Angalia overtake ya gari ndogo kwenye highway

Angalia overtake ya gari ndogo kwenye highway

Mkuu
Unachosema Siyo Sahihi Hiyo Mistari Unavyoiona Barabarani Inamkataza Dereva Kulipita Gari Lililo Mbele Unaposema Ni Clear Siyo Kweli

Mleta Picha Anasema Ukweli Kuwa Wakati Mwingine Unaweza Kumlaumu Huyu Ukamwacha Yule

Hiyo Gari Ndogo Ina Kosa Ndiyo Maana Basi Limetanua Kuepusha Ajali Hapo

Your very right gentleman!
Unajua kusoma picha maana bus limetoka nje ya msitari kuepusha ajali
 
aisee....! madereva wenyewe ndio nyinyi kazi ipo
1.ame overtake sehemu isioruhusiwa.
2.hakuwa makini, maanake hilo bus limempisha angalia limetoka nje ya barabara kabisa.

Yeye ameona kuwa kuko"clear"sasa sijui hilo basi nalo lilikuwa clear au vipi.
 
Wengi tunaokutana nao Road ni watembeza Magari sio Madereva, kuna Dada yupo Ewura Aliwahi kuniambia amepata Leseni japo hajawahi walau ku sit kwenye Siti ya Dereva hata Mara moja kwenye Maisha yake. Trafick wawe wanafanya zoezi la kustukiza kutambua kama Madereva wanajua alama kuu za Usalama barabarani
 
Kitonga hiyo mkuu? naona kama ni maeneo hayo. Lakini ameshaangalia mbele akaona kuko clear ndo maana akafanya hivyo. Jambo la msingi ni kua na uhakika na unachokifanya.
Inaelekea nawe ni walewale wasioelewa sheria za barabarani na kupelekea majanga ya ajali.
Kwani huoni hapo kuna alama (mistari) ambayo pande zote mbili (anayekuja na anayekwenda) haruhusiwi kuipita gari ya mbele yake (overtake)!?
Watanzania tuna safari ndefu bado.

 
Au lorry lilikuwa limeharibika limepaki ? Na mpiga picha ulikuwa makini na speed ya kasi ya kupiga.

All in all kwa kuangalia tu huenda na hilo lorry halipo kwenye movement hence limepaki mahali hatarishi

Lori liko kwenye mwendo mkuu, huoni kuwa dereva amekanyanga breki kumpisha huyo kilaza?
 
Au lorry lilikuwa limeharibika limepaki ? Na mpiga picha ulikuwa makini na speed ya kasi ya kupiga.

All in all kwa kuangalia tu huenda na hilo lorry halipo kwenye movement hence limepaki mahali hatarishi
Mkuu umeshindwa kuona hilo lorry limefunga break hizo taa za break zinawaka.... Hakuna gari lililopaki hapo
 
Wengi tunaokutana nao Road ni watembeza Magari sio Madereva, kuna Dada yupo Ewura Aliwahi kuniambia amepata Leseni japo hajawahi walau ku sit kwenye Siti ya Dereva hata Mara moja kwenye Maisha yake. Trafick wawe wanafanya zoezi la kustukiza kutambua kama Madereva wanajua alama kuu za Usalama barabarani
Mkuu kwa hilo madereva wengi watafeli, majuzi nilikuwa ofisi ya vehicle inspector kufuatilia mambo flani hivi,walikuja madereva wawili ku-renew leseni zao, wamegeuziwa ukutani kutestiwa zile alama za barabarani hata hawakuambulia tatu.Walirudishwa wakaambiwa wakazisome upya ndo warudi tena.Hao ni sample tu ila wako wengi,na wanapata leseni kwa njia za panya.
 
Naona jamaa wa Lori kafungga breki kabisa, si unaona taa zinawaka kabisa za breki
 
Kitonga hiyo mkuu? naona kama ni maeneo hayo. Lakini ameshaangalia mbele akaona kuko clear ndo maana akafanya hivyo. Jambo la msingi ni kua na uhakika na unachokifanya.

Hiyo ni Ihovi mkuu, huyo pumbavu wa gari ndogo amtafuta huyo dereva Luwinzo bus, amnunulie hata bia mbili tu, lakini iwe jioni baada ya safari!
 
Watu wanashindwa kuelewa maana ya ile mistari barabarani, wanajiendeshea tu...
Kwa hiyo mistari inamaanisha kuwa dereva yeyote haruhusiwi ku-overtake.
Alama za barabarani si lazima hadi trafic awepo, tujiongoze wenyewe...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom