Angalia haya ndiyo matunda ya uhuru bwana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalia haya ndiyo matunda ya uhuru bwana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by engmtolera, Oct 22, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [​IMG]


  Mkazi mmoja wa kijiji cha Mgungira Sengeke Gadala akichota maji kwenye kidimbwi jirani na eneo la shule ya sekondari Wembere kutokana na kukosekana kwa upatikanaji wa huduma ya maji katika kijiji hicho, maji hayo yamekuwa yakitumika kwa matumizi ya kupikia na kunywa.(picha via Mo Blog)

  source: Wavuti - Habari
   
 2. m

  massai JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  alafu unaambiwa tanzania ni nchi yenye neema na iliyobarikiwa sana kwa kuwa na mito, maziwa, mabwawa,maliasili,madini,na amani na utulivu.Sasa mnatakiwa mtulie na mteseke hivyohivyo.Mmekubali mateso mfurahie amani,sasa sijui ndio amani gani tena hiyo
   
 3. M

  Maengo JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Halafu unakuta mjomba katinga suti ya mwarabu anajipongeza, anakenua habari hana kabisa....!
   
 4. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hata Marekani kuna watu wanashindia mlo mmoja. Hatuwezi kusema kuwa Serikali haijafanya chochote tangu uhuru, lakini tatizo ni spidi ya utekelezaji wa mafanikio hayo.
   
 5. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  hebu tukumbushe eneo hilo ni jimbo lipi la uchaguzi na mbunge wake niani????
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Matabaka yalikuwepo hata kabla ya kristo kuzaliwa. Hizo ni changamoto ndogondogo sana.
   
 7. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #7
  Oct 22, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
 8. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Amani mtaipata kwa kua mnaitaka,ila kubalina na mateso mpaka mnaingia kaburini.
   
 9. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Miaka 50 ya UHURU hiyo!!! Eti "Tumejaribu.. tumeweza... na tunasonga mbele!!!" Full Kichefuchefu!!!!....
   
 10. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  dah! hawa magamba kwa propaganda ndiyo wenyewe, eti tunasonga mbele kumbe ni waongo...
   
 11. S

  Sting007 JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Tatizo Watanzania tumeridhika na umasikini tulionao, na tutaendelea kuwa masikini na fukara kwa matatizo ambayo tunaweza kuyatatua sisi wenyewe.
   
 12. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #12
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  tena eneo lenyewe tunaelezwa ni jirani na shule ya sekondari,sijui hata hao walimu na wanafunzi wanaishi vipi mazingira hayo,tunahitaji kuboresha maeneo ambayo tunaona ni ya msingi kwa maisha ya binadamu

  sio kwamba srikali haijafanya kitu la hasha imefanya mengi sana tena sana lakini pale tunapoona panaweza kufanyiwa kazi lakini watu wakaleta uzembe ni lazima tusema

  ni imani yangu kuwa hilo eneo watertable yake ipo karibu sana kiasi kwamba kama serikali ingeamua hata kuchimba kisima kimoja tu ingewezekana kina mama wanaopata tabu ya kutafuta maji umbali mrefu na watoto mgongoni kadha hiyo ingeisha

  naishukuru serikali kwa hapa tulipo,ingawaje hatukutakiwa twe hapa bado tunakazi yakufanya
   
 13. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  hawa ndio mabango yanayotakiwa siku ya uhuru
   
 14. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,226
  Trophy Points: 280
  Sitashangaa kusikia mbunge wake yupo Dar siku zote kikazi.
   
 15. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa sababu USA kuna wanaoshindia mlo mmoja ndo kiwe kigezo cha kuhalalisha udhaifu wenu wa kiuongozi?
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mwita25 kusoma umesoma lakini bado mpumbavu wala si mjinga .Wako wanao kunywa maji kama hayo ? Maana unaogelea US ipi ? Wazungu katika kujipanfa wali hakikisha kwamba watu wao ambao hawana uwezo wanapata senti ama wana access na nguo , chakula na mahali pa kulala .Ingia supermarkets utaona zina bei tofauti na vyakula ni vile vile vina standard sawa .Unaamua uende wapi kulingana na pesa yako.Hata maduka ya nguo ni hivyo hivyo .Uongo upi utaka kusema ? Marekani ipi mzee wengine tumekaa huko sana wala si kwenda UN na kurudi .
   
 17. G

  GAGAGIGIKOKO Senior Member

  #17
  Oct 22, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni sisi wenyewe wananchi kutoukataa mfumo huu dhalimu!!! Bila majority kujitoa mhanga dhidi ya hawa vibaraka,tutabaki kulalama tu.Hawa ******* wana -take advantage sana wanapoona tunanungunika tu bila kuwakabili kivitendo! Tunahitaji kubadilika sana!
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Atakayesema kuwa serikali haijafanya chochote tangu uhuru huyo ni muiongio namba moja. Haya yote tunayoyashuhudia hii leo (kazi ni kwako kupima kama ni mafanikio ay kufeli) yamefanywa na serikali yetu hii tukufu
   
 19. only83

  only83 JF-Expert Member

  #19
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mawazo yako ni ya kijinga,kizembe,kipumbavu sana...hivi mateso ya watanzania ni changamoto ndogondogo? watu wanakufa kwa magonjwa ya kuhara ni changamoto ndogondogo? Acha kuleta siasa mavi kwenye mambo ya msingi mkuu...
   
 20. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #20
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  nadhani tusifananishe Tanzania na marekani ila itakuwa sawa kabisa kama tutafananisha Tanzania na China,kwani ktk miaka ya hivi karibuni tulikuwa nao swa kiuchumi na mambo mengine na hata ilitokea wakati Mwl Nyerere aliwahi wapa wachina msaada wa chakula lakini tuangalie wapo wapi kwa sasa,nini kimewafanya wawehapo walipo wakati tulikuwa kuwa nao sawa

  pia tujilinganishe na Philipines hii nchi tulikuwa nayo ktk nchi masikini lakini wenzetu wanasimamia malengo na wanafika pale wanapopataka,tuiangalie kwa kagame tusijifanye hatuoni kagame ndio anaondoka hivyo tutabaki tukilalamika na kutolea mifano tu,

  wakati wenzetu wanakimbia sisi tumekaa,ahadi nyingi kwa wapiga kura wetu zisizotekelezeka,ni kama tunakomoana vile,

  narudia tena kuwa serikali imefanya mambo mema mengi sana lakini hatukutakiwa tuwepo hapa tulipo,sijui kama mnaelewa kuwa Tanzania ni namba moja kwa kuzalisha Tanzanite lakini wauzaji wakuu ni S.Africa na pia Tanzania ni ya tatu kwa uzalishaji wa Dhahabu Africa lakini bado watu wetu wanakosa hata visima vya futi 12,wapi tunakokwenda?
   
Loading...