Angalizo kwa CHADEMA juu ya Jimbo la Kigoma Kusini!

Kwa Tanzania watu wanapenda kuwatumikia wananch pale tu Posho zao na Malupulupu yanapoimarika.Angalia posho zilipanda kwa siri lakini hakuna Mbunge aliyefichua Ufisadi huo.Mpendazoi alijitoa CCM na kwenda CCJ WABUNGE WENGI WALIMSIKITIA KUKOSA mafao!Sasa humu ndani Watu wanamhurumia Kafulila kwa kukosa Posho na si nafasi ya kuwatetea watu ktk Ukweli.Kafulila kasema Mbatia ni Kibaraka wa CCM.sasa hapa kuna uongo?. Ni kweli kafukuzwa na mkweli na muongo hawakai pamoja.
 
CDM NI CHAMA KIKUU CHA UPINZANI LAKINI BILA KUWA NA NGUVU YA UMOJA NA VYAMA VINGINE HALI INAWEZA KUWA MBAYA.KULE IGUNGA BILA MPASUKO WA CCM CDM ISINGE SHINDA. Kuimarika CDM KUNATOKANA NA MPASUKO WA VYAMA VINGINE.
 
Kama Igunga, hapo CCM ipeleke majembe yake yote, Mwigulu, Nape, January na Lusinde aka kibajaji, jimbo linakwenda CCM.

Baada ya wizi wa igunga nasikia haya majembe yalipelekwa mwanza na badala ya kulima yaliishia kutoa matusi ya nguoni baada ya kuzidiwa na nguvu ya umma lol!
 
NCCR wanarudi katika zama zile za mvurugano wakati walikuwa wameanza kujijenga upya! wanaingia hasara kubwa kwa kufanikisha mkakati wa Mbatia, kumvua uenezi ilikuwa adhabu tosha kabisa
 
Mabilioni ya pesa inaenda kuteketezwa tena kwenye kajimbo kamoja tu! Masikini Tanzania yangu!
kwa mujibu wa Tendwa..uchaguzi mdogo hutumia bilion19 hadi 20 mbali na Vyama husika kutumia gharama zao! so ni zaidi ya billion 20 Mkuu!
 
Ushahidi kuwa Mbatia ni Kibaraka wa CCM umedhirika mda mfupi baada ya Kafulila kuvuliwa uanachama Vyombo vya habari vimeripoti Mbatia kapeleka barua kwa Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete kutaka kumuona kuhusu maoni ya NCCR juu ya katiba mpya.Hapo awali Kafulila alipinga kwenda Ikulu kwa suala hilohilo lakini Mbatia akamukemea.Japokuwa Viongozi wa dini akiwemo Pengo wamepinga mchakato huo kwa kuwa hawana imani na Serikali ya Kikwete Mbatia anasubiri kuitwa.Taarifa zinaonyesha kuwa CCM IMEANDAA vyama vya upinzani vinavyoitumikia viende ikulu ili kuua agenda ya upinzani wa CDM inayosambazwa kwa wananch.Tayari baada ya NCCR watafuata TLP,SAU,UPDP YA dovutwa, Tadea ya Chipaka,na kile cha Cheyo
 
If we get rid of snitch Zitto, mambo yote yatakua kwenye mstari. Kafulila aende PPT maendeleo, otherwiz akalime mawese! Ila Zitto simpendi, mnafiki!
 
CDM wataibuka kidedea Kigoma kusini hata bila ya Kafulila
Ni kweli kabisa CDM wanaweza kushinda bila Kafulila lakini kwenye Vita ni lazima ujihami sana kwani sheria zetu zinasema ukishindwa kwa kula moja bado umeshindwa sasa kwa nini kukataa kula ya Kafulila ambaye ni Mpinzani kama Chadema?.Suala la tofauti kimutizamo lipo kila mahali na ndio maana ya vyama vya upinzani?Vyama vingi vinatokana ni mitizamo mingi ya upinzani na sio mitizamo ya kuunga mkono CCM!Kule Kenya Kibaki na Odinga hawaelewani Kimutizamo lakini wote hawa ndio wameingusha KANU chama tawala ambacho kilikuwa na nguvu kuliko CCM.We angalia CCM pamoja na kumutukana Rostamu Aziz hawakuwa tayari kupoteza kura yake .Leo Mbatia katangaza kwenda kumuona JK kuhusu Katiba mbinu ni hiyo hiyo CCM inataka kuhifadhi kura zote za NCCR kigoma kusini.Kule Igunga kulikuwa na ndoa kati ya CCM na CUF lakini Kigoma kusini kuna ndoa ya NCCR na CCM!Kama ulimusikiliza Mh Agripina Buyogera ana sema yeye na Mbatia walizunguka sana na Mbatia huku Agripina akimutelekeza mume wake kuhakikisha majimbo yote yanakuwa NCCR ,lakini akaogopa kumalizia kuwa fedha za kuzungukia zilitoka CCM!!.Ukweli Mbatia ni Injinia wa Maji ,hafanyi kazi sasa alipata wapi fedha za kuzunguka na mke wa mtu wakati NCCR haina ruzuku na Mbatia hana Kazi??
 
Taarifa kutoka kwenye Kikao zinaonyesha kwamba Mh Agripina Na Moses Machali ndio waliopinga kabisa hoja ya Kafulila kubaki kwenye NCCR na mimi nawaunga mkono kwani kama Mbatia ni Kibaraka na Mkutano umepitisha Mbatia aendelee kuwa Mwenyekiti Basi Mkosamali na Kafulila walipaswa kurejesha kadi zao kwa Kuwa kubakia ni kuendelea kuwa Chini ya CCM wakati wao ni Wabunge wa Upinzani?Mimi natazamia Mkosamali aonyeshe ukomavu wa Kisiasa kama kweli atakuwa tayari kutii maagizo ya CCM hasa hili la kwenda kumuona rais Kikwete kuhusu Katiba?Ni bora Kafulila aliyefukuzwa kwa kuanda mkakakati wa kumutoa Kibara wa CCM kuliko kuendelea kumutumikia Kibaraka wa CCM huu ni ukolon Mamboleo!
 
Sio lazima kafulila arudi chadema, kumbuka alivyoondoka kwa dharau na kiburi, mi napendekeza kafulila kama anaipenda chadema kweli aombe radhi cdm na cdm isimpe nafasi yoyote ya uongozi kwa sasa, impe nafasi ya kuwa mwanachama tu.
Kafulila toka amekuwa mbunge umaarufu wake jimboni umekuwa ukiporomoka kwa kasi sana kwani muda wote alikuwa akipanga mikakati yao na zitto, nimeongea na wafanyabiashara wengi tu wanao tokeo jimboni kwake na walinieleza kuwa kafulila amewabadilikia.
Pia cdm ina hazina kubwa ya watu wenye uwezo wakutosha kugombea huo ubunge na sio lazima tumtumie huyo kafulila au huyo mgombea wa mwaka jana, kwanza kwa kufanya hivyo tutakuwa tunampa kichwa zaidi na hakika hataacha tabia zake uasi, bila kupata adhabu kidogo hatojifunza.

yaani kafulila aombe radhi CDM kwa sababu alisema ukweli? acheni kutisha watu bwana.......kusimamia haki Tanzania ni kazi sana si CCM si upinzani!
 
Mwenye matokeo yaliyopita kigoma kusini atupatie tuanze na tathmini

CCM------
CHADEMA____
NCCR______



CandidatePolitical PartyNumber of Votes Percentage Votes
KAFULILA DAVID ZACHARIANCCR-MAGEUZI23,16240.34
KIFU GULAMHUSSEIN SHABANICCM20,36735.47
MUSLIM HAIDERALI RAJABALICHADEMA7,67613.37
OPTATUS BEDA LIKWELILECUF3,4686.04
AZIZI HASSANI MOHAMEDCHAUSTA4910.86
FILIPO JOHN FUMBO DP3450.6
SELEMANI SAIDI MSANUJAHAZI ASILIA3100.54
MVANO RASHIDI RAMADHANINRA580.1
MWAJUMA MALIKI ATHUMANIUPDP570.1
MWITO JUMA KHAIRALLAHSAU570.1
ZABIBU MRISHO KALIZAUMD520.09
SPOILT VOTES1,3762.4
TOTALS57,419100

http://www.nec.go.tz/index.php?modu...n=9&district=67&const=239&ward=&button=Search
 
CDM NI CHAMA KIKUU CHA UPINZANI LAKINI BILA KUWA NA NGUVU YA UMOJA NA VYAMA VINGINE HALI INAWEZA KUWA MBAYA.KULE IGUNGA BILA MPASUKO WA CCM CDM ISINGE SHINDA. Kuimarika CDM KUNATOKANA NA MPASUKO WA VYAMA VINGINE.
Hivyo vyama vingine ni vipi hivyo unaweza taja hata kimoja.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom