Angalizo kwa CCM: Zoa zoa ya wapinzani ni kutengeneza bomu la atomic

waco1920

Member
Oct 20, 2020
14
33
Nimewiwa kutoa tahadhari kwa Chama tawala na pendwa! Cha CCM juu ya nguvu hii kubwa inayotumika kuwavuta ndani ya chama viongozi au wanachama wenye ushawishi kutoka katika Vyama vya upinzani. Kwa wakati huu, kwa sura moja tunaweza kuona Kuwa ndiyo njia pekee ya kutumia ili kuvidhoofisha au kuviua Vyama hivyo. Kwangu nasema HAPANA!

Nasema hivyo kutokana na historia ya Vyama vyenyewe! Hapa Tanzania tuna aina tofauti ya vyama kwa maana ya misingi na aina ya uendeshwaji wake. Vyama kama vya akina Shibuda, Cheyo, au Wazee wa ubwabwa, ukimnunua mmoja tu, basi na Chama kimekufa!

Lakini siyo kwa Chama kama CHADEMA ambacho ni taasisi kubwa na yenye mtandao mpana zaidi ambao akitoka mmoja kumi huibuka tena kwa nguvu na moto wa ajabu.

KWA NINI CCM INATENGENEZA BOMU! Nasema hivo kutokana na ukweli Kuwa hawa wanaoletwa kwa upepo wa kisulisuli hawana jipya wanalokuja nalo! Bali wanaonekana Kuja kubana nafasi hata zile chache za wale wafia Chama ambao wametembea nacho wakati za mvua na zile za kiangazi.

Kwa ujumla wanacheka kiunafiki na kuwapigia makofi ya kinafiki pale wapinzani wanaingizwa ndani ya Chama kwa kiki ya kuubomoa upinzani, hii hawakubaliani nayo hata kama hawasemi! Ila siku watakapopata jukwaa la kusemea, ndiyo wataanza kuchomana vidole machoni.

Natoa ANGALIZO tu ili siku itakapotokea, watunza kumbukumbu watauleta uzi huu kama rejeo!

NAOMBA TUWAKARIBISHE AKINA HALIMA MDEE NA KUNDI LAKE KATIKA CHAMA CHETU KAMA MASHUJAA LAKINI TUWEKE TAHADHALI!

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
 
Hatutengenezi bomu ila tunatimiza azma ya kufuta wakwamisha maendeleo
 
Mimi mwenyewe kesho narudi CCM, fursa zipo huko. Ukiwa na kadi ya CCM wewe maisha umeyapatia kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom