitto ni Naibu Katibu Mkuu wa chama, nilitegemea wakati wa matukio makubwa ya chama Mwenyekiti wa chama angewaeleza wana-mageuzi kwa nini Zitto hayupo lakini hili halifanyiki. Ni wangapi waliwahi kuhoji ni kwa nini? Au tumeridhika na jibu rahisi ni MSALITI. Rejea NCCR ya Mrema na tafakari tafsiri halisi ya mgogoro. Hili ni tatizo. Na tatizo lipo ndani ya chama. Kama tumekataa hoja na na fikra kinzani kama moja ya kanuni za kidemokrasia basi tusitarajie kuishi kwa muda mrefu ndani ya ulingo wa siasa za kiushindani.

  Kamwe wana-CDM tusibweteke na mafanikio ya sasa, bado tuna kazi kubwa ya kujenga chama. Mabadiliko ndani ya chama ni Muhimu.
   
 2. b

  bariadi2015 Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 26, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli mabadiliko ndani ya chama ni muhimu,lakini tunabadili nini na kwamaufaa gani????sio kila mabadiliko yanamafanikio, na ukiona watu wanapiga kelele ujue wameona,for the issue of zitto kabwe,sisuport chochote kuhusu huyu jamaa maana tayari tunajua katumika kiasi gani na mafisadi na mpaka wamampigia debe kelele zake za kutaka uongozi wa juu sababu atawabeba na hatawawajibisha.sie sio vipofu na tunajua kiala mtu ana mapungufu yake,lakini sio kila pungufu linaathari ispokuwa lile linalo haribu mifumo na kuleta uhusiano mbaya kwenye jamii yoyote.
  zitto alitaka sana awe kiongozi wa kambi rasim ya upinzani bungeni,na kuna baadhi ya magamba ambao walimsaport kwa hali na mali ili apate hiyo nafasi,watu kama kina rostam na wengine wengi ambao ni wezi wadhambiki na wafisadi wa mali za uma.hivi toka lini mwizi akakupa pesa pesa aliyoiba asitake something in return????????mabadilioko ni muhimu wakakti yanapohitajika tu,espacially kwenye chama chenye malengo ya kuchukua dola kama cdm.
   
 3. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Hilo darasa la tuition wafundishe familia yako, imeshindikana deal na mkeo na wanako. Mabadiriko gani unayoyataka yafanyike ndani ya chadema wewe? Wanafiki kujificha ni vigumu sana, gamba kuu wewe. Tuache tuendelee na mapambano ya kuchukua nchi 2015. Peoples power, M4C.
   
 4. L

  Lwesye JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 5,297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Zitto hasafishiki Mbelwa unataka viongozi wenzake waanze kumuombea ruhusa kwa wananchi wakati yeye mwenyewe anaratiba ya kazi na ni sehemu ya watu wanaopanga mipango kazi ,kwa nini hashiriki shughuli za kujenga chama basi kama anaona kuna muhimu
  Halafu lugha za kuchanganya mawazo ya wananchi kwa nini yeye hupenda kuzitumia pale anapoona kuna mjadala mkubwa wa kitu fulani katika jamii,utaanzaje kutaka uraisi wakati unajua agenda ya chama chako ni kuendeleza vuguvugu la mabadiriko nadhani wewe unataka kumukweza mtu ambaye yeye mwenyewe amejiona kashindwa kuhimili kasi ya chama chake
   
 5. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jenga hoja,nadhani umekuwa mbogo na kushindwa kutoa argument zenye mashiko, tunapozungumzia mabadiliko hakuna maana kubadilisha viongozi tu bali tunalenga katika kujitathmini kimuundo, kisera na kimkakati, bado kurugenzi ndani ya chama hazifanyi kazi kwa ufanisi, labda nikuulize swali, unajua kuna kurugenzi ngapi ndani ya CDM,umekuwa mfuasi bila kujua CDM vizuri, bado kuna changamoto ya kutoa mafunzo kwa viongozi wa ngazi za chama wa chini, lazima tujenge ethics za vijana ndani ya chama, lazima kuboresha kanuni imara za kusimamia chaguzi za ndani za chama,tumeona haya kwenye uchaguzi wa BAVICHA tusiwe washabiki tu, kijana yoyote mtanashati wa akili anapaswa kutoa fikra chanya ambazo zitasaidia kujenga chama.
   
 6. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,164
  Likes Received: 10,511
  Trophy Points: 280
  Kwasasa mm sijui cha mabadiliko ya kimuundo, sujui uchafu gani, sijui nn....nachoelewa sasa hivi ni M4C only...
   
 7. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  "swala langu hapa ni udhaifu wa baraza la wanawake chadema (bawacha) sijui wanafaida gani ndani ya chadema au ni kwa ajili ya ubunge wa viti maalumu hili ni lazima uongozi wa c.d.m ulifanyie kazi au kuuondoa uongozi wote kwa maslah mapana ya chadema bila kuangaliana usoni kwani wapigakura wengi wa tanzania ni wanawake.

  tunahitaji bawacha isimame kama baraza ndani ya c.d.m lifanye kazi ya kuwaunganisha wanawake wawe na mwamko wa kuiunga mkono cdm.mwanamke akiwezeshwa anaweza viongozi chadema liangalieni hili kwa maslah ya chama". Na Mayage

  Ndugu zangu wale wasioona haja ya mabadiliko hili ni moja ya mabadiliko ninayozungumzia. Kamwe tusibweteke...
   
 8. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Fikra tulivu huzaa hoja makini..tafakari upya, changamoto ndio kieelelezo cha imani kubwa ya kifikra kukabiliana na mahitaji ya nyakati
   
 9. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,164
  Likes Received: 10,511
  Trophy Points: 280
  Sasa ulishindwa nn kuwa straight kuanzia mwanzo wa thread yako....Mara oh Zitto, Mbowe sijui Dr. Slaa...
   
 10. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Soma kwa kuelewa sio kwa kukariri, kamwe usikubali kuishi na hisia bila kutambua uhalisia...
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu nakusoma vizuri sana na hakika umenigusa sana. Kuna kirusi kimeingia ndani ya chama ambacho kinaitwa UMAARUFU wa MUDA na kwa bahati mbaya umekuwa mtaji mkubwa kwa baadhi viongozi na wanachama wa Chadema. Hili huhitaji kulitazama upande mmoja ukiwa ndani isipokuwa kujitoa pembeni ukalitazama kwa makini ili upate kuona athari zake..

  Swala la Mbowe, Zitto na Dr.Slaa ni habari inayotokana na Umaarufu wa Muda kiasi kwamba ni kawaida ya watanzania kusahau walipotoka. Haiwezekani watu wale wale waliokuwa wakipatana miaka 10 niliyopita wakaweza kukisimamisha chama leo hii kila mmoja wao anajituma yeye na kujenga kambi yake ili mradi Upinzani wenyewe haujawa na nguvu ya ushiwishi mkubwa ili kufikia ushindi mwaka 2015.

  Tofauti zao hazitokani na lolote zaidi ya kugombea nafasi za juu ktk Uongozi. Vyama vingi ktk nchi maskini vimeshindwa ushindani ktk demokrasia kutokana na tabia mbaya ya ushindani wa WATU ndani ya chama. Majungu, Ulafi, Unafiki na Majigambo hudhoofisha nguvu ya umoja pale ambapo demokrasia inapotafsiriwa kama haki ya Mgombea badala ya haki ya wananchi kumchagua kiongozi wao na wadhungu wanasema - Democracy is a means for the people to choose their leaders and to hold their leaders accountable for their policies and their conduct in office.

  Ni muhimu sana viongozi na wanachama wafahamu hili na kwamba haki ya mtu kugombea ni kipengele ndani ya hoja nzima ya demokrasia. Na isije tafsirika vibaya ya kwamba tunaweza kuisimamisha demokrasia ya kweli ndani ya vyama.. Hii sio kweli hata kidogo isipokuwa ndani ya vyama kuna sheria na kanuni zake na ni lazima viende sabamba as to say, the laws and procedures apply equally to all members.

  Nimesema demokrasia ndani ya vyama haiwezi kusimama kama tunavyotaka, ni kutokana na kwamba ili demokrasia ya kweli isimame kuna utaratibu wake na nitatoa mifano miwili mitatu.. Kwanza, ni lazima uchaguzi usimamiwe na chombo huru kinachojitegemea -.For a Democracy to stand, elections must be free and fair, they have to be administered by a neutral, fair, and professional body that treats all political parties and candidates equally.

  Pili, wananchi wanatakiwa kupiga kura zao kwa siri pasipo vitisho ama fujo -Voters must be able to vote in secret, free of intimidation and violence. Na tatu lazima kuwepo na Independent Observer..

  Sasa ukitazama yote haya ni mambo ambayo hayawezekani ktk uchaguzi ndani ya chama na watu wengi sana wanapenda kutumia hili neno Demokrasia hata ktk chaguzi ndani ya vyama pasipo kuelewa misingi yake.. Demokrasia inawezekana tu ktk ngazi ya ushindani wa VYAMA. Demokrasia inatokana na ushindani wa Itikadi,hivyo kinachoshindana ni SERA za vyama viwili vinavyopingana ktk ngazi za majimbo hadi Kitaifa na sio ushindani wa Mbowe, Zitto au Dr.Slaa ktk uongozi wa chama au kugombea Urais. Ikiwa kuna tofauti kubwa za kimtazamo na kifikra baina ya viongozi hawa basi ni bora wao wenyewe warudi shule ya SIASA wajipange upya ili wapate kujua where they belong!...

  Inasikitisha sana kuona viongozi na wanachama wanakubaliana ktk Itikadi na sera lakini wanagombana ktk ushandani wa nani awe kiongozi au mwakilishi wa chama. Hata hatua hiyo sii kazi yao isipokuwa wanachama ndio watamchagua mgombea ndio wenye haki ya kuchagua na sii haki ya mtu binafsi ambayo inapingana na sheria ama kanuni za chama. Sheria na kanuni zipo kuwalinda watu wote na hivyo haiwezekani sheria na kanuni ikabadilishwa kwa sababu ya kumwezesha mtu mmoja.

  Na wala sioni sababu kabisa ya Mwenyekiti kusimama na kuwaelezea wana mageuzi kwa nini Zitto hakufika ikiwa Zitto hakuwa mgeni rasmi ama alotarajiwa kuendesha matukio hayo. Unafiki unaoendeshwa na baadhi ya kuendeleza mgogoro ambao hauna maana kabisa kwa chama isipokuwa kuwagawa zaidi ndio sababu ya mwendelezo wa mahusiano mabaya baina ya viongozi. Unapojiunga na chama hukuingia kutafuta marafiki wala maelewano isipokuwa unaunga mkono itikadi na sera za chama hivyo nafasi yoyote utakayohitajiwa utakuwa tayari kukitumikia chama. Kuna nchi Mwenyekiti wa Chama na Sektrarieti yake huchaguliwa ama kupendekezwa na mgombea Urais yaani uongozi wa chama hutokana na mtu atakaye simama kugombea Urais. Hakuna cha demokrasia wala haki ya mtu..Je tungeyaweza haya?..
   
 12. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu, ipo mitazamo hasi ambayo inajengeka ndani ya chama ambayo inahitaji ufafanuzi, mara nyingi watu wanahoji ni kwa nini kombinesheni ya Zitto na viongozi wengine wa juu wa chama haionekani? Kila chama kina itifaki ambayo hutoa itiririko wa nafasi katika chama,hivyo tuna changamoto ya kujenga kombinesheni imara without individualism ambayo itaonyesha tunasimamia itikadi na sera moja na tunasimamia kwa pamoja mabadiliko na kubeba jukumu la kuyatafsiri mabadiliko yenyewe.

  Wakati wa M4C ya mara ya mwisho Jangwani wengi waliuliza Zitto yuko wapi. Lakini kulikuwa na tetesi yupo Marekani akifungua matawi ya chama, kulikuwa na kosa gani kutambua jukumu ambalo ni kwa manufaa ya chama. Tukumbuke huyu ni NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lakini kwa nini watu wajiulize hivyo ikiwa hawajajenga fikra mbovu vichwani. Hivi kweli leo JK yupo canada kuna mtu anataka kujua Mukama, Pinda au Msekwa wako wapi?..Kwa nini tunapenda kujiuliza maswali ambayo yanazidi kujenga utenganishi?..

  Mimi naikubali hoja yako sana tu isipokuwa hili swala la viongozi wetu kutokuwa na Umoja ktk kukijenga chama kutokana na tofauti zao binafsi linanipa wasiwasi zaidi maana haya yote ni matokeo mabaya ya Ushirikiano wao mawasiliano. Mwaka 2005 hatukufikia kujiuliza hivyo na wala haikuwa issue kabisa lakini baada ya Chadema kupanda nafasi ya pili chama rasmi cha pinzani, sasa ndio tunaziona sura kamili za viongozi wetu..

  Jamani mwee Chadema haiwezi kuendeshwa na mtu mmoja mmoja au kutegemea nguvu ya Mbowe, Zitto au Dr.Slaa hawa wote wamepikwa ndani ya chama na inasikitisha sana, watu kama siye tulojiunga kutokana na chama kutupa msukumo wa tumaini jipya leo tunakuja aminishwa kuwa chama kina wenyewe. Chama hakiwezi kuweka mtaji wake kwa WATU fulani na hili ndilo lilowaangusha NCCR akiondoka mtu mmoja tu chama kinavurugika. Binafsi sijali kama Mbowe ni Mwenyekiti au Zitto ni naibu katibu they work for us, ni wanachama ndio walowachagua kushika nafasi hizo - They serve people sio nafasi ya kujineemesha wao! =
  80 percent of problems are often due to 20 percent of the causes
  [​IMG]
   
 14. M

  Makyomwango JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa hili nakuunga mkono, ki ukweli baraza hili ni kama halipo nami nashauri livunjwe ili liundwe upya. Kama kuna mtu anaweza kutuwekea janvini M'kiti, katibu na sekretarieti ya baraza hili afnye hivyo ili tuweze kuwachambua vizuri kwamba hawafanyi kazi kama M4c inavyotaka
   
Loading...