Angalizo kwa CHADEMA juu ya Jimbo la Kigoma Kusini!

Heading ya Magazeti siku moja Baada ya Uchaguzi jimbo la Kigoma Kusini:
1.CCM yaibuka Kidedea tena Kigoma kusini
2.Chadema Kuandamana Nchi nzima kupinga Matokeo ya Uchaguzi mdogo Kigoma Kusini
3.Dr Slaa aionya NEC,asema taratibu zimekiukwa Uchaguzi mdogo Kigoma Kusini
4. CCM watumia Bilioni 3 Uchaguzi mdogo kigoma Kusini,Mbowe,Slaa wamtupia lawama Zitto wasema Mchango wake kuipigania Chadema ulikua mdogo
5.CCM haikamatiki yarudisha jimbo la Kigoma Kusini
6. Dr Slaa alalama asema Kulikua na Uchakachuaji mkubwa jimbo la Kigoma Kusini,Kamati Kuu ya CDM kukutana wiki ijayo kutangaza maandamano Nchi nzima bila kikomo!

Ongeza na:
No. 7 Kada wa Chama na kiongozi wa kampeni afumaniwa na mke wa mtu kwa mara nyingine tena
 
yaani kafulila aombe radhi CDM kwa sababu alisema ukweli? acheni kutisha watu bwana.......kusimamia haki Tanzania ni kazi sana si CCM si upinzani!
Mlimponza aende NCCR kwa kisingizio cha demokrasia ndani ya CDM, mmefanya apoteze ubunge kwa tamaa na mbinu zenu za kijinga, bado mnaendelea kumfuata kumdanganya tena, Kafulila ndugu yangu this time changanya na zako hii Zittos' group hatari achana nayo, ni hawa hawa walimponza Machage hadi akaenguliwa uchaguzi wa m/kiti Bavicha.
 
Sio lazima kafulila arudi chadema, kumbuka alivyoondoka kwa dharau na kiburi, mi napendekeza kafulila kama anaipenda chadema kweli aombe radhi cdm na cdm isimpe nafasi yoyote ya uongozi kwa sasa, impe nafasi ya kuwa mwanachama tu.
Kafulila toka amekuwa mbunge umaarufu wake jimboni umekuwa ukiporomoka kwa kasi sana kwani muda wote alikuwa akipanga mikakati yao na zitto, nimeongea na wafanyabiashara wengi tu wanao tokeo jimboni kwake na walinieleza kuwa kafulila amewabadilikia.
Pia cdm ina hazina kubwa ya watu wenye uwezo wakutosha kugombea huo ubunge na sio lazima tumtumie huyo kafulila au huyo mgombea wa mwaka jana, kwanza kwa kufanya hivyo tutakuwa tunampa kichwa zaidi na hakika hataacha tabia zake uasi, bila kupata adhabu kidogo hatojifunza.

Au nawewe unataka kugombea kupitia CDM ndoo maana hutaki Kafulila akaribishwe CDM??? ,,, mhhhhh siasa za TZ kiujumla zinachosha.
 
Mambo yote haya ni tamaa ya madaraka, ubinafsi na ukosefu wa akili. Niliwahi kuandika kwamba Kafulila anasumbuliwa na utoto au siasa za makundi, Zitto ni mwana CDM mwenzangu, kijana na ninampenda sana, ila amemponza Kafulila tangia akiwa CDM, Tabia za kutokufuata katiba na taratibu za chama si uungwana. Mbinu hawa jamaa wanazofanya za kulazimisha mtandao wa kisiasa kwa ndoto za kuingia Ikulu zitawagharimu wote.

Demokrasia inamruhusu Kafulila kujiunga na chama chochote cha siasa. Angalizo kama Kafulila alishindwa kuelewana na viongozi wa CDM akiwa afisa mdogo wa chama kweli kunauelewano akiwa mbunge kupitia CDM? Nakubali ajiunge na CDM ila wasimpitishe kuwa mgombea wa Ubunge kupitia CDM kwani chama kinamjua na tabia zake hawezi badilika, muda wa migogoro hakuna tena wananchi wanataka kazi. Zito wewe ulimponza kafulila sasa imekula kwake mshauri na mweleze kupanda ngazi inahitaji uvumilivu, huwezi kupiga ncha ya mkuki konzi. Chama makini kinajengwa na watu makini.

No Kafulila kugombea Ubunge kupitia CDM. Hatutaki migogoro na waroho wa madaraka.
 
C O U G H bwana wanafurahisha. Ila namsikitikia tu huyu bwana mdogo MTATIRO aliyeamua kujiunga na MMEMKWA.
 
Aombe samahani na agombee via Cdm ila wampe masharti ya kutogombea kitu chochote mbali na hyo ya ubunge na wamkabidhi kwa Prof Baregu amtengeneze
 
kafulila tuliza kichwa.usibweteke.ukirudi cdm umejimaliza kisiasa,watakupokea halafu hawakuteui kugombea,ili kukuangalia kama umejirekebisha.jnia pekee ni kukata rufaa wakati unajipanga na kupima upepo wa kisiasa ni wapi uende pasi na kuharibikiwa.
 
Kigoma hawaitaji chakula cha msaada, sijui magamba watawapa nini?

Kafulila rundi kundini, kujuta na kuomba msamaha ni jambo la kawaida kwa binadamu! Fikra zako na za wananchi wako haziko compatible na rangi ya yellow na kijani!
 
Mambo yote haya ni tamaa ya madaraka, ubinafsi na ukosefu wa akili. Niliwahi kuandika kwamba Kafulila anasumbuliwa na utoto au siasa za makundi, Zitto ni mwana CDM mwenzangu, kijana na ninampenda sana, ila amemponza Kafulila tangia akiwa CDM, Tabia za kutokufuata katiba na taratibu za chama si uungwana. Mbinu hawa jamaa wanazofanya za kulazimisha mtandao wa kisiasa kwa ndoto za kuingia Ikulu zitawagharimu wote.

Demokrasia inamruhusu Kafulila kujiunga na chama chochote cha siasa. Angalizo kama Kafulila alishindwa kuelewana na viongozi wa CDM akiwa afisa mdogo wa chama kweli kunauelewano akiwa mbunge kupitia CDM? Nakubali ajiunge na CDM ila wasimpitishe kuwa mgombea wa Ubunge kupitia CDM kwani chama kinamjua na tabia zake hawezi badilika, muda wa migogoro hakuna tena wananchi wanataka kazi. Zito wewe ulimponza kafulila sasa imekula kwake mshauri na mweleze kupanda ngazi inahitaji uvumilivu, huwezi kupiga ncha ya mkuki konzi. Chama makini kinajengwa na watu makini.

No Kafulila kugombea Ubunge kupitia CDM. Hatutaki migogoro na waroho wa madaraka.
Mkuu ni vizuri sana mkatofautisha uongozi ndani ya chama na mbunge mwakilishi wa wananchi wa jimbo lake. Kafulila anaweza kuwa mwanachama wa CDM lakini sio lazima awe kiongozi wa chama na swala hili linatakiwa sana kutazamwa upya ndani ya vyama vyote vya Upinzani maana inaonyesha wazi vyama hivi pasipo kuwatumia viongozi wa chama kugombea majimbo basi chama hakina watu. Mbona CCM sekretaiet yake karibu yote hawana mamlaka ndani ya serikali.?...

Tuseme kesho Chadema wamechukua nchi nani watakuwa viongozi wake kama sio hawa hawa wabunge na viongozi wa chama?. Sekretariet nzima ndio itashika uongozi wa juu wa serikali na vivyo hivyo vyama vingine vyote. Sasa unajiuliza ni wakati gani huyu mtu mmoja anaweza kuwa kiongozi wa chama, Mbunge na waziri mtarajiwa?. Nadhani umefika wakati vyama hivi viweke masharti ukitaka kugombea nafasi ndani ya chama hutaweza kushiriki kugombea Ubunge ili kuwapa wengine nafasi kulitumikia Taifa..

Vyama vya Upinzani havijajipanga kuchukua nchi na hizi vurugu ndani ya chama ni dalili tosha kuonyesha kwamba kuna mkorogo..pia nafasi za utumishi ni chache sana hazikusambazwa ipaswavyo, hivyo kila mmoja wao anajua pasipo nafasi ndani ya chama huwezi kujijenga Kitaifa maana hakuna nafasi isipokuwa kwa kupitia uongozi wa chama. Huko CCM, huyo Mukama au Nape hana haja wala sababu ya kugombea Ubunge wala kuchaguliwa kuwa waziri au balozi anatumikia kazi za chama tu..lakini nenda vyama vya Upinzani Seif Hamad ndiye Katibu wa chama Kitaifa, ndiye makamu wa rais wa Zanzibar na pengine ndiye mwenyekiti wa CUF Zanzibar..Huyu mtu mmoja!
 
kafulila tuliza kichwa.usibweteke.ukirudi cdm umejimaliza kisiasa,watakupokea halafu hawakuteui kugombea,ili kukuangalia kama umejirekebisha.jnia pekee ni kukata rufaa wakati unajipanga na kupima upepo wa kisiasa ni wapi uende pasi na kuharibikiwa.
 
Nakubaliana nawe asilimia mia moja,tuachane na Mashibuda,hakuna haja ya kuchukua left overs
 
Mambo yote haya ni tamaa ya madaraka, ubinafsi na ukosefu wa akili. Niliwahi kuandika kwamba Kafulila anasumbuliwa na utoto au siasa za makundi, Zitto ni mwana CDM mwenzangu, kijana na ninampenda sana, ila amemponza Kafulila tangia akiwa CDM, Tabia za kutokufuata katiba na taratibu za chama si uungwana. Mbinu hawa jamaa wanazofanya za kulazimisha mtandao wa kisiasa kwa ndoto za kuingia Ikulu zitawagharimu wote.

Demokrasia inamruhusu Kafulila kujiunga na chama chochote cha siasa. Angalizo kama Kafulila alishindwa kuelewana na viongozi wa CDM akiwa afisa mdogo wa chama kweli kunauelewano akiwa mbunge kupitia CDM? Nakubali ajiunge na CDM ila wasimpitishe kuwa mgombea wa Ubunge kupitia CDM kwani chama kinamjua na tabia zake hawezi badilika, muda wa migogoro hakuna tena wananchi wanataka kazi. Zito wewe ulimponza kafulila sasa imekula kwake mshauri na mweleze kupanda ngazi inahitaji uvumilivu, huwezi kupiga ncha ya mkuki konzi. Chama makini kinajengwa na watu makini.

No Kafulila kugombea Ubunge kupitia CDM. Hatutaki migogoro na waroho wa madaraka.
Unataka kugombea wewe??? Hakuna mwnye hati miliki CDM kila mtu anayepinga Ufisadi anafaa kuungwa mkono ilimuladi hatumiwi na CCM
 
Nafikiri best option ni CDM kuliomba hilo jimbo either kupitia Kafulila au mtu mwingine; sasa wanajua who is who so watalichukua bila shida hilo linaenda Chadema bila shaka. Kafulila akirudi akapiga magoti kwa wazazi wake kama mwanampotevu will be good chadema kuonyesha maturity na hii itawapa credibility sana mbele ya safari kuwa wako kusimamia principle sio watu as character
 
Back
Top Bottom